NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Monday, March 31, 2014

MHE. MWIGULU NCHEMBA AMVALISHA SKAFU YAKE MWIMBAJI WA INJILI BAADA YA KUGUSWA NA NENO LA MUNGU

Mh:Mwigulu Nchemba alivutiwa na Uimbaji wa Kijana huyu Daniel Thomas na Kuamua Kumvisha Skafu yake ya Bendera ya Nchi yetu.Lilikuwa ni tukio la Kuvutia lililovutia Wengi sana na Kuamsha nderemo na Vifijo kwenye Uzinduzi wa Albamu hiyo.
HATIMAYE Shughuli Nzima imemalizika Salama na Kwa Maombi Makubwa ili kituo kile cha Watoto Yatima kikapate Kusimama na Kutumika Sawasawa na Mapenzi ya Bwana.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh:Mwigulu Nchemba hii leo ameshiriki ibada ya Uzinduzi wa Albamu ya Nyimbo za Injili za Mwimbaji Rehema kutoka Rukwa iliyofanyika Victory Church Ubungo-External.Mbali na Ufunguzi huo Mh:Mwigulu Nchemba amechangia Zaidi ya Milioni 10 Kwaajili ya Ujenzi wa Kituo Cha Watoto Yatima huko Rukwa kitakacho Simamiwa na Mwimbaji Rehema.
Mh:Mwigulu Nchemba ameomba Watanzania kushikamana na kuasaidiana katika Shida,Kujali na Kuwatunza Watoto Yatima.
Pia Mwigulu NChemba ametumia nafasi hiyo Kuwasihi Washarika,Wachungaji na Maaskofu Kuendelea Kuliombea Taifa hili kipindi hiki cha Bunge la Katiba.
Amewasihi Wananchi waache Kuangalia Vyama vya Siasa,Waangalie hoja na sio nani Katoa hoja.
Watu Wanataka Kutumia Mwanya wa Uundaji wa Katiba Mpya kupitisha Mambo yatakayo ligawa Taifa sikuza Usoni,Hivyo ni dhahiri Kila Mjumbe wa Bunge la Katiba ni lazima akubali Kuwa Muwazi kwa Watanzania waliomtuma Kushiriki kazi ya Kutunga Katiba Mpya,Kitendo cha Kufanya Mambo kwa Siri ni Kuwanyima Watanzania haki yao ya Kujua kile walichowatuma Wajumbe pale Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha(Uchumi) na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Mh:Mwigulu Nchemba akikata Utepe na Kuzindua rasmi Albamu ya Nyimbo za Injili Zilizoimbwa na Bi.Rehema.Tukio hili limefanyika Victory Church Mabibo External hii leo Tar.30/03/2014.Bi.Rehema amezindua Albamu yake ya pili.Mwaka 2012/12 aliachia Albamu ya Kwanza iliyozinduliwa na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda huko Rukwa.
Bi.Rehema akishukuru Kwa Mgeni Rasmi kwa tendo la Kuzindua Albamu yake Rasmi aliyoielekeza kwenye Ujenzi wa Kituo Cha Watoto Yatima Wilayani Rukwa.
Bi.Rehema akiingia kuzindua Albamu yake ya Pili Tangu aanze Kuimba nyimbo za Injili.
Naibu Waziri wa Fedha Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Washarika waliofika kwenye Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
Mchekeshaji Kutoka EATV Comedy akiimba Wimbo wake wa Kumsifu yesu,Kwa sasa Msanii huyu anafanya Kazi ya Kutangaza Injili Kupitia Nyimbo za Kumtukuza na Kumsifu Yesu.
Mh:Mwigulu Nchemba akicheza kwaKusifu Utukufu wa Mungu kwa Pumzi tunayoendelea Kutumia.Ni Kwa Neema tu.
Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba akimpongeza Mme Wake Mara baada ya Kucheza pamoja na Vijana wa Bi.Rehema wakati wa Kumsifu Mungu.
Sehemu ya Washarika waliofika Kushuhudia Tendo Kuu la Uzinduzi wa Albamu ya Bi Rehema hii leo hapa External Mabibo.
Mh:Mwigulu Nchemba akisisitiza Washarika na Makanisa yote Kushikamana Kuombea Taifa katika Kipindi hiki cha Bunge Maalumu la Katiba,Mwigulu amesema hiki ni Kipindi Kigumu sana kwa Taifa letu,Katiba Inatungwa kipindi amacho Dunia imechafuka kuna mambo mengi yasiyo na tija kwa Taifa tunahitaji Kuungana kuyazuia.Hivyo lazima tukio la Utunzi wa Katiba liwe la wazi,Kufichaficha Mambo kwa Siri ni hatari sana,hakuna haja ya Kujificha wakati tuliopo Bungeni wote ni Wawakilishi wa Wananchi hivyo Wananchi Mnahaki ya Kupata kile tunachokisimamia Bungeni.
N/Waziri wa Fedha(uchumi) Mh:Mwigulu Nchemba akikabidhi Mchango wake kwa Bi.Rehema mara baada ya Kuzindua Albamu ya Mtumishi wa mungu huyu.Fedha hizi zinakwenda Moja kwa Moja kwenye Ujenzi wa Kituo cha Watoto yatima huko Mkoani Rukwa.
Bi.Rehema akishangilia na Kuuonesha Umma Mchango wa Mh:Mwigulu Nchemba katika Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima huko Rukwa kwa Njia ya Uimbaji.
"Kwa hiki nilichokitoa,Naomba nikawapelekee Marafiki Zangu na Wabunge wa Mkoa wa Katavi hizi CD ili wachangie kwenye Ujenzi wa Kituo cha Watoto Yatima" Mh:Mwigulu.
Mwenye Nguo ya Juu Rangi ya Njano ni Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Ndugu. Beatrice Mwaipaja akijumuika Kwenye Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
Masanja wa EATV akiendelea Kuburudisha kwa Kumsifu Yesu kupitia Nyimbo zake.
Mwimbaji Daniel Thomas akiimba wimbo wake wa "IBADA NJEMA HUANZIA NYUMBANI" wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Bi.Rehema.
Mh:Mwigulu Nchemba alivutiwa na Uimbaji wa Kijana huyu Daniel Thomas na Kuamua Kumvisha Skafu yake ya Bendera ya Nchi yetu.Lilikuwa ni tukio la Kuvutia lililovutia Wengi sana na Kuamsha nderemo na Vifijo kwenye Uzinduzi wa Albamu hiyo.
Meza Kuu wakiendelea Kumsifu Bwana kwa kushirikiana na Waimbaji mbalimbali waliokuwa wakipanda Jukwaani Kusifu.
Bi.Magadalena Nyambalya akiimba wimbo wake wa "SAFARI YA MBINGUNI" Wakati wa Uzinduzi wa Albamu hiyo ya Bi.Rehema.
Mke wa Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Mwimbaji Maarufu Nchini Ndugu Upendo Nkone mara baada ya Kupanda Jukwaani kwaajili ya Kumsifu Mungu.
Mwimbaji Upendo Nkone aliomba Kuimba pamoja na Mh:Mwigulu Nchemba na Mke wake wimbo wa mmoja kwaajili ya Kumtukuza Mungu. Wimbo uliombwa ni "USIFURAHI JUU YANGU".
Wimbo wa Niacheni Nimbe,Mungu amejibu Maombi Yangu ndio Unaendelea hapa,Ni Wimbo wa Upendo Nkone ambao Ukiimbwa popote ni Lazima Utambue Uwepo wa Mungu.
Mwimbaji na Mchekeshaji Msanja Mkandamizaji akisifu wakati wa Uzinduzi wa Albamu ya Bi Rehema hii leo Victory Church Ubungo-External.
Mh:Mwigulu Nchemba akimtunza Mwimbaji Masanja Mkandamizaji.
Musa Baba wa Imani akiwatoa wana wa Israel Nchi ya Misri na kuwapeleka Nchi ya Ahadi.

NGASSA AENDELEA KUONGOZA KWA UFUNGAJI AFRIKA: AL AHLY YAVULIWA UBINGWA NA WAARAB WENZIE

AL AHLY ya Misri juzi Jumamosi usiku ilivuliwa taji la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Al-Ahly Beghazi ya Libya, lakini Mrisho Ngassa wa Yanga anaendelea kuongoza kwa ufungaji (mabao sita) katika michuano hiyo licha ya kuwa timu yake ilishatolewa mashindanoni.
Mafarao hao ambao pia ni mabingwa wa Super Cup, wametolewa kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya kukubali pia kipigo cha bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa Libya. Al-Ahly ilifuzu kwenye raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuiondoa Yanga kwa penalti.
Katika mechi nyingine zilizochezwa juzi Jumamosi, bao pekee la mshambuliaji wa TP Mazembe, Mbwana Samatta, ambaye huichezea pia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, lilitosha kuipeleka mbele klabu yake hiyo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na sasa iko robo fainali.
Mazembe ambayo imefuzu kwa faida ya bao la ugenini, iliifunga Sewe Sports ya Ivory Coast bao 1-0 baada ya wapinzani wao awali kushinda mabao 2-1 mjini Abidjan wiki moja iliyotangulia.
Mechi nyingine zilizopigwa siku hiyo As Vita Club ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliitoa Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kwa mabao 3-2 huku CS Sfaxien ya Morroco ikiiondosha Horoya ya Guinea kwa jumla ya mabao 3-0.
Mechi nyingine za ligi hiyo zilitarajiwa kucheza usiku jana Jumapili ambapo klabu pekee ya ukanda wa Cecafa iliyosalia, Al-Hilal ya Sudan ilikuwa icheze ugenini na AC Léopards, AS Real Bamako itaikaribisha Espérance de Tunis, Zamalek ilikuwa wageni wa Nkana ya Zambia na ES Sétif ilikaribisha Coton Sport.
Chanzo: Mwananchi

DC KAHAMA ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUMSAKA MTENDAJI WA KATA ALIYETOROSHA MKULIMA WA BANGI

Baadhi ya miche ya bangi iliyopatikana katika shamba hilo ikiwa imeshikiliwa na askari polisi
Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya (kulia) akitoa agizo hilo kwa mkuu wa kituo cha polisi Kahama Elias Haway na mkuu wa Upelelezi Wilaya Twaha Juma.
MKUU wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, ameliagiza jeshi la polisi wilayani humo kumtafuta na kumkamata Afisa Mtendaji wa Kata ya Mega, Peter Kupingwa, kwa tuhuma za kuhusika katika kumtorosha mkulima wa Bangi.

Mpesya ametoa agizo hilo jana baada ya kufika katika shamba lililokuwa limelimwa bangi hiyo lililopo katika kijiji cha Masabi, huku akiwa ameongozana na askari polisi na kukuta bangi hiyo imeshavunwa na kubaki miche kadhaa iliyochukuliwa kama ushahidi. 
Imedaiwa Afisa mtendaji huyo alitoa agizo la kuachiwa kwa Mtuhumiwa Juma Maliatabu ambaye juzi alikamatwa na sungusungu baada ya Afisa Kilimo wa kata hiyo Edwin Kasaba kuwapa taarifa za kukuta zao hilo katika shamba la Malingita.

Mpesya ametaka kukamatwa kwa Kupingwa ambaye ni mwajiri wake kutokana ma kuonesha kukerwa na kitendo alichokifanya cha kutetea na kuendelea kuwakumbatia watuhumiwa na kuongeza kuwa hakuna aliye juu ya sheria.
Shamba hilo la Hekari moja na nusu limelimwa mahindi huku yakiwa yamechanganywa na zao la Bangi ndani yake, jambo lililomfanya Afisa kilimo kwenda kukagua kama sehemu yake ya kazi kutembelea mashamba ya wakulima na kutoa ushauri.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, Shamba hilo linamilikiwa na Ndugu wawili Juma Maliatabu na Malingita Maliatabu ambaye pia hadi sasa hajulikani alipo baada ya kukosekana katika msako huo wa Polisi ambao bado unaendelea. 
Hata hivyo Jeshi la wilaya ya Kahama lililokuwa likiongozwa na Mkuu wa kituo cha polisi Kahama Elias Haway na Mkuu wa Upelelezi Wilaya Twaha Juma limefika katika kaya za Watuhumiwa kwa lengo la kuwakamata bila Mafanikio.

WABUNGE KUANZA KUPITIA RASIMU YA KATIBA

Wajumbe wa Bunge la Katiba.
BUNGE Maalumu la Katiba linaendelea na kikao chake na miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanywa kuanzia leo, ni kurekebisha baadhi ya kanuni za uendeshaji wake na kuanza kujadiliwa kwa ibara zilizopo ndani ya rasimu ya Katiba.
Pamoja na kazi hiyo ya kufanyia marekebisho kanuni za Bunge, Makamu Mwenyekiti wa Bunge hilo Maalumu la Katiba, Samia Suluhu Hassan akiahirisha kikao cha Bunge juzi, alisema leo Bunge litaanza kazi ya kupitia rasimu ya Katiba kwa kuanza na Sura ya Kwanza na Sura ya Sita. 
Sura ya Kwanza inazungumzia muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Sita inazungumzia masuala ya Muungano.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, mjadala kuhusu Kamati ya Bunge utafanyika kwa muda usiozidi siku mbili na baada ya mjadala, kila Kamati itaandaa taarifa kuhusu mambo yaliyoafikiwa na wajumbe walio wengi kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye Bunge Maalumu.
Kanuni hizo zinasema endapo kutakuwa na wajumbe ambao hawakuunga mkono maoni ya wajumbe walio wengi katika Kamati, wajumbe hao wanaweza kuandaa maoni yanayohusu maeneo ambayo hawakukubaliana nayo na yatajumuishwa kwenye taarifa ya Kamati.
Baada ya Kamati kuandaa taarifa yake, Mwenyekiti wa Kamati inayohusika atamjulisha Mwenyekiti kwa maandishi kuwa Kamati imekamilisha kazi yake. 
Kwa mujibu wa kanuni, keshokutwa wenyeviti wa Kamati 12 za Bunge hilo Maalumu la Katiba sasa wanatarajia kuwasilisha taarifa za kile walichojadiliana katika sura namba moja na sita za rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu.
Baada ya jaribio la awali kutaka baadhi ya kanuni kurekebishwa kugonga mwamba wiki iliyopita, sasa azimio lenye lengo hilo litawasilishwa leo.
Jaribio la awali lilishindikana baada ya wabunge wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kupinga mpango wa kutaka kanuni hizo kurekebishwa wakati hazijaanza kutumika, wakisema ni mbinu za kutaka kuwadhoofisha.
Walitaka kanuni za 37 na 38 pekee ambazo ziliwekwa kiporo ndizo zijadiliwe. 
Ukawa kupitia kwa Mwanasheria wao, Tundu Lissu, ulipinga jaribio hilo hata kabla ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho kusoma azimio hilo ndani ya bunge wiki iliyopita, huku Lissu akiita karatasi iliyokuwa na mapendekezo hayo kuwa ni 'takataka'.
Kutokana na mzozo huo, Mwenyekiti wa Bunge hilo Samuel Sitta alilazimika kuagiza Kamati ya Kanuni kuahirisha uwasilishaji wa Azimio la Marekebisho hayo ya kanuni wamalize kwanza utata ulioibuliwa na Ukawa; ambao ulisababisha kikao cha Bunge kuahirishwa kutokana na vurugu.
Taarifa zilizomfikia mwandishi, zilisema baada ya kutafakari kwa kina na kupitia kwa Kamati ya Maridhiano, Ukawa wamekubali kufanyiwa marekebisho kwa baadhi ya kanuni baada ya kuonekana kuwa baadhi zinawabana wabunge katika ushiriki wao kwenye vikao vya Bunge na hata kwenye vikao vya Kamati.
Alhamisi iliyopita Mwenyekiti Sitta alitangazia wajumbe kwamba kwa vile marekebisho ya kanuni yalikwama, sasa Kamati zitaendesha mijadala kwa kutumia kanuni zile zile za Bunge Maalumu.
Agizo hilo la Sitta lilionekana kuwa mwiba kwa wabunge wengi, ambapo kanuni ya 32 inawabana kuvaa mavazi rasmi, mjumbe kusimama anapotaka kutoa hoja hata kama wako wachache na vikao vya kamati vitalazimika kuanza saa tatu asubuhi hadi saba mchana na baadaye saa 10 jioni hadi saa mbili usiku, kama ilivyo kwa vikao vya Bunge, jambo ambalo limeonekana kuwa ni mwiba mkali.
Hata hivyo inadaiwa baadhi ya kanuni zilizotakiwa awali kuwasilishwa kwa marekebisho, hazitakuwepo kutokana na makubaliano yaliyofikiwa ikiwemo kanuni inayohusu uamuzi kupitishwa kwa theluthi mbili za pande zote mbili za Muungano ili utaratibu wa kutumika uwe wa wingi wa kura.
Kanuni nyingine ambayo pia ilikuwa ifanyiwe marekebisho na baada ya mashauriano hayo itabaki kama ilivyo, ni ya 32(1) ambayo inasema kila Kamati itajadili rasimu ya Katiba kwa wakati mmoja kwa kuzingatia mgawanyo wa sura mbili za rasimu kwa mujibu wa ratiba itakayopangwa na Kamati ya Uongozi.
Hatua hiyo inaondoa mpango aliotangaza Mwenyekiti Sitta wiki iliyopita kwamba Kamati zitabadili kanuni hiyo ziweze kujadili kanuni tatu tatu au nne nne, suala ambalo lilipingwa na Ukawa ukidai msingi wake unalenga katika kujadili sura nyingi kwa pamoja jambo litakaloondoa umakini.
Chanzo: Zirro blog

BADO MUAFAKA KATI YA MAREKANI NA URUSI HAUJAPATIKANA

John Kerry akutana na Serguei Lavrov kuhusiana na taharuki kuhusu Ukraine
WAZIRI wa mashauri ya Nchi za kigeni wa Marekani John Kerry, amesema kuwa hakuna makubaliano yaliyoafikiwa baina yake na mwenzake kutoka Urusi Sergei Lavrov, katika mkutano wadharurakuhusu mzozo wa Ukraine.

Marekani inasisitiza kuwa hatua ya urusi kutwaa eneo la Crimea baada ya kura ya maoni sihalali.Bwana Lavrov ametoa masharti makali yasiyoegemea upande wowote huku akitaka uhuru wa Ukraine kama taifa utambuliwe.Waziri wa Urusi amesema kuwa ni jukumu la Kiev kuandaa katiba mpya ili kuwezesha hilo lifanyike, mbali na kulinda maisha ya waukraine wachache wanaozungumza kirusi dhidi ya uvamizi kutoka kwawaukraine wanaounga mkono kujiunga na jumuiya ya Ulaya.Marekani imetaka hatua ya kuongeza wanajeshi zaidi wa Urusi katika mpaka mashariki ya Ukraine kukomeshwa mara moja.

Mazungumzo ya Paris siku ya ijumaa yalifuatwa na mazungumzo ya simu kati ya Rais Vladimir Putin wa Urusi na Rais Obama wakati aliposimama kwa muda akiwa njiani kuelekea Washington siku yaJumamosi, Bwana Kerry alibadilisha mkondo na kuelekea Paris.Ukraine inasisitiza kuwa Urusi ina njama ya kuigawanya Ukraine na kulisambaratisha kama taifa.Waandishi wanasema kuwa Maafisa wa Marekani wamegawanyika iwapo mazungumzo hayo yaliyopangwa yametokana na nia halisi ya Urusi ya kujaribu kupunguza taharuki iliyopo au ni mipango ya hatua zaidi ya kijeshi.
Pentagon inaamini kuwa maelfu ya wanajeshi wa Urusi wamekita kambi karibu na mpaka na Ukraine kwa niya ya kuwatishia viongozi wa Ukraine.

ANGALIA PICHA ZA KAMPENI ZA CHADEMA JIMBO LA CHALINZE

Ally Bananga, mgombea wa Chadema Mathayo torongey na viogozi wengine wakiwa katika kampeni Jimbo la Chalinze.
Mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ndugu Mathayo Mang'unda Torongey akiendelea na mikutano ya Kampeni Jimboni Chalinze, Ijumaa Machi 28, 2014,

TASWIRA ZA KAMPENI YA UCHAGUZI JIMBO LA CHALINZE KUPITIA CHADEMA

Makamanda wakiwa wamekwama kupita kwenye barabara wakielekea kwenye kampeni za Ubunge Jimboni Chalinze.
Mgombea wa nafasi ya Ubunge Jimb la Chalinze Ndugu Mathayo Torongey akibadilishana mawazo na wanakijiji Jimboni Chalinze.
Katibu wa CCM Kata ya Kimange Bwana Haji aliondoka CCM na kujiunga na CHADEMA huku akikabidhiwa kadi yake na Makamu Mkiti Said Issa Mohamed.

ZILIZOSOMWA ZAIDI