Sunday, August 17, 2014

VAN GAAL ASEMA KIPIGO CHA JANA KITAPOTEZA KUJIAMINI MAN UNITED, AKIRI PIA IPO HAJA YA KUSAJILI



Louis van Gaal akiondoka uwanjani jana baada ya Manchester United kuchapwa na Swansea.
*********
KOCHA Louis van Gaal amesema kwamba kujiamini kwa Manchester United itaondoka baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-1 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya England nyumbani mbele ya Swansea.
Bao la Gylfi Sigurdsson dakika ya 72 lilimvuruga kocha mpya wa United, Van Gaal kuftia ushindi mfululizo katika mechi sita za kujiandaa na msimu, Mashetani hao Wekundu wakifungwa kwa mara ya kwanza nyumbani katika mchezo wa ufunguzi ndani ya miaka 42.
"Unaposhinda kila kitu katika wakati wa maandalizi na kuja kufungwa mechi ya kwanza, hiyo haiwezi kuwa mbaya," amesema. 
"Tumejijengea hali ya kujiamini kwa kiasi kikubwa na kisha itaondoka kwa sababu ya matokeo haya,".’ 
Mholanzi huyo alilazimika kuwachezesha kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya England Jesse Lingard na Tyler Blackett, akiwa amesaini wachezaji wawili tu wapya— Ander Herrera na Luke Shaw msimu huu.
Alipoulizwa kama kipigo hicho kitamlazimu kuingie sokoni kusajili kuboresha kikosi, Van Gaal alisema: 
"Nilifikiri hivyo mkabla ya mechi hii, hivyo hakuna tofauti. 
Wakati tunacheza Marekani niliona kama hivyo. Kweli tunahitaji mabeki. Lakini huwezi kusema hivyo, kwa sababu tumepoteza mechi moja na tumeshinda nyingine zote, hiyo ni beki. Ni timu ambavyo tumecheza,".
Katika staili yake maarufu, Van Gaal, Mholanzi hiyo hakumnyooshea kidole yeyote baada ya mechi. 
Kocha huyo mpya wa United, aliwalaumu wachezaji wake kwa kucheza ovyo. Pia alisema walikosa hali ya kujiamini na hawakucheza kitimu.
"Ni siku mbaya sana kwetu. Imewaangusha sana wachezaji, mashabiki, mimi, na viongozi,"alisema. 
Na Bin Zubeiry

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI