Tuesday, September 30, 2014

CHAMA KIPYA CHA ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY ‘ACT’ CHAPOKEA WANACHAMA WAPYA

 
Mwanachama wa zamani wa CHADEMA, Batuli Abdallah  akijieleza mbele ya wanahabari (hawako pichani)
 
 Yassin Bahama aliyekuwa mwanachama wa zamani wa Chadema akizungumza.
 
Mohamed Ngulangwa aliyekuwa mwanachama wa zamani wa CCM akivaa fulana ya chama hicho.
 
Wajumbe waliohudhuria mkutano.
 
Mwenyekiti  wa ACT,  Hamis Chambuso akiwa ameshika kadi za Chadema zilizorudishwa na wanachama hao wapya.
 
Wajumbe na wanahabari wakiwa mkutanoni.

CHAMA cha siasa hapa nchini cha Alliance for Change and Transparency ‘ACT, leo kimewapokea wanachama wapya ambao wamehama toka vyama mbalimbali vya siasa nchini.

Waliopokelewa ni  Yassin Bahama aliyekuwa mjumbe wa serikali ya mtaa wa matofalini,  Ujiji Kigoma, Batuli Abdallah aliyekuwa Katibu  Mwenezi Bavicha katika Jimbo la Kawe, Ofisa na mwasisi  wa chama cha Chauwa,  Sylvester Kasonga pamoja na Engineer Mohammed Ngulangwa toka Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza  mbele ya GPL, eneo la Msasani Club, jijini Dar, Mwenyekiti  wa Mkoa wa ACT, Hamis Chambuso amewakaribisha na kuwapongeza  wanachama hao wapya kwa hatua waliyoichukua.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI