Sakata la Michael Wambura kuondolewa kwenye kinyang’anyiro za uchaguzi wa mkuu wa Uraisi wa klabu ya Simba SC leo limefikia tamati.
Kamati ya rufani ya shirikisho la soka Tanzania, TFF, imetengeu maamuzi ya kamati ya uchaguzi wa klabu ya Simba SC wa kuliengua jina la mgombea wa Urais wa klabu hiyo, Micheal Richard Wambura.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, wakili Julius Mutabazi Lugaziya amesema mchana huu katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa mikutano wa TFF, jijini Dar es salaam kuwa kamati yake ilikaa juzi na jana na kufikia maamuzi ya kutengua maamuzi ya kamati ya uchaguzi ya Simba chini ya mwanasheria, Dkt. Damas Ndumbaro kwasababu klabu hiyo ilikiuka kanuni ilijiwekea yenyewe kwa mujibu wa katiba.
Lugaziya amesema kuwa uamuzi wa kumrudisha Wambura umeangali zaidi busara kwasababu Simba ilikiuka katiba yake kwa kumuacha mwanachama aliyesimamishwa kuendelea kufanya shughuli za klabu, na kama akiondolewa basi katiba na kamati ya uchaguzi vyote vitakuwa batili.
“Tangu aliposimamishwa, muomba rufani (Wambura) hajawahi kuchukuliwa kama mtu aliyesimamishwa. Kwanini?, kupoteza haki za uanachama ni pamoja na kupoteza haki za kulipa ada, haki za kushiriki mikutano, haki ya vikao vya maamuzi na haki ya kuteuliwa katika vyomvyo mbalimbali vya Simba SC”. Alisema Wakili Lugaziya.
“Tangu kutangazwa kusimamishwa, amekuwa akishiriki shughuli za Simba. Amekuwa akishiriki mikutano yote mikuu na dhararu, ikumbukwe kuwa mwanachama halali tu ndiye anatakiwa kushiriki mikutano hiyo na mwanachama ambaye amesimamishwa hatakiwi kushiriki, lakini tangu kutangaza kusimamishwa, Wambura amekuwa akishiriki”. Alifafanua Lugaziya.
“Kubwa zaidi, mpaka sasa Wambura ni mjumbe wa kuteuliwa wa kamati ya utendaji ya Simba na alishiriki katika mikutano ya katiba pamoja na kushiriki kuiteua kamati ya uchaguzi”. Wakili huo aliongeza kuwa kama mtu batili ameshiriki kufanya maamuzi, basi maamuzi nayo ni batili. “Wambura alishiriki katika mkutano wa katiba na kuiteua kamati ya uchaguzi, maana yake kama Wambura ni batili, basi katiba na kamati ni batili”. Kama tunafikia maamuzi ya kusema katiba na kamati ya uchaguzi ya Simba si halali, kwasababu mtu batili alishiriki, athari yake ni kubwa. Kamati alishasema huko nyuma kwamba Simba ilikuwa inamchukulia Wambura kama mwanachama”. Alisema Lugaziya.
0 comments:
Post a Comment