Chanel Tapper, mwanafunzi wa California nchini Marekani anashika rekodi ya kuwa na ulimi mrefu kuliko dunia nzima. Ulimi wake una urefu wa sentimeta 9.75 (inchi 3.8).
Ulimi wake ni mara mbili ya ulimi wa binadamu wa kawaida, na una upana kama kiganja cha mkono.
Chanel aligundua kuwa ana ulimi mrefu kuliko kawaida alivyokua ana miaka nane akipiga picha na mama yake uku wakiwa wametoa ndimi zao nje. Mama yake alivyoiangalia ile picha alishtuka na kushangazwa na urefu wa ulimi wa mwanae na toka hapo watu wengine wakawa wanamuongelea pia.
Anasema kila anapotoa ulimi wake nje watu hubaki na butwaa na kumuambia awaonyeshe tena kwani hawaamini wanachokiona. Watu wengine hushtuka sana na kuanza kuwaambia watu wengine waje kuona.
Wengine humuuliza kama ulimi wake unaweza kugusa pua yake na maswali mengine kadhaa. Kila anayeona ulimi wa Chanel inabaki kuwa kumbukumbu isiyosahaulika kwake na ataendelea kusimulia kwa wengine.
No comments:
Post a Comment