NYUMBANI KITAIFA

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BIASHARA

Ulimwengu wa habari.

MATAIFA MENGINE

Ulimwengu wa habari.

KATIKA BURUDANI

Ulimwengu wa habari.

MAAJABU DUNIANI

Ulimwengu wa habari.

Saturday, August 1, 2015

MSHINDI WA NAFASI YA UBUNGE VITI MAALUM CCM MKOA WA SINGIDA, AMPONGEZA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI, DK.KONE

IMG_1615
Mshindi wa kwanza wa nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Aysharose Ndogholi Mattembe, akiwashukuru wapiga kura 318 (hawapo kwenye picha). Aysharose  ambaye ni Mkurugenzi wa shule ya British Zanzibar ya Kisauni Zanzibar, alipata ushindi huo mnono baada ya kuwabwaga wapinzani wake 13 kwenye uchaguzi uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa.
IMG_1574
Mshindi wa kwanza wa nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Aysharose Ndogholi Mattembe (kulia) akiwa na msindi wa pili ( kura 235)  nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Martha Moses Mlata (kushoto), kwa pamoja wakiwashukuru wapiga kura wao, muda mfupi baada ya kutangazwa washindi. Kwa nyuma yao,ni aliyekuwa msimamizi uchaguzi wa UWT mkoa ambao ulichagua wana CCM wawili nafasi ya ubunge viti maalum, Dk. Parseko Kone.
IMG_1618
Msindi wa kwanza wa nafasi ya ubunge viti maalum CCM mkoa wa Singida, Aysharose Ndogholi Mattembe (wa kwanza kushoto), akiwa na wapinzani wake 12 wakifuatilia ufungaji wa mkutano huo uliofanywa na Katibu UWT mkoa wa Singida, Angela Mirembe.(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu, Singida
MSHINDI wa kwanza ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida,Aysharose Ndogholi Mattembe, amemshukru na kumpongeza msimamizi wa mkutano mkuu wa uchaguzi UWT uliofanyika hivi karibuni, Dk.Parseko Kone,kwa madai kwamba alitenda haki kitendo kilichochangia mkutano umalizike kwa amani na utulivu mkubwa.
Uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa katoliki mjini hapa,Mattembe alizoa kura 318 na kufuatiwa na Martha Moses Mlata aliyetetea nafasi yake kwa kupata kura 235.
Akifafanua, Mattembe ambaye ni Mkurugenzi shule ya British Zanzibar iliyopo Kisauni,alisema msimamizi huyo ambaye ni mkuu wa mkoa wa Singida,alitenda haki kuanzia mwanzo wa mkutano hadi mwisho.
“Nadhani katika kutaka pasiwepo na malalamiko,msimamizi Dk.Kone,alitutaka sisi wagombea wote tuwepo kwenye chumba cha kuhesabia kura.Uwepo wetu ndani ya chumba hicho,kuliondoka kabisa wazo la  wizi wa kura kwenye uchaguzi wetu”,alisema.
Alisema kuwa kwa ujumla msimamizi alikuwa ‘fair’ kabisa na ndio maana hata wagombea waliopata kura ambazo hazikutosha, kwanza walishukuru uchanguzi umefanyika kwa haki na uhuru na waliondoka ukumbi wakiwa na amani ya hali ya juu pamoja na mashabiki wao.
Katika hatua nyingine,Mattembe aliwaahidi wajumbe wa mkutano huo zaidi ya 940,kwamba hatawaangusha na wategemee ushirikiano na vitendo atavipa kipaumbele zaidi.
Kwa upande wake  msanii maarufu wa filamu na aliyekuwa Mlimbwende nambari moja nchini mwaka 2006, Wema Sepetu ametingisha kwenye kura za maoni kuwania nafasi mbili za ubunge Viti Maalum (Wanawake).
 Katika kinyang’anyiro hicho, Wema alipata kura 90 akiwa nyuma ya wagombea wakongwe watatu; Diana Chilolo aliyeshika nafasi ya tatu kwa kupata kura 182, Martha Mlata aliyeibuka wa pili kwa kura 235 na AyshaRose Matembe aliyekuwa wa kwanza kwa kuzoa kura 318.
 Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi huo, Dk Kone, walioshiriki wengine kwenye uchaguzi huo na matokeo yao kwenye mabano kuwa ni Sarah Mwambu (74), Martha Gwau (44), Rehema Madusa (24), Aziza Ntandu (5), Mary Marco (3), Sofia Joseph (2), Salome Mpondo (1), Leah Samike (1) na Elizabeth Lucas (0)
Aidha, msimamizi huyo alimtangaza Sarah Mkumbo kuwa mwakilishi wa kundi la Walemavu wakati Hawa Athman alichaguliwa kuwakilisha kundi la Mashirika yasiyo ya Kiserikali.
Akitoa shukrani zake kwa wajumbe, Wema alisema kuwa anawashukuru wajumbe kwa kuonesha imani kubwa kiasi hicho kwake japo ni mara yake ya kwanza kujitokeza na akawahakikishia kuwa huo ndio mwanzo tu wa safari yake.
Naye Chilolo, ambaye ametumikia nafasi ya ubunge Viti Maalum mkoa wa Singida kwa miaka 15 na sasa ndiye  Mwenyekiti wa UWT mkoa, aliwataka washindi wote kushirikiana kwa dhati ili CCM ipate ushindi kwenye Uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

BASATA IMEMFUNGIA SHILOLE MWAKA MMOJA, HAKUNA KUFANYA MUZIKI

Shilole Akiwa Jukwaani Huku Mali zake Zikiwa Nje Nje...

Breaking news zilizoifikia usiku wa July 30 2015 kutoka Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) ni kwamba baraza hili limemfungia Shilole kutojihusisha na kazi yoyote ya sanaa kwa muda wa mwaka mmoja.

Barua iliyoifikia  imeandikwa kutoka BASATA imesema >>> ‘Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili‘

‘BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako‘ – BASATA

‘Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae ‘ – BASATA

Je ni Sawa Kwa Shishi Kufungiwa?

BABA HAJI ASHANGILIA ANGUKO LA WEMA SEPETU..AFURAHIA WEMA SEPETU KUSHIKA NAFASI YA MWISHO


STAA wa filamu Bongo, Adam Haji ‘Baba Haji’ juzikati aliangusha sebene la nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa kuwa staa wa kike nchini aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wema Isaac Sepetu ameangushwa.

Akionekana mwenye furaha huku akiserebuka muziki alisema kuwa mbunge wenu amekosa ubunge, jambo lililowafanya baadhi ya wasanii wenzake waangue kicheko kwa kuwa inafahamika kuwa ana bifu naye.

“Jamani mmesikia majibu? Mbunge wenu kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.

Bifu la Baba Haji na Wema lilianza kitambo ambapo wawili hao walikutana kwenye Ukumbi wa Bilicanas, Posta jijini Dar ambapo Wema alimchana jamaa huyo kuwa ananuka jasho.
#GPL

SHAMSA FORD: MCHAWI WA MAISHA YAKO NI WEWE MWENYEWE

NIDHAMU ni silaha kubwa katika maisha.kuna ambao Mungu aliwabariki kwa nafasi zao lakini hawakuweza kutumia nafasi zao vizuri kwasababu ya kukosa nidhamu.walihisi wao ni bora kuliko wengine ndo maana walibarikiwa.
Mwisho wa siku wakishapotea au mambo kwenda tofauti na walivyokuwa wanadhania wanaanza kulaumu watu.Wengine wataingia hadi kwenye ushirikina kwa kusemwa wamerogwa..Mchawi wa maisha yako ni wewe mwenyewe...MUWEKE MUNGU MBELE,KUWA MVUMILIVU,ACHA TAMAA,FANYA KAZI KWA BIDII, PENDA KUJIFUNZA NA KUBALI USHAURI
Shamsa Ford "@shamsaford" on instagram

HAWA NDIYO MASTAA WALIOMFUATA LOWASSA UKAWA *PICHAZ*

Staa wa Bongo fleva, Emmanuel Elibariki, ‘Nay wa Mitego’.
NI shidaah! Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Zamani, Edward Ngoyai Lowassa (pichani) kukaribishwa katika Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao, mastaa mbalimbali Bongo wameamua na wengine kushawishiwa kumfuata wakiamini katika uwezo wake kiuongozi, Amani limenasa mpango mkakati kamili.
Chanzo makini kililieleza gazeti hili kwamba mastaa wote waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa wakati akiwania kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupeperusha bendera ya chama hicho katika nafasi ya urais na baadaye jina lake kukatwa kabla ya kufikishwa Kamati Kuu (CC), wameamua kuhamia Ukawa kumfuata mwanasiasa huyo aliyejiunga huko kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
TUJIUNGE NA CHANZO
“Moto huku Ukawa umewaka. Yale makundi mawili ya M4C (Movement For Change- Chadema) na 4 U Movement (Kundi la Marafiki wa Lowassa) sasa yameingia kazini. Mkakati maalum umeandaliwa kuhakikisha kila mwenye ushawishi katika jamii anafikiwa, wakiwemo wasanii wa sanaa mbalimbali.
“Wameanza na wasanii waliokuwa nyuma ya Lowassa kwa sababu wanaamini wana wafuasi wao, ambao watashawishiwa wawashawishi hao watu wao wawaunge mkono katika kuhakikisha wanaing’oa CCM madarakani,” kilisema chanzo hicho.
Wema Sepetu.
WEMA AKARIBISHWA
Chanzo hicho kimeweka wazi kuwa licha ya wasanii kwa jumla, lakini pia mastaa wenye mvuto mkubwa kwa jamii watafuatwa wao rasmi, kama ilivyotokea majuzi ambapo mwigizaji Wema Isaac Sepetu alifuatwa na 4 U Movement (Team Lowassa) kushawishiwa kujiunga na Team Lowassa.
Wiki iliyopita Wema alitoswa katika kura za maoni za kuwania Ubunge wa Viti Maalum (UWT-CCM) Mkoa wa Singida kwa kushika nafasi ya nne, lakini akapokewa kwa kishindo katika mapokezi yaliyojaza watu jijini Dar.
“Yaani Wema hivi karibuni aliitwa na watu wa Lowassa kwenye hoteli moja maarufu jijini Dar ambapo ajenda kubwa ni yeye kuungana na Ukawa kwa vile wanaamini ana mashabiki wengi,” kilisema chanzo hicho.
HUYU HAPA WEMA
“Ni kweli, juzi nilipigiwa simu na watu waliojitambulisha kuwa ni Team Lowassa, wakasema wana mazungumzo na mimi, ilikuwa tukutane Jumanne, lakini nilikuwa na shughuli nyingine nikashindwa kwenda.
“Tulikubaliana tukutane jana, lakini sijaelewa hasa ajenda ni nini na kwa maana hiyo siwezi kusema lolote kwa sasa kama ninaenda Ukawa au la,” alisema muigizaji huyo, alipozungumza na gazeti hili.
Jacquiline Wolper.
WOLPER ACHOCHEA
Kana kwamba haitoshi, staa mwingine wa filamu za Kibongo, Jacqueline Walper Massawe ambaye tangu awali alijitoa muhanga kufa pamoja kisiasa na mbunge huyo wa Monduli, anatajwa kuwa kinara wa kampeni katika mitandao mbalimbali ya kijamii akiweka wazi kuwa atamfuata Lowassa popote atakapokwenda kwani ni shabiki wake mkubwa.

Aunt Lulu.

AUNTY LULU RASMI UKAWA
Ahadi kama hiyo ilitolewa pia na mwanadada Lulu Semagongo ‘Aunty Lulu’ aliyetangaza kujiunga rasmi na Ukawa kwa sababu ya Lowassa.
Kala Jeremiah.

Mastaa wengine ambao wamemfuata Lowassa Ukawa ni pamoja na Deogratius Shija, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Kala Jeremiah, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’, Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Bahati Bukuku.

MAHABA NIUWE!! HATIMAYE KAKA’KE ZARI AMCHUMBIA LINAH!

Esterlina Sanga ‘Linah’ na mchumba wake amabye ni kaka za Zari, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’
Hatimaye staa wa Bongo Fleva ambaye ni zao la Nyumba ya Vipaji Tanzania (THT), Esterlina Sanga ‘Linah’ amechumbiwa rasmi na yule jamaa wake, Wiliam Bugene ‘Boss Mtoto’ ambaye ni kaka kiukoo wa mpenzi wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.’
Akizungumza na Amani kwenye mahojiano maalum alipotimba katika Tamasha la Filamu la Kimataifa (ZIFF), Zanzibar hivi karibuni, Linah alisema kuwa ana furaha maishani mwake kwa kumpata mtu mwenye mapenzi ya kweli ambaye atafunga naye ndoa ‘soon’.
“Tayari ameshanichumbia, anajulikana kwetu na mimi najulikana kwao. Kifuatacho ni ndoa yangu,” alisema Linah ambaye hivi karibuni amesema ataachia wimbo mpya utakaokuwa gumzo.
Furaha ya Linah inakuja kufuatia kumpata mwanaume huyo ambaye amekuwa akionekana naye kila kiwanja wakiwa wamegandana kimahaba ikiwa ni miezi kadhaa tangu alipodai kuporwa bwana’ke, Nagari Kombo anayedaiwa kakwapuliwa na Wema Sepetu.

Kabla ya Boss Mtoto na Kombo, huko nyuma Linah aliwahi kuripotiwa kuwa kwenye uchumba ‘serious’ na msanii mwenzake, Amini Mwinyimkuu.

ITAZAME ORODHA YA NCHI 10 ZINAZOONGOZA KWA MATUKIO YA UBAKAJI DUNIANI

Bado matukio ya ubakaji yameendelea kushika kasi katika nchi mbalimbali duniani licha ya kuwepo kwa sheria za kuwabana wahusika.
Hapa kuna hizi nchi 10 ambazo zinaongoza kwa matukio ya ubakaji duniani.
1. Afrika Kusini
Afrika ya Kusini ndio nchi yenye idadi kubwa ya kesi za ubakaji duniani wanazofanyiwa watoto wa dogo..mwaka 2000 jumla ya kesi 67,000 ziliripotiwa.
2. Botswana
Nchi ya Botswana inashika nafasi ya pili kwa matukio ya ubakaji..mwaka 2011, 10.3% ya wanawake zaidi ya 600 walifanyiwa vitendo vya ubakaji
3. Lesoth
33% ya wanawake walibakwa wakiwa na umri wa miaka 18 huku kukiwa na 66% ya kesi za ubakaji kila mwaka
4. Swaziland
Kasi ya ubakaji kwa wasichana chini ya miaka 18 imekuwa ikiongezeka..Ripoti ya UNICEF imesema msichana mmoja kati ya watatu hubakwa na kuchangia uwepo wa maambukizi ya VVU kwa wingi
5. Bermuda (Uingereza)
Nchi hii ipo mpakani mwa Uingereza..imekua na matukio mengi ya ubakaji hadi kupelekea wanawake kutengewa sehemu yao kuepuka vitendo hivyo
6. Sweeden
Tangu mwaka 2005matukio ya ubakaji yamekua yakitokea na hayabadiliki licha ya kupitishwa sheria kali
7. Suriname (America ya Kusini)
Matukio mengi ya ubakaji katika nchi hii iliyopo Amerika ya kusini yamekuwa hayaripotiwi licha ya kutokea mara kwa mara..lakini yamekua yakipungua kadri siku zainavyokwenda
8. Costa Rica
Tangu mwaka 2000 matukio ya ubakaji yamekuwa yakiongezeka na kufikia 42% ya kesi hizo kila mwaka.
9. Nicaragua (America ya Kaskazini)
Hiki ni moja ya visiwa masikini duniani lakini kinaongoza kwa matukio ya ubakaji kwa asilimia kubwa.. 
10. Crenada (America ya Kaskazini)

Kila anayepatikana na kosa la ubakaji katika nchi hii adhabu yake ni miaka 15 jela

ZILIZOSOMWA ZAIDI