Thursday, November 1, 2012

VITUO VYA MAFUTA VYAANZA KUTOA HUDUMA NCHINI KOTE.

Baadhi ya wateja Jijini Dar wakiwa katika foleni wakisubiri huduma baada ya Vituo hivyo kuanza kutoa huduma ya mafuta (Picha na theeastafrica blog)
Baadhi ya vituo vingi vya mafuta jijini Dar es salaam vimetii agizo la Serikali la kuuza mafuta kwa bei elekezi baada ya kutouza nishati hiyo kwa muda , huku vingine vikiwa bado vimefungwa kwa takribani muda wa siku tano mfululizo.

Watumiaji wa petrol jijini hapa wameonja adha ya kukosekana kwa mafuta ya petrol, huku wakitembea umbali mrefu kutafuta nishati hiyo, na wengine kuacha kabisa magari majumbani.

Upatikanaji wa nishati hiyo umekuja baada ya mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji EWURA kutoa bei elekezi kwa wafanyabiashara ya mafuta.

Hata hivyo habari kutoka baadhi ya mikoa hapa nchini, zinaeleza kuwa nishati hiyo imekosekana, huku mkoa wa Ruvuma ukielezwa kuwa kuathirika zaidi, na kusababisha baadhi ya biashara kusimama.

No comments:

Post a Comment