Saturday, August 2, 2014

AZAM YAILIPA SIMBA SC MILIONI 60 USAJILI WA KAPOMBE, MNYAMA NAYE AKILIPA KITUO CHA MOROGORO MILIONI 9

Makamu wa Rais wa Simba SC, Geofrey Nyange 'Kaburu' (kushoto) akimkabidhi hundi kiongozi wa Morogoro Youth Football Academy
SHOMARY Kapombe alishakamilisha usajili wake wa kujiunga na mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc na ataitumikia klabu hiyo msimu ujao wa ligi kuu na ligi ya mabingwa barani Afrika.
Kapombe alisajiliwa na Azam kutoka klabu ya AS Cannes ya Ufaransa ambapo aliuzwa na Simba chini ya uongozi wa Ismail Aden Rage.
Katika mauzo ya kapombe, kulikuwa na kipengele cha Simba kupata asilimia kadhaa kama mchezaji huyo atauzwa klabu yoyote duniani.
 ya Kapombe kuuzwa Azam, Simba walitakiwa kulipwa milioni 60 kama mkataba unavyoelekeza.
Kulikuwa na mvutano wa kulipwa fedha hizo, lakini Azam wameamua kumalizana na Simba ambapo jana waliipa klabu hiyo ya Msimbazi milioni 60 baada ya kumnunua Kapombe.
Lingine kubwa zaidi, jana simba imewakabidhi ‘Morogoro youth Football academy’ milioni 9 kama share ya kituo kwa mauzo ya Mchezaji shomari Kapombe.
Wakati simba inamsajili Kapombe kutoka kwenye kituo kulikuwa na makubaliano ya kuwapa 15% on ward sale.
Hiki ni kitendo cha kuigwa na klabu nyingine zenye utaratibu wa kuchukua wachezaji vijana.
Na Mpenja blog

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI