Wednesday, December 5, 2012

A/MASHARIKI: WAKENYA WAONYWA JUU YA WASHUKIWA WA MAHAKAMA YA UHALIFU

Aliyekuwa katibu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan, amewaonya wakenya kuhusu hatari ya kuwachagua wagombea uarais ambao wanakabiliwa na kesi katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita iliyopo the Hague.

Akizungumza mjini Nairobi, Annan amesema kumchagua Uhuru Kenyatta na William Ruto katika uchaguzi wa mwakani utatatiza uhusiano wa Kenya na ulimwengu mzima.

Mwandishi wa BBC mjini Nairobi anasema huenda wagombea hao wakajibu onyo alilotoa Annan kwa hasira.
Ingawa hakuwataja kwa majina, naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta na William Ruto, bwana Annan aliambia BBC kuwa kiongozi yeyote anapaswa kuwa na uwezo wa kusafiri na kukutana na viongozi wengine wa kimataifa.

"wakati unapomchagua kiongozi ambaye hawezi kufanya hivyo, ambaye hatakuwa huru kufanya hivyo au kupokelewa , sio kwa manufaa ya nchi na nadhani watu wote wataweza kuelewa hilo,'' alisema Annan.
Wanasiasa hao wawili wanatakikana katika mahakama ya ICC kuhusiana na jghasia za baada ya uchaguzi mwaka 2007
 
Uhuru Kenyatta na William Ruto wanatakikana na mahakama ya ICC kuhusiana na ghasia za mwaka 2007
Duru zinasema kuwa serikali nyingi hazipendi kujihusisha moja kwa moja na wanasiasa ambao ni washukiwa wa uhalifu na ambao wanatakikana katika mahakama ya ICC.

Anasema kuwa matamshi ya Annan huenda yakawaghadhabisha sana Ruto na Uhuru lakini haijulikani ni kwa kiasi gani yataweza kuwashawishi wapiga kura kutowapigia kura wawili hao.

Ingawa Koffi Annan anaheshimiwa sana, wakenya wengi bado wana mazoea ya kupiga kura kwa misingi ya kikabila.

No comments:

Post a Comment