Thursday, September 4, 2014

MWANAUME: DALILI ZA MWANAMKE ANAYEKUPENDA JAPO HAJAKWAMBIA NI HIZI!

1 KUONGEA NA KUKAA MUDA MWINGI NA WEWE
Kama msichana anakupenda hatoichezea nafasi ya kukuona, kukaa na kuongea na wewe. Siku zote atatafuta nafasi ya kuongea au kukuona. 
Unapoongea naye anakuwa makini kukusikiliza na hufurahi kila unachokiongea hata kama hakifurahisha.

2 ATAKUPA MAWASILIANO YAKE 
Hawezi kukunyima namba ya simu kwa mara ya kwanza hata kama ni siku ya kwanza mmeonana.

3 ATAKUTAMBULISHA KWA NDUGU NA RAFIKI ZAKE
Hajali wengine wakimtazama wanapomuona yupo nawe. Atakutambulisha kwao bila kujali chochote. 

4 WIVU 
Anajisikia wivu anapokuona na wasichana wengine. Unachart nao ukiwaita majina ya kimapenzi.

5 ATAKUMBUKA SIKU ZAKO MUHIMU
Atajitahidi kukumbuka siku yako ya kuzaliwa na hata akakuletea zawadi. 
Akishagundua kitu cha pekee ulichokuwa ukikitarajia umekifanikisha kama kufaulu mtihani au kupata kazi haraka sana atajitahidi kukupongeza.

5 MAENDELEO YA BAADAYE 
Hupenda kuongelea maendeleo yake ya baadaye na kukujumuisha katika hayo. Yupo tayari hata kukushirikisha ndoto zake.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI