Redford
*******
MUIGIZAJI na muongozaji wa filamu wa hollywood Robert Redford amechaguliwa kupokea tuzo ya heshima ijulikanayo kama lifetime achievemnet Award katika tamasha la filamu la New york.
Tunzo hiyo atapokea kutokana na mafanikio aliyoyapata kipindi chote cha ushiriki wake katika utengenezaji wa filamu nchini Marekani.
Redford
Tamasha hilo la filamu ambalo huandaliwa katika viwanja vya Lincolin Centre limemteua Redford kupokea tuzo hiyo ambayo pia hujulikana kama Chaplin Award kutokana na uwezo wake wa kuongoza na kuigiza aliouonnyesha katika filamu nyingi zilizompatia umaarufu.
Waandaji wa tunzo hiyo wanasema kuwa Redford sio tu muigizaji wa kimataifa bali pia ni msanii ambae anapendwa na ameweza kutengeza filamu zake binafsi bila kutegemea kampuni kubwa za utengenezaji wa filamu.
Redford ataungana na orodha ya wasanii wengine waliowahi kupokea tunzo hiyo kama Charlie Chaplin, Elizabeth Taylor na Rob Reiner.
Muigizaji huyo wa filamu za all is lost na captain America atapewa tunzo hiyo katika tamasha la 52 la filamu la new York linalotarajia kufanyika mwezi April mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment