NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Monday, July 6, 2015

MWANAMUZIKI JIDE ALA BATA CHINA HUKU NYUMBA YAKE AKIPIGWA MNADA BONGO

Deogratius Mongela na Chande Abdallah
GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini Hong Kong, China akila bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.

Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi kutopatikana.

Wakati gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.

Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.

Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa mnada.
#GPL

YEMI AELEZA SABABU YA KUWASHAMBULIA WAANDAJI WA TUZO ZA BET

Mwimbaji maarufu wa Nigeria, Yemi Alade.
Lagos Nigeria
BAADA ya mwimbaji maarufu wa Nigeria, Yemi Alade, maarufu kama  Jonny Crooner kutokana na wimbo wake, kushindwa katika mpambano wa Tuzo za BET nchini Marekani, amewashambulia waandaji wa mashindano hayo kwamba hawakuwafanyia haki waimbaji kutoka Afrika.
 
“Kusema ukweli Waafrika hatutendewi haki kama wenzetu kutoka mabara mengine,” alisema mwimbaji huyo mrembo akisisitiza kwamba hakusema hivyo kwa vile hakupata tuzo yoyote kwenye mashindano hayo.
Aliongeza kwamba iwapo atachaguliwa tena kushiriki BET, hilo anamuachia Mungu ambaye ndiye Hubariki na si binadamu.  Iwapo Mungu ataendelea kunibariki, hakuna awezaye kulizuia jambo hilo.”

WAFAHAMU NAVY KENZO (@NAVYKENZO) FROM TANZANIA

Navy Kenzo is Tanzanian afro pop/dance duo consisting of Aika – female singer/rapper and Nahreel – singer/ major award winning producer from Tanzania. Navy Kenzo is signed under the label of “The Industry Studios” founded by Nahreel that works with major Tanzania artists like Vanessa mdee, Diamond Platinumz, Joh Makini etc.
 Aika and Nahreel met in India 2008 while studying their degrees. In 2011, back to Tanzania, the duo joined a group called Pah One, but left and in April 2013, the two formed their own group called Navy Kenzo, the group started building a local buzz through their shows and radio plays with a major hit song called chelewa/bokodo which was on top of the charts and gained popularity within East Africa and beyond their good songs are since breaking through major chats and televisions like soundcity, Wbs, NTV and radios like the beat fm, naija fm, so on. With the success to break through the music market, the two have been able to bring more musical and even unique rhythms to their fans and market as well.
 Navy Kenzo has been nominated as best group of the year two times at the kilimanjaro music awards Tanzania.
According to them, success is built by art of mind and hard work, the two have accomplished so much in short time because they are willing to keep breaking the walls.
Instagram: @navykenzooffial
Facebook: Navy Kenzo
Twitter: @navykenzo
Youtube: NavyKenzoVevo
Recent releases:
Moyoni
I just wanna love you
Viza ft Young Dee
Collabos
Safari – Nikki wa pili ft navy kenzo & joh makini,Vanessa Mdee, gnakko & jux
 Nomination
2013-2014 best group of the year – Kilimanjaro Music Awards – KTMA
2014-2015 best group of the year -Kilimanjaro Music Awards – KTMA
          MANAGEMENT/BOOKINGS:
           Paschal (Navy Kenzo Manager)
                      +255 765 332 134
                   navykenzo@gmail.com
           Marion (Navy Kenzo Publicist)
                      +255 782 481 971
                   theindustrytz@gmail.com

STAN BAKORA AFUTURU SAA KUMI...KWEUPEEEEEEE...PEEEE!!!!! *VIDEO*

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kuna marafiki wako tayari kukuharibia Swaumu yako, mcheki STAN BAKORA hapa..


BI HINDU AULA....! ACHAGULIWA KUWA KIONGOZI SIMBA SC.





Mtangazaji wa 100.5 Times fm Bi Chuma Suleimani a/k/a Bi Hindu ameteuliwa kuwa Mwanamke pekee katika Baraza jipya la wazee la klabu ya wekundu wa msimbazi Simba SC lililotangazwa na kamati ya utendaji ya Simba.

Bi Hindu anaungana na wazee wengine wa kipindi tangu Simba inaitwa Sunderland, Omary Mtika (Mwenyekiti), Ally Hassan, Abdulsharif Zahoro na Omary Moshi.
Akizungumzia uteuzi huo Bi Hindu ambaye husikika kila siku za Jumatatu – Alhamis saa sita mchana mpaka saa kumi kwenye kipindi cha Mitikisiko ya pwani (Timesfm), amesema kuwa amefurahia uteuzi huo na ameahidi kuendelea kujitolea kwa mapenzi yake yote kuijenga klabu hiyo.
“Aveva ana busara na akili ameona haitowezekana kuendesha jambo peke yao bila ya wakongwe ambao wapo ndio kama sisi tuloitumikia kitambo, nawapongeza sana Mwenyezi Mungu awabariki sana na nafurahi sana lakini kubwa akili zao nafuu zao na raha yangu mimi Tukutane Oktoba”, alisema Bi Hindu.
Uteuzi wa Bi Hindu pamoja na wazee wengine umekuja mwaka mmoja tangu uongozi mpya wa Simba chini ya Rais Evans Elieza Aveva uingie madarakani mwezi june mwaka 2014.
Hongera sana Bi Chuma Suleiman Bi Hindi Bibi wa Mcharazo wa Bi Mkubwa kwa hatua hiyo.


Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ


Copy and WIN : http://ow.ly/KNICZ

KIM KARDASHIAN AMPA KAMPANI DADA YAKE

Mwanamitindo ambaye kwa sasa ni mama kijacho, Kim Kardashian.
New York, Marekani
MWANAMITINDO ambaye kwa sasa ni mama kijacho, Kim Kardashian hivi karibuni ameonyesha upendo wa hali ya juu baada ya kutoka ‘out’ na mtoto wa dada yake, Kourtney Kardashian, Mason Disick ambaye kwa sasa yuko katika kipindi kigumu baada ya kumwagana na mzazi mwenzake, Scott Disick.

Kim alionekana sehemu mbalimbali za mitaa ya New York akiwa na Mason pamoja na mwanaye North, ambapo iliripotiwa kuwa wikiendi hiyo Kourtney ambaye pia ni mwanamitindo aliutumia muda mwingi akiwa nyumbani kwake Las Vegas na wanae wengine,  Reign na Penelope.

BREAKING NEWS: MRAMBA, YONA KWENDA JELA MIAKA MITATU


 Mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam imewahukumu kwenda jela miaka mitatu aliyekuwa waziri wa zamani wa fedha Basil Mramba,na aliyekuwa Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona baada ya kukutwa na hatia ya uhujumu uchumi, matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia serikali hasara ya sh bilioni 11.7.
Endelea kufuatilia taarifa zetu kufahamu zaidi.
#ITV

ZILIZOSOMWA ZAIDI