Wednesday, July 30, 2014

TAIFA STARS KUKWEA PIPA KWENDA AFRIKA KUSINI LEO

images
Release No. 132
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAIFA STARS KWENDA AFRIKA KUSINI
Msafara wa watu 27 wa kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars) kinaondoka Leo saa 10 jioni kwa ndege ya Air Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kitapiga kambi ya siku mbili kabla ya kuingia Maputo kuikabili Msumbiji (Mambas).
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager (Julai, na baadaye jioni kuunganisha safari ya Afrika Kusini.
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji itachezwa Agosti 3 mwaka huu Uwanja wa Taifa uliopo Zimpeto nje kidogo ya Jiji la Maputo.
Msafara huo wa Taifa Stars kwenda Afrika Kusini unajumuisha wachezaji 19 na waliobaki ni maofisa wa Benchi la Ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu Mart Nooij kutoka Uholanzi.
Wakati kiungo Mwinyi Kazimoto ametua Julai 29, 2014 nchini kuungana na wenzake, washambuliaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu wao wataungana na wenzao Julai 30, 2014 jijini Johannesburg wakitokea Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
Wakati huo huo, Serengeti Boys imewasili salama jana (Julai 28 mwaka huu) jijini Johannesburg, Afrika Kusini kwa ajili ya mechi ya michuano ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 dhidi Afrika Kusini (Amajimbos).
Mechi hiyo ya marudiano ya raundi ya pili itachezwa Jumamosi, Agosti 2 mwaka huu kwenye Uwanja wa Dobsonville uliopo Soweto kuanzia saa 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Kusini.
Timu hizo zilitoka suluhu katika mechi ya kwanza iliyofanyika Julai 18 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam. 
Serengeti Boys inahitaji ushindi kwenye mechi hiyo au aina yoyote ya sare ya mabao ili ifuzu kwa raundi ya tatu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI