WAWAKILISHI
wa Tanzania katika michuano ya CECAFA Nile Basin Cup, Mbeya City fc
wameaga mashindano hayo baada ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Victoria
University ya Uganda katika mchezo wa robo fainali uliomalizika dakika
chache zilizopita mjini Khartoum.
Mbeya
City wametolewa katika michuano hiyo wakiwa wameshinda mechi moja,
kufungwa moja na kutoka suluhu mechi moja katika hatua ya makundi.
Lakini wamepoteza mechi ya pili katika mashindano haya baada ya kufungwa hatua ya robo fainali na kufungashiwa virago.
Afisa habari wa Mbeya City fc, Freddy Jackson amesema wanashukuru kwa kilichotokea kwani ndio matokeo ya mpira wa miguu.
Freddy amesema wachezaji wamejitahidi kucheza kwa juhudi, lakini hawakuwa na bahati.
“Ndugu
tunashukuru kwa maombi yenu, alichotupangia mungu ndicho tulichopata.
Mechi imemalizika , Mbeya city O victoria 1, hivyo basi tumeyaaga
mashindano”. Amesema Freddy.
No comments:
Post a Comment