Friday, November 30, 2012

CHADEMA YAJITATHMINI KINONDONI

 Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Dk Willibrod Slaa akifungua Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kinondoni kuhusu Uhai wa Chama uliofanyika Makao Makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto ni Ofisa wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwita Mwikwabe Waitara na Naibu Katibu Mkuu Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Subira Waziri (wa tatu kulia).
 Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akizungumza na wajumbe waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo la Kinondoni
 Ofisa wa Sera na Utafiti wa Chadema, Mwita Mwikwabe Waitara
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria katika mkutano huo.
(Picha na Habari Mseto Blog)

AIRTEL YAMUANDALIA PARTY AY KUMPONGEZA KWA KUPATA USHINDI

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Airttel Tanzania, Ambwene Yessaya 'AY' akiwa ameshika tuzo hiyo aliyozawadiwa hivi karibuni katika mashindano ya Chanel-O huko Afrika Kusini.
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava) kwa pamoja wakionyesha tuzo ya  Channel O  aliyoipata Mwanamuzi huyo nchini Afrika Kusini. Tukio hilo limefanyika leo wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY kwa ushindi alioupata pamoja na kumwandalia sherehe ya kumpongeza itakayofanyika leo usiku nyumbani Lounge jijini Dar es Salaam 
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongo flava)  na Balozi wa Ambwene Yessaya 'AY' akiwashukuru watanzania kwa kumpigia kura na kumwezesha kupata tuzo hiyo kulia ni Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde na kushoto ni  DJ wake Athur Baraka.
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari ambapo Airtel imempongeza AY balozi wake kwa kupata tuzo ya chanel O ya video bora, Katikati ni AY  akifatiwa na DJ wake Athur Baraka.

TANZANIA YAKITAKA KITUO CHA CNN KUACHA UPOTOSHAJI JUU YA MPAKA WA TANZANIA NA MALAWI

SERIKALI ya Tanzania imekitaka kituo cha televisheni cha Kimataifa cha CNN kusahihisha taarifa potofu ilizotoa kuhusu mgogoro wa mpaka unaoendelea kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa.

Taarifa hizo zinaonyesha kwamba mpaka wa Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa upo kwenye ufukwe wa Pwani ya Tanzania jambo ambalo Serikali imesema siyo sahihi.

Akiongea na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene amesema Serikali ya Tanzania imesikitishwa sana na taarifa hiyo na kuitaka CNN kuisahihisha mara moja.

“Tumesikitishwa sana na taarifa hiyo na tunashangaa kuona chombo kikubwa kama CNN wanaweza kutoa taarifa za uongo kwa kiasi hicho” amesema Bw. Mwambene.

Amesema ukweli ni kwamba unapozungumia eneo la Tanzania kilometa za mraba 947,300 (947,300 sq km)  ikiwa ni pamoja na  nusu ya eneo la ziwa kaskazini mwa mpaka wa Tanzania na Msumbiji na kwamba mpaka upo katikati ya ziwa kama ilivyo kwa mpaka wa Malawi na Msumbiji.

Kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 24 Novemba, 2012, CNN International yenye makao yake Makuu nchini Marekani  imekuwa ikiendesha  kipindi kuhusu mgogoro wa Tanzania na Malawi na kuonyesha kwamba mpaka uko pembezoni mwa ufukwe wa Tanzania.

Bw. Mwambene amesema kuwa suala hilo hivi sasa linatarajiwa kupelekwa katika Baraza la Marais wastaafu wa Nchi za Umoja wa SADC kwa ajili ya kulitafutia ufumbuzi.

Wakati huo huo, Sherehe za miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam Desemba 9 mwaka huu.

Kauli mbiu za sherehe za uhuru mwaka huu ni uwajibikaji , uadilifu na uzalendo ni nguzo ya maendeleo ya Taifa letu.

IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI

Thursday, November 29, 2012

WILDAF NA SIKU 16 DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TZ

Ni katika maandalizi ya Kipindi cha JAHARA kinachorushwa kila siku za wiki kuanzia Jumatatu mpaka Jumamosi, Pichani ni Mtangazaji wa kipindi hicho Bw Spencer Lameck na Bi. Anna Kulaya ambaye ni Afisa Mwandamizi katika shirika ambalo si la Kiserikali WILDAF.
Bi. Ana Kulaya akiongea juu ya shirika la WILDAF lakini zaidi akieleza jinsi shirika hilo linavyofanya kazi, lakini pia akapata fursa ya kuielezea Kampeni ya SIKU 16 DHIDI YA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA TANZANIA kampeni ambayo imefanyika hivi karibuni lakini pia hufanyika kila mwaka mnamo tarehe 25 Novemba kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya wanawake na watoto.
Bi. Jackline Waya,pia ni Afisa mmojawapo katika shirika la WILDAF ambapo akapata fursa ya kuelezea malengo ya kampeni hiyo na zaidi malengo ya Shirika hilo.

USIKOSE KUANGALIA KIPINDI HIKI CHA JAHARA IFIKAPO SIKU YA IJUMAA SAA MOJA MPAKA SAA MOJA NA NUSU ASUBUHI.

KAMA UNA JAMBO AMBALO NI LA MANUFAA KWA UMMA WA WATANZANIA NA UNGEPENDA UMMA HUO ULIPATE, BASI KATIKA KIPINDI HIKI UTAPA FURSA HIYO, WASILIANA NA MTAYARISHAJI NA MHARIRI WA KIPINDI HIKI KWA NAMBA ZIFUATAZO: +255 652 294 780, +255 719 583 949

WAOMBOLEZAJI: ''SAFARI NJEMA SHARO WETU''

ULIMWENGU WA HABARI KATIKA PICHA
Jeneza  lenye  mwili wa Sharo Milionea  likitolewa 


Wananchi  wakiwa na huzuni wakati  mwili wa Sharo Milionea  ukitolewa 



Umati  wa  waombolezaji  wakiwa nyumbani kwa Sharo Milionea 

Shekh akiombea  mwili  wa jeneza  leye mwili wa Sharo Milionea


Waumini wa dini ya kiislamu  mkoani Tanga  wakiufanyia  dua za mwisho mwili wa Sharo Milionea 

 Mwili wa Marehemu Sharo Milionea ukiswaliwa hapo jana kabla ya kupelekwa kwenye nyumba yake ya milele 
Hapa  ndipo  mwili wa Sharo Milionea  ulipohifadhiwa
 Rafiki mkubwa wa marehemu Sharo Milionea, Mzee Majuto akiwa ameshikwa mkono wakielekea kwenye mazishi, Muheza mkoani Tanga.

MAMIA ya wakazi  wa mkoa  wa Tanga pamoja na  wasanii wa  kundi la Bongo Movie wameshiriki kikamilifu katika mazishi ya msanii Sharo Milionea yaliyofanyika  wilayani Muheza mkoani Tanga eneo la umbali wa takribani kilometa 2 kutoka nyumbani  kwa msanii  huyo.

Imedaiwa kuwa umati  mkubwa wa wananchi wamejitokeza kwa wingi  kuuaga mwili  wa msanii  huyo huku  baadhi  wakigombea  kuaga mwili  huo, kitendo kilichopelekea upotevu wa amani kwa muda.

Hata  hivyo  vurugu hizo zilidaiwa kutokea  wakati  wa  kuuaga mwili ambapo  kila mmoja aliyejitokeza eneo hilo alitaka  kuugusa  mwili  wa Sharo Milionea .

Miongoni  mwa  viongozi  wa  vyama  vya  siasa  waliofika  ni pamoja na  Nappe Nnauye, Mukama, huku Miongoni  mwa  wasanii wa Bongo Movie waliofika hapo ni pamoja na Vicent Kigosi 'Ray', Kitale pamoja na wengine wengi.

Mwili  huo  umezikwa  eneo la umbali  wa kilomita  2  kutoka  nyumbani kwao marehemu. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU SHARO, PEMA PEPONI. AMIN!

Habari kwa hisani ya mtandao wa francis godwin

HOSPITALI YA SINZA, YALALAMIKIWA KWA KUCHAFUA MAZINGIRA


WANANCHI waishio karibu na hospitali ya Sinza Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam wameilalamikia hospitali hiyo kwa kitendo cha kuchoma taka ambazo moshi wake unawaathiri kiafya kwa namna moja ama nyingine kwani huuvuta pindi taka hizo zinapochomwa.
Eneo la nyuma la Hospitali hiyo ambalo bomba lake limekuwa likilalamikiwa kutoa moshi mkali ambalo umekuwa ni kero kwa wakazi hao.
Bomba linalolalamikiwa kuwa linatoa moshi unaowaathiri wakazi karibu na hospitali hiyo.
Bomba likionekana kutoa moshi, kitu ambacho kimekuwa ni kero kwa wakazi hao kwani huishia maeneo ya karibu. 










STARS KUINGIA KAMBINI BAADA YA CHALENJI

Release No. 186
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 28, 2012

STARS KUINGIA KAMBINI BAADA YA CHALENJI
Timu ya Taifa (Taifa Stars) inatarajia kuingia kambini baada ya kumalizika michuano ya Kombe la Chalenji inayofanyika Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole jijini Kampala, Uganda. Michuano hiyo iliyoanza Novemba 24 mwaka huu itamalizika Desemba 8 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen, Stars itaingia kambini kujiandaa kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia (Chipolopolo) itakayochezwa Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Baada ya pambano dhidi ya Chipolopolo, wachezaji watapata mapumziko ya wiki mbili kabla ya kuingia tena kambini Januari 6 hadi 20 mwakani kwa ajili ya mechi nyingine za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Morocco.

Kim anatarajia kuongeza kipa mmoja kwenye kikosi chake ili kuwasaidia nahodha Juma Kaseja na Deogratias Munishi pamoja na chipukizi kadhaa kutoka timu za Taifa za vijana za Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.

Vilevile Kim anafuatilia wachezaji wengine kwenye timu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) ambayo pia inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji ikiwa katika kundi C pamoja na timu za Eritrea, Malawi na Rwanda.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Tuesday, November 27, 2012

Monday, November 26, 2012

SHARO MILIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI

Msanii maarufu wa Luninga, Sharo Milionea (pichani), amefariki dunia leo katiak ajali ya gari iliyotokea kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga. Kamanda wa Polisi Tanga, Constantine Massawe, amethibitisha kutokea kifo cha msanii huyo aliyekuwa aliyekuwa na vipaji vingi ikiwemo kuimba na kufanya michezo ya runinga.
 
MSANII nyota wa vichekesho na muziki wa kizazi kipya nchini, Hussein Ramadhani, maarufu kwa jina la Sharo Milionea amefariki dunia kwa ajali ya gari jana saa mbili usiku katika barabara ya
Segera-Muheza wakati alipokuwa akitoka Dar es Salaam kwenda Muheza.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Constantine Massawe amesema kwa njia ya simu kuwa, Sharo alipata ajali katika eneo la Maguzonizoga wilayani Muheza baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha barabara na kupinduka mara kadhaa.

Kwa mujibu wa Kamanda Massawe, marehemu Sharo alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR na kwamba alikuwa peke yake kwenye gari.

Kamanda alisema hakukuwa na kona kali sana wala ubovu wa barabara kwenye sehemu aliyopata ajali Sharo Milionea na kwamba gari hilo limehifadhiwa mahali salama kwa sababu halitembei.

Kamanda Massawe alisema mwili wa marehemu Sharo umehifadhiwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza.

Marehemu Sharo alianza kujipatia umaarufu baada ya kushiriki kwenye filamu za vichekesho zilizokuwa zikitayarishwa na msanii mkongwe wa fani hiyo, Amri Athumani maarufu kwa jina la King Majuto.

Baadaye alijitosa kwenye fani ya muziki wa kizazi kipya, ambapo alifanikiwa kuteka soko la muziki huo baada ya kuibuka na kibao cha Chuki za nini.

Hivi karibuni, Sharo alijiongezea umaarufu zaidi baada ya kushiriki kutengeneza matangazo ya Kampuni ya Simu moja hapa nchini akiwa na King Majuto.

Mtandao huu wa ULIMWENGU WA HABARI unatoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki pamoja na wapenzi wa kazi za marehemu Sharo Milionea.
Habari na Liwazozito

Sunday, November 25, 2012

MAKAMU WA RAIS AZINDUA MKOA MPYA WA KATAVI


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe wakizindua rasmi mkoa wa Katavi kwa kuweka jiwe la msingi katika kilima cha kijiji cha Kabungu kwa ajili ya kujenga kituo cha kumbukumbu ya historia ya mkoa wa Katavi, Kijiji Cha Kabungu ndipo palipozaliwa Wilaya ya Mpanda Mwaka 1947 na Boma la mtawala wa kwanza wa kikoloni Mpanda lilijengwa hapo, baada ya uwekaji wa jiwe la msingi kijijini Kabungu, Makamu wa Rais alirejea mjini mpanda katika viwanja vya Kashaulili ambapo kumefanyika shughuli mbalimbali za uzinduzi rasmi wa mkoa huo na hotuba mbalimbali zikienda sambamba na sherehe za ngoma za makabila mbalimbali ya asili ya mkoa wa Katavi. PICHA NA FULLSHANGWE BLOG.COM.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Mh. Paza Mwamlima huku akipungia mkono wananchi waliofika kumlaki na kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi kijijini hapo.
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kabungu wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kuzindua mkoa wa Katavi, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajab Rutengwe na kutoka kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi Bw. Mselem Said.
Mkuu wa mkoa wa Katavi akimkaribisha Makamu wa Rais Dt. Gharib Bilal ili kuongea na wananchi wa kijiji cha Kabungu. 
Msafara wa magari ya Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal ukiwasili katika eneo lilipowekwa jiwe la msingi kwa uzinduzi wa mkoa wa Katavi katika kilima cha kijiji cha Kabungu Mkoani Katavi.
Wazee waasisi wa kijiji cha Kabungu wakinyanyua matawi ya miti juu kama ishara ya kumpokea Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal wakati alipowasili katika kijiji hicho leo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakiimba wimbo mara baada ya Makamu wa Rais kuwasili kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda tayari kwa Sherehe za kuzindua mkoa wa Katavi
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akimsikiliza Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati wa uzinduzi wa mkoa wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili kulia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt. Mary Nagu.
Kutoka kulia ni Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal, Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe, Naibu Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye, Mkuu wa mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Issa Machibya wakiwa katika sherehe za uzinduzi huo.
Baadhi ya wawekezaji waliohudhuria katika uzinduzi huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili.
 
Mkuu wa mkoa wa Katavi akiongea na kukaribisha viongozi mbalimbali kutoka salam zao kutoka mikoa waliyotoka na wizara mbalimbali.
Waziri wa Ardhi na makazi Goodluck Ole Medeye akizungumza na wana Katavi na kuwaasa mambo mbalimbali kuhusu ardhi yao hasa katika suala zima la uwekezaji, ambapo amewaambia wasiuze ardhi bali waingie ubia na wawekezaji ili kunufaisha vizazi vyao pia.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda akiwasalimia wananchi wa Katavi na kuwapongeza kwa kupata mkoa mpya wa Katavi.
 
Mama Aisha Bilal akisalimia wananchi wa katavi katika sherehe hizo.
Kwaya ya Vijana ya Moravian mjini Mpanda wakitumbuiza katika uzinduai huo uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda.
 
Martha Mbogo mwimbaji wa kundi la Katavi Curture Group akiimba wakati kundi hilo lilipokuwa likitumbuiza katika uzinduzi huo mjini Mpanda.
 
Wananchi wa Mpandawakinyanyua mkono yao juu kama ishara ya kushangilia kuazinduliwa kwa mkoa wao wa Katavi uliofanyika kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
 
Wananchi wakishangilia
 
Watoto Daniel Ntwangile na Christina Benadito wakitunzwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda mara baada ya kuimba na kucheza vizuri na Kwaya ya Vijana Moravian Mjini Mpanda wanaofuatia ni Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji Dkt Mary Nagu, Mke wa Makamu wa Rais mama Zakia Bilal na Mke wa Waziri Mkuu mama Tunu Pinda wakijiandaa na wao kuwatunza
 
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwalimu wa Veta Chuo cha Veta Mpanda Trojemsi Bashato wakati alipotembelea banda la Veta.
 
Makamu wa Rais akisikiliza maelezo kutoka kwa Thomas Lemunge mfanyakazi wa kampuni ya simu ya TTCL wakati alipotembelea Banda la kampuni hiyo, kulia ni Bw Huphrey Ngowi mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni hiyo.
Makamu wa Rais Dkt. Gharib Bilal akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa huduma Mwandamizi wa benki ya Wanawake TWB BiMargaret Msengi wakati alipotembelea katika banda hilo leo.
Makamu wa Rais Akizungumza na wafanyakazi wa benki ya NMB wakati alipotembelea katika banda hilo leo njini Mpanda Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Katavi Dkt. Rajab Rutengwe.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Mizengo Pinda akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Gharib Bilal akizungumza na wana Katavi wakati wa uzinduzi wa mkoa wa mpya wa Katavi leo kwenye viwanja vya Kashaulili mjini Mpanda leo.