Afisa Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya
Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera akieleza kwa waandishi wa Habari (hawapo
pichani) kuhusu mfumo mpya wa kielektroniki wa ukusanyaji mapato unatumiwa na manispaa hiyo,wakati wa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari(MAELEZO) Fatma Salum.
Mchambuzi wa Mifumo ya Komputa Bw. Jackson Kiema
akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) mashine ya kielektroniki
inayotumika katika ukusanyaji wa mapato na kuhifadhi taarifa za mapato, wakati
wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Afisa
Uhusiano wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Bw. Sebastian Mhowera.
Picha na Hassan Silayo - MAELEZO
***************************************
MFUMO
MPYA WA UKUSANYAJI WA MAPATO
Kutokana na kukua kwa sekta ya
mawasiliano nchini, Manispaa ya Kinondoni imeanzisha utaratibu wa ulipaji wa
kodi kwa kutumia huduma ya simu za mkononi na Max-malipo.
Huduma hiyo mpya inayotolewa kupitia
mfumo unaojulikana kama “e–payment system”,humwezesha mwananchi kulipa kodi
yake muda wowote, kwa haraka na urahisi na mahali popote.
Huduma hii inatolewa na Manispaa kwa
kushirikiana na wakala anayetambulika kama “Max-malipo” ambaye kupitia huduma
zake mitaa 171 iliyopo katika Kata 34 imeunganishwa katika mifumo hiyo ya
ulipaji kodi.
Mfumo huu wa ukusanyaji wa kodi
ndani ya Manispaa ni hatua ya utekelezaji unaozingatia maelekezo ya waraka wa
Serikali Na. 5 wa mwaka 2009 unaohamasisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa Umma, kwa
ufanisi na kwa wakati.
Kimsingi hatua hii inahamasisha
ushirikishwaji wa wananchi katika utoaji wa maamuzi yanayohusu mambo yao na
kuwezesha uwepo wa Serikali iliyo wazi, inayowajibika na makini katika
kutekeleza majukumu yake kwa Taifa.
Hivyo basi kutokana na malengo na
umuhimu wa kuwarahisishia wananchi, Manispaa iliona ni vema ikaingia haraka
ndani ya utaratibu huu ili Mwananchi aweze kulipia kodi popote kwa kutumia Max-malipo au wakala wa simu za mkononi
yaani Tigo pesa Na. 212888 na M-Pesa Na. 212888.
MAFANIKIO
YALIYOPATIKANA.
Katika kipindi kifupi cha muda wa
miezi 3, tangu mfumo huu mpya ulipoanzishwa rasmi kumekuwa na mafanikio makubwa
kama ifuatavyo:-
Mapato
yameongezeka kwa kiwango kikubwa mfano; ada ·
ya
kuchangia huduma za Afya (Cost sharing) imeongezeka kutoka Tshs. 45,000,000/=
kwa wiki hadi kufikia Tshs. 65,000,000/= kwa wiki, sawa na ongezeko LA 69%
·
Chanzo
cha kodi ya majengo hadi mwishoni mwa Machi tulikusanya Tshs. 339,000,000/= tofauti na awali ambapo hadi kipindi kama mwaka
2013 tulikusanya sawa na ongezeko la asilimia 269 hiki Tshs. 126,000,000/=
Maeneo
mengine ongezeko la mapato limezidi bajeti ya mwaka iliyotakiwa kukusanywa. Kwa
mfano katika ushuru wa huduma za jiji (City Service Kavy) ambapo tumezidi kwa 18% ·
Ushuru
wa Masoko umeongezeka kwa wastani wa asilimia 20 ya lengo la kila mwezi.
·
Lesseni
za biashara hadi Machi tumekusanya Tshs. 2.4 Bilioni sawa na 93% ya bajeti ya
Manispaa ya chanzo hiki ya Tshs. 2.6 Bilioni kwa mwaka.
Napenda kuwahakikishia wananchi wa
Kinondoni kuwa Manispaa ya Kinondoni itazidi kuboresha huduma zake ili kuweza
kufikia malengo yaliyokusudiwa na kuwawezesha kuwa na maisha bora kutokana na
mafanikio haya, lipa.
Lipa kodi kwa maendeleo ya Manispaa
yako.
IMETOLEWA NA
SEBASTIAN
MODESTUS MHOWERA
AFISA
UHUSIANO WA MANISPAA
HALMASHAURI
YA MANISPAA YA KINONDONI
SIMU
NA:
0754-227024
No comments:
Post a Comment