Monday, March 24, 2014

COASTAL UNION YAMLETEA MAJANGA MESSI



HASIRA katika mchezo limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa siku za hivi karibuni hasa ukizingatia watu wamekuwa wakiweka kinyongo baada ya kushindwa katika mechi wanazocheza.


Hili limetokea mara nyingi katika pande zote, kwa upande wa mashabiki lakini pia kwa wachezaji, hasa pale timu zao zinaposhindwa na timu pinzani, kwani tumeshuhudia mashabiki wakivunja viti katika viwanja mbalimbali, lakini pia wakitupa chupa na ghasia nyingine kadha wa kadha.

Jambo hili pia limetokea kwa kiungo mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Yahaya Singano ‘Messi’ ambaye alivunja vioo vya mlango wa uwanja wa Taifa mara tu baada ya mechi yao dhidi ya Coasal Union kumalizika.


Katika mechi hiyo, Simba walilala kwa bao 1 - 0 na Messi alipoteza nafasi safi katika dakika ya 90 baada ya kubaki yeye na kipa lakini akashindwa kufunga.

Hali hiyo ilionyesha kumchanganya na wakati anaingia vyumbani aliupiga teke mlango na kuvunja vioo.
Eneo la mlango uliovunjwa
Kutokana na hali hiyo, askari waliingia na kutaka mumtia nguvuni, lakini Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga alijitokeza na kuanza kuzungumza nao.

Baada ya mazungumzo hayo ya dakika kadhaa wakiwa na Kamwaga, askari walionyesha kuiiondoa katika jambo hilo.


Mmoja wa askari hao alisema wameliacha jambo hilo mikononi mwa Simba na uongozi wa uwanja wa Taifa na kitu kizuri kwao, aliyevunja mlango huo anajulikana.

Tujaribu kuzituliza hasira zetu pale linapokuja suala la ushindani, kwani michezo ni furaha na amani.

0 comments:

Post a Comment

ZILIZOSOMWA ZAIDI