wahamiaji kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika
Mamlaka nchini Libya imesema kuwa imeshindwa kudhibiti idadi ya wahamiaji wanaotaka kuingia Ulaya kwa kutumia mlango wa nyuma.
Inadaiwa kuwa zaidi ya raia laki tatu wamo nchini Libya wakitaka kuvuka bahari ya Mediterenean.
Walinzi
wa pwani ya Libya wameiambia BBC kwamba wamepata miili zaidi baharini,
ya watu ambao wamepoteza maisha yao kwa kutaka kuvuka bahari hiyo.
Wale wanaokamatwa wakitaka kuanza safari hiyo huwekwa katika jela ndogo ambazo zimejengwa katika pwani ya bahari hiyo.Mwandishi wa BBC katika mji wa bandari ya Misrata amesema kuwa Libya sasa ndio mlango wa raia wa afrika kuingilia Ulaya.
Muungano wa Ulaya umeonya kuwa mwaka 2014 utakuwa na wahamiaji wengi watakaowasili katika fukwe za mataifa ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment