MAHAKAMA ya usuluhishi wa kimichezo (CAS) imetupilia mbali rufaa ya klabu ya Barcelona na kutangaza kuifungia klabu hiyo kutofanya usajili kwa muda wa mwaka mmoja kutokana na kukumbwa na kashfa ya kusajili wachezaji chini ya umri wa miaka 18.
Hatua hii inafuatia kutupiliwa mbali kwa rufaa iliyowasilishwa na klabu hiyo ikipinga kufungiwa kusajili kutokana na kuvunja sheria ya kuwasajili wachezaji mwenye umri Chini ya miaka 18.
Barcelona ambayo iko katika nafsi ya pili katika msimamo wa ligi kuu nyuma ya Real Madrid imezuiliwa kusajili katika dirisha dogo la usajili la mwezi January,pamoja na kipindi cha dirisha la usajili la majira ya joto.
Hii ina maana kuwa klabu hii itaruhusiwa kusajili wachezaji kuanzia January 2016 ambapo pia imetozwa faini ya dola za kimarekani 455,000.
Mapema mwezi April mwaka huu shirikisho la soka duniani FIFA lilitangaza kuifungia klabu ya Barcelona kufanya usajili baada ya kufanya uchunguzi na kubaini kuwa kati ya mwaka 2009 na 2013 Barcelona ilikiuka sheria kwa kusajili wachezaji 10 waliokuwa na umri wa chini ya miaka 18.
Mapema klabu ya Barcelona iliamua kupinga maamuzi hayo kwa kukata rufaa katika mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa kimichezo.
No comments:
Post a Comment