Saturday, June 28, 2014

AFYA YA JACK PATRICK YATETEREKA GEREZANI

UNAWEZA sema ni majanga juu ya majanga yanazidi kumkumba modo wa Bongo, Jacqueline Patrick ‘Jack’ baada ya wiki iliyopita kushindwa kupanda kortini kufuatia kutetereka kwa afya yake bila ufafanuzi wa kina.
Mbali na kuwa na afya tete, pia Jack anadaiwa kulalamikia haki za msingi za kibinadamu ambazo anazikosa mahabusu kwa kuishi maisha kama ya mtu aliye kifungoni.
Mtu mmoja anayejitolea kumpa msaada na kumtembelea Jack mahabusu, Macau, China alikoshikiliwa, Matilda alisema Jack anaumia kwa kupewa maisha kama tayari amehukumiwa, anaona bora hukumu yake ipite ajue moja.
“Kiukweli Jack anaumwa, alishindwa hata kwenda mahamani, mbaya zaidi hata wakili wake naye hakutokea siku hiyo.
“Halafu kule mahabusu anafanyishwa kazi ngumu ambazo hastahili kama mahabusu na amesema hata watu wake wa karibu ambao anaamini kwa kipindi hiki wangekuwa wanampa faraja hawaoni, anatamani angekamatiwa Bongo labda kuna watu wanapenda kwenda kumtembelea kule Macau lakini hawana uwezo.
“Wabongo wengi ambao wako Macau kwa ajili ya sanaa ya sarakasi ndiyo kidogo wanakwenda kumtembelea siku mojamoja,” alisema Matilda.




Chanzo: Amani

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI