Saturday, January 9, 2016

HIZI NDIZO NCHI KUMI ZENYE UTAJIRI BARANI AFRIKA


Leo nina hii orodha ya nchi kumi zenye utajiri barani Afrika

Namba 10 ni Tunisia 
Tunisia wao biashara yao kubwa ni spare za magari pamoja na kuuza mafuta na utalii.

Namba 09 ni Libya 
Imeelezwa kwamba hii ndio nchi ya kwanza Afrika ambayo bado ina akiba ya kutosha ya mafuta ndani ya Afrika mpaka sasa, na hiyo ndio moja ya rasilimali inayoiingizia pesa nyingi nchi hiyo.

Namba 08 ni Angola. 
Inasifika kwa kuwa na madini mafuta na watu wake kujishughulisha zaidi na kilimo jambo ambalo linaifanya nchi hiyo kuingia katika orodha hii ya nchi tajiri Afrika.

Namba 07 ni Kenya 
Hawa ni majirani zetu kabisa wao nao wameingia katika orodha hii ambapo biashara yao kubwa ni chai na kahawa pamoja na bisahara ya kuuza maua kwenda Ulaya ambayo nayo ni biashara ambayo imeonekana kuiingizia pesa nyingi Taifa hilo.

Namba 06 ni Sudan 
Sudani meingia kwenye orodha ya nchi za Afrika tajiri na kipato kikubwa hutokana na kuzalisha pamba duniani

Namba 05 ni Morocco, 
Morocco wao wamejikita zaidi katika uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya utalii, viwanda vya nguo pamoja na kilimo.

Namba 04 ni Algeria
Algeria imeingia kwenye orodha hii ikiwa na sifa kubwa katika uuzaji wa gesi na mafuta.

Namba 03 ni Misri 

Namba 02 ni South Africa 
Sehemu kubwa ya Utajiri wao inatokana na uchimbaji wa madini.

Namba 01 ni Nigeria
Kipato kikubwa cha nchi hii kinatokana na uzalishaji wa mafuta, pia ni nchi ambayo inasifika kwa kuwa na idadi kubwa ya watu.

No comments:

Post a Comment