Katika kuhakikisha kuwa Radio Mlimani
inaendana na ulimwengu wa Sayansi na teknolojia katika ukusanyaji na
usambazaji wa habari, Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano
kwa Umma ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imemualika mtaalam kutoka
nchini Finland Markiku Liukkonen kwa ajili ya kutoa mafunzo juu ya
utangazaji wa redio kwa njia ya mtandao (podcasting) kwa watangazaji
wa Radio Mlimani.
|
Baadhi ya watangazaji wa Mlimani Redio wakipokea mafunzo kutoka
kwa mtaalam kutoka
nchini Finland Markiku Liukkonen (Aliesimama kushoto) |
Mafunzo hayo ya siku mbili
yamefunguliwa na Coordinator war Radio Mlimani Bw. Ernest Mrutu
ambapo amesema kuwa baada ya watangazaji hao kupewa mafunzo hayo
Radio Mlimani itasikika duniani kote kwa njia ya mtandao kwani
wataweza kurusha vipindi vya radio kupitia internet (podcasting).
|
Mmoja wa wapokeaji wa mafunzo hayo bw. Njonjo Mfaume akipitia kwa makini baadhi ya vitu muhimu alivyoelekezwa na mtaalamu huyo. |
No comments:
Post a Comment