Monday, April 7, 2014

NCHIMBI MGENI RASMI TAMASHA LA PASAKA SONGEA

ALIYEKUWA Waziri wa Mambo ya Ndani, Emmanuel Nchimbi anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Aprili 26 Wilayani Songea mkoani Ruvuma.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama wakazi wa mkoa huo na maeneo ya jirani wajitokeze kwa wingi kufanikisha sherehe ya kufufuka kwa mwokozi Wetu Yesu Kristo.
Msama alisema mbali ya Nchimbi kuwa mgeni rasmi Songea, jijini Mbeya mgeni rasmi atakuwa ni Mbunge wa viti maalum, Mary Mwanjelwa wakati mkoani Dodoma mgeni rasmi atakuwa mbunge wa Tarime, Nyambari Nyangwine. Aidha Msama alitoa fursa kwa wakazi wa mikoa litakapofanyika Tamasha la Pasaka kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha ufanikishaji wa ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha wenye uhitaji Maalum cha Jakaya Mrisho Kikwete rafiki wa Wasiojiweza.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI