WANAWAKE wa mjini wanasema makubwa, madogo yana nafuu! Msemo huo unakwenda sambamba na tukio la hivi karibuni la mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Rukia Mabeseni mkazi wa Kigogo jijini Dar kukodi ngoma ya kibao kata kwa lengo la kwenda kumsuta shoga yake aitwaye mama Mariam.
Rukia Mabeseni akimsuta shoga yake pamoja na wenzie.
Ilikuwaje? Msikie Rukia Mabeseni
“Shost wangu, huyu mama Mariam huyu aliwahi kumzawadia mwanangu baiskeli katika sherehe yake ya kuzaliwa, nikashukuru na nikajua shoga ninaye.“Cha ajabu juzijuzi hapa alikuwa na sherehe yake, bahati mbaya mimi sikuwa kwenye hali nzuri, nikampelekea zawadi ndogo, hee! Kumbe mwenzangu hajaridhika.
“Si akaanza kunisema vibaya kwa watu, eti kama hali yangu ilikuwa mbaya kwa nini sikusema mapema badala ya kumpelekea matambara, kwa kweli iliniuma sana.“Ndiyo nimeamua kumrudishia zawadi yake ya baiskeli kwa staili hii ili aweke kumbukumbu kuwa alichonifanyia si kitu kizuri,” alisema Rukia.
Wakizidi kumsuta.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyekuwa eneo la tukio, Rukia akiwa na wapambe wake waliokuwa wamevalia sare za madera kufika nyumba kwa mama Mariam, hakufungua mlango kwa kukwepa aibu.Ikaelezwa kuwa, baada ya kundi hilo la wanawake lililokuwa likicheza kwa staili ya kukata mauno kuondoka, msutwaji huyo aliamua kukimbilia Kituo cha Polisi cha Kigogo kutoa taarifa akihisi kuwa watamrudia tena na kumfanyia vurugu.
Hata hivyo, baada ya Rukia kusikia kuwa wameenda kushitakiwa, walirudi tena ambapo safari hii mama Mariam alikubali yaishe kwa kuomba msamaha. “Ameomba msamaha na amefuta kesi kwa sababu alisema kuwa alighafirika tu, hata hivyo alinipigia simu na kuniambia anaumwa anaomba tuongee yaishe ikibidi tukamuone tumalize tofauti zetu,” alisema Rukia.
No comments:
Post a Comment