Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement
Mshana (kushoto) pamoja na Mshauri wa mambo ya Utamaduni Bw. Lzu Dong (kulia)
wakipeana zawadi mara baada ya Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya
Kijana (Jin Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es
Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Elisante Ole Gabriel akifurahi mara baada ya kukata utepe kama ishara
ya kuzindua Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin
Tai Lang) uliofanyika jana katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Clement
Mshana akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kwajili ya
kuzindua rasmi Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang)
uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Naibu
Kati u Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo Elisante Ole Gabriel akitoa hotuba yake mbele ya viongozi
mbalimbali
wakati wa Uzinduzi wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai
Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu Kampuni ya Star Media (T) Ltd Bw. Jack Czhou
akieleza jambo wakati wa Uzinduzi huo wa Tamthilia ya Mapenzi na Furaha ya Kijana
(Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na
wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya
Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati
wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang)
uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi toka Kampuni ya Star Media (T0 Ltd na
wasanii waliotumika kuweka lugha ya Kiswahili katika Tamthiliya ya Furaha ya
Kijana (Jin Tai Lang) wakisikiliza kwa makini hotuba toka kwa mgeni rasmi leo wakati
wa Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana (Jin Tai Lang)
uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya mgeni rasmi, Watendaji na Viongozi
mbalimbali mara baada ya Uzinduzi wa Tamthiliya ya Mapenzi na Furaha ya Kijana
(Jin Tai Lang) uliofanyika katika Viwanja vya TBC jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Benedict Liwenga
************************
Na Benedict Liwenga - MAELEZO
SHIRIKA la Utangazaji Tanzania (TBC) na Shirika la Radio ya
Kimataifa ya Jamhuri ya Watu wa China (CRI), kwa pamoja yameshirikiana katika
sherehe ya Uzinduzi wa Tamthiliya ijulikanayo kwa jina la MAPENZI NA FURAHA YA KIJANA (Jin
Tai Lang) ambayo imechezwa na China
na kuwekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili na wasanii wa Tanzania.
Sherehe hiyo imefanyika katika Viwanja vya TBC ikishuhudiwa
na mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Elisante Ole Gabriel akiwemo Mwakilishi wa Balozi toka Ubalozi wa China nchini
Tanzania, Wajumbe wa Bodi ya Wakaurugenzi TBC, Mkurugenzi Mkuu Star Media
Tanzania, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara mbalimbali na wafanyakazi.
Hatua ya uzinduzi wa sherehe hiyo ni matokeo ya utekelezaji
wa Sera ya Serikali ya kujenga mahusiano na ushirikiano na nchi rafiki kupitia
nyanja mbalimbali ikiwemo habari, Utamaduni na michezo.
“Pamoja na kutekeleza sera za Serikali pia TBC tunatambua
umuhimu wa kuwa na michezo ya kuigiza ambayo inazingatia utamaduni wa
Watanzania na niwahakikishie kuwa Tamthiliya hizi zimeonesha hali hiyo.”.
Alisema Mkurugenzi Shirika la Habari Tanzania Clement Mshana.
Mashirika ya habari ya TBC na CRI yamekuwa mstari wa mbele
katika kuimarisha ushirkiano nah ii ni mara ya tatu kuwa na Tanmthiliya ya
Kichina iliyowekwa sauti kwa lugha ya Kiswahili ambapo mwaka 2012 kulikuwa na
tamthiliya ya MAU DOU DOU NA VISA VYA MAMA WAKWE ZAKE,
ikifuatiwa na tamthiliya mbili nyingine ya MAISHA
YA MAMA na FURAHA YA BABA ambazo
zote zimepata umaarufu.
No comments:
Post a Comment