Rose Ndauka katika ubora wake wakati wa utayarishaji wa kipindi cha Mkasi kinachotarajiwa kurushwa Jumatatu hii ya Novemba 23.
Na Andrew Chale
Msanii wa Filamu za kibongo, Rose Ndauka, anatarajia kufunguka mambo mbalimbali katika kipindi cha luninga cha kila wiki cha Mkasi. Kwa mujibu wa mtandao wa kijamii wa kipindi hicho cha Mkasi umetupia picha cha star huyo wa Bongo na kueleza kuwa naye siku hiyo ya Jumatatu.
Kipindi hicho bora kabisa ndani ya Afrika Mashariki na kujizolea mashabiki lukuki sehemu mbalimbali za nchi za Afrika ikiwemo Afrika Mashariki. Rose Ndauka anatarajiwa kukabiliwa na maswali makali kutoka kwa mwendeshaji Mkuu wa kipindi hicho, Salama Jabir. Kipindi cha Mkasi kinachorushwa hewani kupitia kituo cha EATV.
Rose Ndauka..
Utayarishaji wa kipindi hicho ukiendelea..
Mmoja wa waandaji wa kipindi cha Mkasi ..
No comments:
Post a Comment