NYUMBANI KITAIFA
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BIASHARA
Ulimwengu wa habari.
MATAIFA MENGINE
Ulimwengu wa habari.
KATIKA BURUDANI
Ulimwengu wa habari.
MAAJABU DUNIANI
Ulimwengu wa habari.
Sunday, July 26, 2015
KUMBE LULU ALIMWAMBIA WEMA SEPETU HAYA BAADA YA JINA LAKE KUKATWA UBUNGE VITI MAALUM
10:01 AM
No comments
Baada ya matokeo ya Ubunge viti maalamu Singida kutoka na Wema Kupigwa chini, Lulu Michael amemtia moyo Wema Sepetu kwa Kuandika ujumbe huu;
Kuna matokeo ya aina 3
>>Kushinda
>>Kushindwa
>>Kudroo.
Mpka hapa ulipofika Leo umethubutu kitu ambacho wanawake wengi ni waoga kujaribu wewe ni mshindi Dada yawezeka Kuna kingine zaidi Mungu amekuandalia
Saturday, July 25, 2015
MCHUNGAJI NATSE AWAAGA JIMBO LA KARATU, QAMBALA KUPEPERUSHA BENDARA YA CHADEMA
9:47 AM
No comments
Mbunge wa Viti Maalumu wilaya ya Karatu,Cecilia Paresso akizungumza katika mkutano huo ambao alichaguliwa na wajumbe wanawake kuwania nafasi hiyo. |
Mwanamke wa kwanza kuwahi kujitokeza kuomba ridhaa ya wanachama kumchagua kugombea nafasi ya ubunge katika Jimbo la Karatu,Fransisca Duwe akijinadi kwa wajumbe. |
Willy Qamballa mmoja wa wagombea akijinadi kwa wajumbe |
Aliyekua Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karatu, Lazaro Maasay akiomba kura kwa wajumbe |
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akiwashukuru wajumbe baada ya kujizolea kura 217 na mpinzani wake wa karibu Lazaro alipata kura 84. |
Mshindi wa kura za maoni za Ubunge Jimbo la Karatu,Willy Qamballa akifurahia na wafuasi wake baada ya kutangazwa mshindi. |
KADAMA MALUNDE MWENYEKITI MPYA WA WANAHABARI SHINYANGA
1:43 AM
No comments
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga aliyemaliza muda wake, Shija Felician akimpongeza Mwenyekiti mpya wa Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Kadama Malunde (mwenye suti) baada ya kutangazwa mshindi katika uchaguzi wa Klabu hiyo.
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga waliomaliza muda wao wakijiuzuru nyadhifa zao kabla ya uchaguzi mkuu kupata viongozi wapya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club- SPC)
Msimamizi wa uchaguzi mkuu wa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga David Nkulila akizungumza jambo wakati wa uchaguzi mjini Shinyanga.
Mwenyekiti mpya wa SPC Kadama Malunde, ambaye pia ni Mkurugezi wa Malunde1 blog akipongezana na mwenyekiti aliyemaliza muda wake Shija Felician (kulia)
Katibu mkuu mpya wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga ndugu Stephen Wang'anyi akizungumza baada ya uchaguzi, kushoto ni mweka hazina aliyetetea kiti chake bi Stella Ibengwe.
Baadhi ya viongozi wa SPC wakiwa katika picha ya pamoja.
Na Mwandishi Wetu, Shinyanga
CHAMA cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club-SPC) Julai 23, 2015 kimefanya Uchaguzi wake Mkuu wa viongozi watakaokiongoza chama hicho kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo ambapo mwanahabari, Kadama Malunde amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa chama hicho.
Akitangaza matokeo hayo Msimamizi wa Uchaguzi huo Mkuu wa SPC uliofanyika mjini Shinyanga, David Nkulila alisema, Malunde ametwaa nafasi hiyo baada ya kuwashinda wagombea wenzake watatu ambao ni Patrick Mabula, Marco Mipawa na Greyson Kakuru.
Kadama Malunde ni mwandishi wa habari wa gazeti la Mtanzania, Kahama FM na Mkurugenzi wa Malunde1 blog ambayo ni blogu Mwanachama wa Chama cha Blogu Tanzania (Tanzania Bloggers Network, TBN). Nkulila aliwataja viongozi wengine wapya waliochaguliwa kuwa ni Stephen Wang’anyi akichaguliwa kuwa Katibu Mkuu, Shaaban Alei kuwa Makamu Mwenyekiti, Katibu Msaidizi Ally Lytawi na mweka hazina ni Stella Ibengwe pamoja na kamati tendaji ya wajumbe watano.
Baada ya kutangaza matokeo hayo Nkulila amewataka wanachama wa klabu hiyo, kuachana na tofauti zillizokuwepo wakati wa uchaguzi na badala yake kushirikiana na viongozi waliowachaguliwa ili kuleta maendeleo na mabadiliko katika klabu hiyo.
Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Mwenyekiti mpya wa SPC, Kadama aliwashukuru wanachama wote wa chama hicho kwa kumkubali aweze kushirikiana nao kuweza kutatua changamoto mbalimbali za wanahabari mkoani hapo pamoja na kuleta maendeleo kwa klabu hiyo. Aidha aliahidi kutenda haki kwa kila mmoja na kuzingatia katiba ya chama katika utendaji wa kazi za chama.
Kwa upande wake Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Felician amewataka viongozi wapya wa klabu hiyo kuendeleza misingi ya ushirikiano waliouacha na kuwasisitiza kufanya kazi kwa uwazi na ukweli huku wakizingatia maadili ya wanahabari.
UZINDUZI WA KAMPENI YA WAZAZI NIPENDENI AWAMU YA PILI WAFANYIKA VIWANJA VYA MWEMBE YANGA TEMEKE JIJINI DAR
1:11 AM
No comments
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya pili katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana. Wa kwanza kushoto ni
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba na wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema.
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID), Anna Bodipo Memba (kulia), akitoa hutuba yake kwenye uzinduzi huo.
Mshauri wa masuala ya Afya ya Jamii kutoka Taasisi ya HBC, Mdadike Thabit (kulia), akimuelekeza jambo mgeni rasmi katika uzinduzi huo Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya watoa huduma kabla ya kufanyika uzinduzi huo.
Wananchi wakiwa wamejipanga foleni kwa ajili ya kupata huduma za afya ya jamii kwenye uzinduzi huo.
Wanamuzi wa bendi ya muziki wa dansi ya FM Academia
wakitoa burudani.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Grace Magema akizungumzia mikakati ya Afya ya Jamii katika mkoa huo.
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila, akitoa hutuba yake ya uzinduzi.
Watoto nao walikuwepo kwenye uzinduzi huo.
Mwanamuziki Juma Nature akitoa burudani kwenye uzinduzi huo.
Wananchi walioshiriki uzinduzi huo.
Kiongozi wa kundi la muziki la Wanaume Family, Chege (kulia), akishambulia jukwaa katika uzinduzi huo. |
Msanii wa kundi la utamaduni la HD Entertainment la Mbezi Beach, Michael Kamugisha, akiwa ameruka juu wakati wa kundi hilo lilipokuewa likitoa burudani katika uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
TANZANIA imeweza kufikia lengo la milenia namba 4 la kupunguza vifo vya watoto kwa theluthi mbili kutoka vifo 152 hadi 54 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Neema Rusibamayila kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo Dk. Seif Rashid wakati akizindua kampeni ya awamu ya pili ya Wazazi Nipendeni katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo mchana.
Alisema pamoja na kutofikia lengo la melenia namba 5 la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa robo tatu kufikia vifo 193 kwa kila vizazi hai laki moja, taarifa za umoja wa mataifa za mwaka 2014 zinaonyesha kuwa Tanzania imeweza kupunguza vifo hivyo toka 770 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 1990 hadi kufikia 410 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2014.
"Sababu zinazosababisha watoto waliochini ya miaka mitano kupoteza maisha ni kuharisha, nimonia na malaria na kuwa zinachangia takribani asilimia 50 ya vifo vya watoto hao waliochini ya miaka mitano" alisema Dk.Rusibamayila.
Alisema utapiamlo nao ni tatizo linalochangia vifo vya watoto hao kwani takwimu za mwaka 2010 zinaonyesha kuwa kiwango cha udumavu ni asilimia 42 kwa watoto waliochini ya umri wa miaka mitano.
Dk.Rusibamayila aliongeza kuwa vifo vya watoto wachanga havijapungua kwa kasi inayoridhisha na vinachangiwa na wale watoto wanaozaliwa njiti, kushindwa kupumua vizuri mara baada ya kuzaliwa na maambukizi ya bakteria.
Monday, July 6, 2015
KIM KARDASHIAN AMUAIBISHA MUMEWE
8:18 AM
No comments
Mwanamitindo wa Marekani, Kim Kardashian.
New York Marekani
Mashabiki wa Kim Kardashian, wameshangaa kitendo cha yeye kutoka nyumbani bila kuvaa Bra na kudai kuwa ni kumuaibisha mume wake kwani hii si mara ya kwanza.
Mashabiki wa Kim Kardashian, wameshangaa kitendo cha yeye kutoka nyumbani bila kuvaa Bra na kudai kuwa ni kumuaibisha mume wake kwani hii si mara ya kwanza.
Papararazi
walimpiga picha Kim akionekana kutovaa sidiria huku mtaani wakijiuliza
kulikoni mume wake hamuoni au ni mtu asiyejali na kumpachika jina la
‘Mastermind’.
“Kivazi hiki kimekuwa kikiwatega watu kwani sehemu kubwa ya kifua chake kiko wazi, si vizuri kwa mama mwenye mtoto kuvaa nguo kama hii, kweli anamhaibisha mumewe”, alisema Shabiki mmoja
“Kivazi hiki kimekuwa kikiwatega watu kwani sehemu kubwa ya kifua chake kiko wazi, si vizuri kwa mama mwenye mtoto kuvaa nguo kama hii, kweli anamhaibisha mumewe”, alisema Shabiki mmoja
DIAMOND AFANYIWA KUFURU NIGERIA
8:16 AM
No comments
Pasua anga! Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’ amefanyiwa kufuru ya bonge la pati na msanii mwenzake kutoka
nchini Nigeria, Kingsley Chinweike Okonkwo ‘KCEE’ Ijumaa Wikienda lina
ubuyu kamili.
Staa grade one kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu kilichosafiri na staa huyo ambaye
yupo nchini humo kwa ziara yake inayofahamika kama ‘Nana Tour’, tangu
Diamond alipofika siku ya kwanza akiwa na mameneja wake, Salam, Babu
Tale, DJ wake aitwaye Romy Jones na wengine, mastaa kibao wakubwa
walikuwa wakihitaji kuwa wenyeji wake.
“Jamaa ana uhusiano mzuri sana na mastaa wa Nigeria. Kuna ambao ameshafanya nao kazi kama Yemi Alade, Tiwa Savage, Bracket, Iyanya, KCEE na P Square (bado haijatoka). “Pia wapo wengine kibao wanaotaka kufanya naye kazi hivyo wanamuwinda.

Waliposikia anakuja kufanya ziara ya wimbo wake mpya kila mmoja alitaka kuwa mwenyeji wake.
“Simu zilikuwa nyingi lakini mwisho wa siku KCEE alikuwa ameshafika uwanja wa ndege kutupokea na hiyo ilikuwa rahisi kwake kwa kuwa naye hivi karibuni alimshirikisha katika wimbo wake wa Love Boat,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kinaendelea kumwaga ubuyu kuwa baada ya kufika nyumbani kwa KCEE, staa huyo mwenye mikoko na majumba ya kutosha nchini humo kupitia muziki, aliwafanyia bonge la ‘sapraiz’ kwa kufungua makabati yake ya rangi ya dhahabu na kuwaonesha tuzo kibao alizozipata kisha wakajimwaga sebuleni ambapo waliandaliwa pati ya madikodiko ya Kinigeria.

Wakipata msosi.
“KCEE ni kati ya wasanii wenye mafanikio na mali kibao. Jumba tu
aliokaribishwa ndani yake lilijengwa kwa kuchanganya nakshinakshi za
dhahabu.”
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Diamond kupitia Mtandao wa WhatsApp kuhusiana na mapokezi yake ambapo alifunguka:
“Nashukuru kwa Nigeria kunipokea vizuri najihisi kama niko nyumbani, nasema asante sana kwa watu hawa kwani wameonesha sapoti ya nguvu hata katika kunipigia kura katika Tuzo za MTV MAMA,” alisema Diamond na kuongeza.
“Kwa sasa akili yangu yote nimeielekeza kimataifa zaidi baada ya kufanya kolabo za kutosha Afrika.”
Hivi karibuni Meneja wa Diamond, Babu Tale alikaririwa akisema kuwa mashabiki wategemee kolabo ya kimataifa na msanii mkubwa na kudokeza kuwa msanii huyo anaweza kuwa Usher Rymond, Chris Brown, Ne-YO au yeyote mkubwa kutoka Marekani.

MMEACHANA? HAKUNA SABABU YA KUCHUKIANA!
8:05 AM
No comments
Mpenzi msomaji wa XXLove karibu kwenye Jumatatu nyingine mwanana
katika ulimwengu wa uhusiano wa kimapenzi.Katika mada yetu tajwa hapo
juu, nitazungumza na wale rakifi zangu walioachana au kuachwa na kuanza
kumchukia mwenza wake.
Ni
kweli kuachwa kunaumiza sana moyo. Kimsingi usiombe kukumbwa na maumivu
ya kuachwa. Lakini kama hilo limekwishatokea, kwa nini uendelee kuumia
na kumchukia aliyekuwa mpenzi wako?
Kitendo cha kukuacha wewe, kinaweza kumtokea hata yeye na kujikuta akilia na kuhuzunika kama wewe. Kama ndivyo basi mapenzi ndivyo yalivyo. Leo kwako, kesho kwake.
Hakuna sababu ya kuchukiana na kuwekeana visasi kwa sababu kama tutafanya hivyo, kwa dunia ya sasa iliyojaa uchepukaji, itakuwa dunia ya visasi kila kukicha.
Ifahamike kwamba, mapenzi hayana fomula, inawezekana mwenza wako akawa amerubuniwa na kuna siku atarejea kwako na kutulia kama unavyotaka.
Siwatetei wenye tabia ya kuacha, wala siyo tabia nzuri kubadilisha wapenzi, lakini pengine ni ujana ndiyo unamsumbua au ni tabia asili ya mwenza wako, tabia ambayo haipaswi kuigwa na ni hatari kiimani, kimaadili na hata kiafya.
Ninavyofahamu mapenzi ni kitu cha ajabu sana, inawezekana mkawa mmeachana kwa muda kwa maana ya kupumzishana au kuna mtu kaingilia kati penzi lenu au mmeachana moja kwa moja.
Haijalishi ni aina ipi ya kuachana ila ninachozungumzia ni kuachana au kuachwa na kujenga chuki, hakuna sababu kwa namna mapenzi yalivyo kwa sababu utachukia wangapi? Hivi kwa mfano, ukiachwa au kuachana na wapenzi watano na wote ukawachukia, si utakuwa umetengeneza bomu la hatari katika maisha yako? Kwa sababu utakuwa ukiwaona moyo wako unaumia na kuwaza mabaya juu yao.

Kama
mlikuwa mnajua mtakuja kugombana, hamkuwa na sababu ya kuanzisha
uhusiano wa kimapenzi na kama mlilazimishana, kupendana hakuna sababu ya
kuchukiana. Naamini hamkujua kama mtakuja kugombana ndiyo maana mliamua
kupendana na ‘kushea’ baadhi ya vitu vyenu.
Sidhani kama mliamua kuwa wapenzi ili mje kupeana stress (msongo), mgombane, mchukiane, muharibiane maisha na mambo mengine.
Kama umeachwa kwa sababu za msingi, kubaliana na ukweli ili maisha yasonge kuliko kuendelea kufikiria na kutengeneza chuki na uhasama na mtu aliyekuacha au kuachana, haisaidii kitu, kama wewe unavyohisi kutendwa na yeye huko alikokwenda anaweza kutendwa vilevile. Mapenzi ni mchezo usiokuwa na bingwa.
Angalizo; kwa wale wenye tabia ya kuacha hovyo, haipendezi kwani kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyatengeneza bila kujua.
Wanawake huamini kwamba unapomuacha, huwa umemchezea kwa maana ya kutimiza haja zako na unapopata mtu mwingine ‘unamshiti’ bila kujua kuwa uhusiano wa mapenzi ni kama kitabu ambacho kinapaswa kifunuliwe kurasa zake. Inawezekana anayekifunua, akafunua kurasa moja na kukutana na andiko alilokusudia au kufunua kurasa zaidi na zaidi.

UKAWA WAJITOA RASMI BUNGENI, WAONDOKA MJINI DODOMA
8:01 AM
No comments
UMOJA wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo
umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya
kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika vyama vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao kuwa hawajaadhibiwa.
Umoja huo pia umemtaka Rais Kikwete kutotia saini miswada hiyo kwa kuwa imepitishwa kinyume na taratibu.
Mbowe amesema kuwa endapo Rais Kikwete atalazimisha kuisaini miswada hiyo, umoja huo utaishitaki serikali kwa wananchi.
Wabunge wote kutoka UKAWA wameazimia kuondoka kabisa leo kutoka mjini Dodoma, na wanataraji kukutana jijini Dar es salaam siku ya Jumatano kwa hatua zaidi.
Wakati huo huo bunge limepitisha muswada wa usimamizi wa mapato yatokanayo na mafuta na gesi, na muswada mwingine wa uwazi na uwajibikaji katika uchimbaji wa madini, gesi na mafuta, hiyo ikiwa ni miswada miwli kati ya mitatu ambayo imekuwa ikipingwa na wabunge kutoka UKAWA.
Muswada mwingine ni ule wa sheria ya Petroli ambao ulipitishwa jana bila ya ushiriki wa wabunge hao.

#EATV
POLE MSANII BANZA:: HAKIKA TUMWACHIE MUNGU!
8:00 AM
No comments
Ugua pole! Hali ya mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja
‘Banza Stone’ ni ya kumwachia Mungu kwani bado ni tete na watu wamekuwa
wakimiminika kwa ajili ya kumuona katika Hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar alikolazwa.
Mwanamuziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ akiwa katika Hospitali ya Mwananyamala jijini Dar alikolazwa.
Ijumaa Wikienda lilitia maguu kwenye hospitali hiyo na kufanikiwa
kumuona Banza ambaye kwa wakati huo alikuwa amezungukwa na watu
mbalimbali, wakiwemo wanamuziki wenzake wa dansi wengi wakiwa ni wale wa
Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
Kila aliyekuwa akimuona mwanamuziki huyo aliyekuwa akibamba vilivyo kila alipopanda jukwaani, alikuwa akihuzunika huku wasanii wenzake wakiangua vilio kutokana na kutoamini alivyo Banza kwa sasa.
Akipewa kikombe cha uji.
“Yaani inahuzunisha kwani huyu siyo yule Banza tuliyemzoea, hali yake
hii ni ya kumwachia Mungu tu kwani ndiye anayejua kila tatizo
linalomtokea binadamu litaondokaje, kikubwa ni kuendelea kumuombea tu
maana hatua aliyopo siyo nzuri, ni Mungu tu aweke mkono wake,” alisema
mmoja wa wanamuziki ambaye hakutaka jina liandikwe gazetini.
Naye
kaka wa Banza, Hamis Masanja alisema waliamua kumpeleka hospitali
kutokana na hali yake kuwa mbaya ambapo Mkurugenzi wa Twanga Pepeta,
Asha Baraka akiwa na viongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)
walifika nyumbani kwa ajili ya kumjulia hali ndipo wakaafikiana
kumpeleka hospitali.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.
Kwa muda mrefu Banza amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi za kichwani hali iliyomsababishia matatizo ya kutosikia na kutoona vizuri huku akishindwa kabisa kunyanyuka kitandani.
Banza akiwa na afya yake jukwaani.
KUTOKA KWA MHARIRI
Ijumaa Wikienda linaungana na Watanzania kumuombea Banza Mungu amponye kwa neno lake kutoka kwenye Kitabu cha Yeremia 30:17 linalosema:
Ijumaa Wikienda linaungana na Watanzania kumuombea Banza Mungu amponye kwa neno lake kutoka kwenye Kitabu cha Yeremia 30:17 linalosema:
“Kwa maana nitakurudishia afya nami
nitakuponya jeraha zako, asema Bwana kwa sababu wamekuita mwenye kutupwa
wakisema ni Sayuni, ambao hapana mtu autakaye.”
#GPL
Subscribe to:
Posts (Atom)
ZILIZOSOMWA ZAIDI
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ilala Mh. Idd Azzan Madawati yaliyotolewa n...
-
MWAKILISHI wa mtandao wa Alibaba ndiye tajiri mkubwa zaidi nchini Uchina kulingana na rekodi za kampuni yake. Hili imethibitishwa n...
-
Hanging With The Bro! Diamond Platnumz & Kanye West Take A Selfie In L.A. Tanzanian music sensation Chibu Dangote also known has Diam...