Tuesday, September 16, 2014

MAGONJWA YA MOYO BADO NI MIONGONI MWA MAGONJWA YANAYOCHANGIA VIFO VINGI TANZANIA

KWA MUJIBU wa takwimu za Shirika la Afya Duniani, WHO zilizotolewa mwaka 2011, Vifo vilivyotokana na magojwa ya moyo nchini Tanzania  vilifikia idadi ya watu 19,083, au asilimia 4.33% ya idadi ya vifo vyote. Na takwimu hizo zilionyesha idadi ya wanaofariki ni watu 117.64 kati ya watu 100,000, na takwimu hizi zikiiweka Tanzania katika nafasi ya 87 ulimwenguni.
Magonjwa haya ya moyo yanasababisha vifo vipatavyo idadi ya watu milioni 12 kwa mwaka duniani kote. Hata hivyo shirika la Afya Duniani limekua likifanya jitihada za lazima za kujaribu kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya moyo na sababu zinazochangia kuongezeka kwa vifo hivyo.
 Magojwa haya ni pamoja na ugonjwa wa moyo, kiharusi, shinikizo la damu , ugonjwa wa pembeni wa mishipa ya moyo, , ugonjwa wa moyo wa kuzaliwa na moyo kushindwa kufanya  kazi ipasavyo.  Katika kuonyesha kukua kwa  maendeleo ya kiteknolojia ya huduma za afya, Hospitali ya Apollo ya mjini  Gujarat , katika mji wa Ahmedabad, ilifanikiwa kufanya upasuaji unaojulikana kitaalam kama  ‘Bentall Surgery’ kwa mwanamke aliyekuwa na zaidi ya miaka 50. Upasuaji wa aina hii mara nyingi ni adimu kufanyika katika nchi ambazo ni masikini na zenye wataalamu wachache, ama zenye mfumo wa chini  wa huduma za afya. Upasuaji huu uliofanywa kwa mwanamama kutoka Tanzania, uliukuwa ni wa aina yake, na ulichukua muda wa saa saba. Hii inaonyesha jinsi gani hospitali hizi zilivyo na uwezo na utaalam wa hali ya juu.
Mama huyo alikuwa akilalamika toka maka 2009 kuhusu maumivu ya mgongo, na alipofanyiwa uchunguzi wa kina, ilionekana kuwa alikua na matatizo katika moyo wake, ambayo hata hivyo hayangeweza kutibiwa hapa nchini. Alipelekwa katika hospitali ya Apollo ya mjini Ahmedabad, hospitali inayosifika kwa kufanya upasuaji kwa ufasaha na uhakika zaidi.
Mama huyu alifanikiwa kufanyiwa upasuaji huo mgumu wa moyo uliochukua zaidi ya masaa saba, ilionekana kuwa alikua na matatizo makubwa katika mishipa ya Aorta ambayo yalisababisha moyo wake ushindwe kufanya kazi kama kawaida. Hatimaye upasuaji huo ulifanikiwa, na pengine asingeweza kupona kama bado angelikuwapo nchini hapa, na hali yake inaendelea vizuri.
“ katika masuala ya afya, bara la Afrika liko kama bara la Asia miaka 25 ama 30 iliyopita. Wale tu wenye kipato cha juu ndiyo wanaoweza kumudu huduma za uhakika nje ya nchi’’,  Anasema Dr Hari Prasad, mkurugenzi mtendaji wa hospitali za Apollo.
“Ni wakati muafaka sasa wa kutumia uwezo wetu na utaalam wetu kuwatibu wenye matatizo. Tulichoifanyia india hatuna budi kuifanyia dunia na nchi zinazoendelea, Anaongezea Dr Pratap C Reddy, mwenyekiti wa hospitali wa za Apollo

Mbali na Tanzania, Hospitali ya Apollo imepania kukita mizizi yake katika nchi mbalimbali za Afrika , ambako imekua ikipokea idadi ya wagonjwa wengi kutoka bara hili, na ina matarajio ya kuanzisha vituo kadhaa vya Afya katika eneo la Afrika ya Mashariki na Afrika magharibi hapo mbeleni.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI