Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu
la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Meck Sadiki.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akielekea eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015.
Waziri
Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la
Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya
usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.
Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Meck Sadiki na Kushoto
kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya
usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015.
Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri
Mkuu,Kassim Majliwa akiwa amezongwa na wananchi wakati alipokwenda
kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam kufanya usafi Desemba
9, 2015.
Baadhi
ya washiriki wa zoezi la usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar
es salaam wakipiga picha kwa kutumia simu wakati Waziri Mkuu, Kasim
Majaliwa alipozunguza nao baada ya kufanya usafi sokoni hapo Desemba
9, 2015.
Gari
alilopanda Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa likitoka kwenye eneo la soko
kuu la Kariakoo alikokwenda kushiriki katika kufanya usafi Desemba 9,
2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema zoezi la usafi lililofanyika leo nchini
kote lisiishie hapo bali liwe endelevu ili Tanzania iwe na taswira nzuri
kwa wageni wanaoingia nchini.
Ametoa
wito huo leo kwenye soko la Kariakoo wakati akishiriki zoezi la kufanya
usafiikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la
kutaka maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru yasiwepo na badala yake watu
wote washiriki kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia amewataka viongozi wa soko la Kariakoo wafike ofisini
kwake Jumatatu ijayo (Desemba 14, 2015) saa 4 asubuhi ili wamueleze
wana mikakati gani ya kuboresha utoaji huduma kwenye soko hilo.
“Natambua
kuwa siyo sahihi kupanga chini biashara tulizonazo. Nataka hawa
viongozi waje wanieleze wana mpango gani endelevu wa kuboresha soko
hili,” alisema Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Waziri
Mkuu ambaye alienda kufanya usafi kwenye soko hilo, alilazimika
kuzungumza na mamia ya wananchi waliofika kushiriki zoezi hilo. Pia
alikagua maeneo mbalimbali ya soko hilo hadi shimoni na kusema
aneridhika na usafi uliofanyika bali amesisitiza usafi huo uendelezwe.
“Kaulimbiu
ya Mheshimiwa Rais Magufuli ya HAPA KAZI TU inatupa ari ya kufanya
kazi. Fanyeni kazi. Watanzania mko huru kufanya kazi yoyote lakini cha
msingi fuateni taratibu na kanuni. Serikali hii tumamua kuwajali watu wa
chini. Tutahakikisha wajasiriamali wadogo, akinamama lishe na
wamachinga mnafanya kazi kwa amani na utulivu, ” alisema.
Rais
Magufuli aliamua kuitangaza siku ya leo (Desemba 9, 2015) ambayo ni
maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru iwe ni siku ya kufanya usafi nchi nzima
ili kuepukana na magonjwa mbalimbali na hasa kipindupindu.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
DAR ES SALAAM.
No comments:
Post a Comment