KUNDI
la mawakili wanaomtetea mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar
Pistorius wanasema kuwa viongozi wa mashitaka wamevuruga kesi hiyo kwa
minajili ya kumfanya kuwa na makosa
Kwenye
taarifa yake ya mwisho wakili wa Pistorius Barry Roux amesema kuwa
bwana Pistorius angefunguliwa mashitaka ya kuua bila kukusudia bali si
ya mauaji baada ya kumpiga risasi na kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Bwana Pistorius anasema kuwa alimpiga risi kimakosa akidhani kuwa alikuwa ni jambazi.
Lakini bwana Roux alikiri kwamba Pistorius anapaswa kupatwa na hatia kwa kosa la kutumia silaha yake katika mgahawa.
Wakati kila upande utakapokamilisha kutoa kauli zao ya mwisho jaji ataahirisha kesi hiyo kwa takriban wiki moja kufanya uamuzi.
Mwanariadha
huyo amekanusha makosa yake dhidi yake ikiwemo kosa la kutumia silaha
yake katika sehemu ya umma pamoja na kumiliki silaha haramu.
Chanzo: BBC
No comments:
Post a Comment