Sunday, April 13, 2014

BREAKING NEWS: HELIKOPTA ILIYOANGUKA DAR ASUBUHI APRIL 13 IKIWA NA VIONGOZI

Screen Shot 2014-04-13 at 1.55.22 PM
Hitilafu ilisababisha helikopta kuanguka wakati ikipaa kuwapeleka kwenye maeneo mbalimbali yaliyoathirika na mvua zinazoendelea kunyesha ambapo hata hivyo walinusurika kifo isipokua majeraha madogo madogo tu.
Screen Shot 2014-04-13 at 1.55.45 PM
Screen Shot 2014-04-13 at 1.55.53 PM
Screen Shot 2014-04-13 at 1.55.08 PM
HELIKOPTA iliyokua ikiwasafirisha Makamu wa Rais Dr. Gharib Bilal, waziri wa ujenzi John Magufuli, Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick imepata ajali asubuhi wakati ikipaa kutoka uwanja wa ndege Dar es salaam. (kwa mujibu wa mashuuda)
Taarifa zilizotoka muda mfupi baadae zimeeleza kupata majeruhi lakini hakuna yeyote aliepoteza maisha baada ya Helikopta hiyo kuanguka wakati ikianza safari kuwapeleka viongozi hao kutembelea maeneo yaliyoathirika na mafuriko.
Wote walitoka salama na majeraha madogomadogo ambapo pia kwenye taarifa nyingine iliyotolewa na TBC, wameendelea na ziara ya kutazama athari za maafuriko kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo Pwani.
Ajali hii ya Helikopta imetokea siku moja baada ya ndege ya shirika la ndege la Kenya kubamiza chini na kuharibu upande wa kulia wa bawa kutokana na ukungu mkubwa uliokuwepo kwenye uwanja wa ndege Dar es salaam wakati ikitua kutokea Nairobi, hakuna aliepoteza maisha ila waliojeruhiwa wakati wa kushuka kwa dharura kutoka kwenye ndege.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI