NDEGE 9 za kijeshi na Moja ya kiraiya zinatafuta mabaki ya ndege ya Malaysia ya MH370.
Maafisa wanaosaidia katika harakati za kuitafuta ndege ya Malaysia ya MH370 iliyopotea majuma tatu yaliyopita , wametangaza kuwa wanabadilisha eneo la kuitafuta mabaki ya ndege hiyo.
Eneo hilo jipya litakuwa kilomita elfu moja mia moja kazkazini mashariki mwa kusini mwa bahari hindi.
Mamlaka ya usalama wa baharini nchini Australia imesema kuwa hatua hiyo inatokana na taarifa muhimu na utafiti wa Malaysia pamoja na matokeo ya utafiti wa rada ya ndege hiyo iliyotoweka.
Eneo inakotafutwa ndege ya Malaysia.
Ndege hiyo iliyotoweka March tarehe 8 ikiwa na abiria 239 sasa inadaiwa kwamba ilikuwa katika mwendo wa kasi kinyume na ilivyokadiriwa na kwamba huenda iliishiwa na mafuta ghafla.
Meneja mkuu wa shirika la utafiti wa anga za juu ya Australia John Young, amesema utafiti mpya unaonesha kuwa ndege hiyo ya MH370 ilikwea juu na kufululiza kwa kasi mno na hiyo inaweza kuwasababu ya mafuta ya ndege hiyo kumalizika haraka.
Kutokana na hesabu hiyo mpya eneo la kutafutwa kwa ndege hiyo imehamishwa hadi umbali wa kilomita 1,850 Magharibi mwa Perth na itakuwa katika eneo lenye kilomita 319,000 mraba katika bahari Hindi.
Chanzo: BBC
0 comments:
Post a Comment