Release
No. 186
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba
28, 2012
STARS KUINGIA KAMBINI BAADA
YA CHALENJI
Timu
ya Taifa (Taifa Stars) inatarajia kuingia kambini baada ya kumalizika michuano
ya Kombe la Chalenji inayofanyika Uwanja wa Taifa wa Mandela ulioko Namboole
jijini Kampala, Uganda. Michuano hiyo iliyoanza Novemba 24 mwaka huu
itamalizika Desemba 8 mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Kocha Mkuu wa timu hiyo Kim Poulsen, Stars itaingia kambini kujiandaa
kwa ajili ya mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia
(Chipolopolo) itakayochezwa Desemba 23 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Baada
ya pambano dhidi ya Chipolopolo, wachezaji watapata mapumziko ya wiki mbili kabla
ya kuingia tena kambini Januari 6 hadi 20 mwakani kwa ajili ya mechi nyingine
za kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
dhidi ya Morocco.
Kim
anatarajia kuongeza kipa mmoja kwenye kikosi chake ili kuwasaidia nahodha Juma
Kaseja na Deogratias Munishi pamoja na chipukizi kadhaa kutoka timu za Taifa za
vijana za Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.
Vilevile
Kim anafuatilia wachezaji wengine kwenye timu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes)
ambayo pia inashiriki michuano ya Kombe la Chalenji ikiwa katika kundi C pamoja
na timu za Eritrea, Malawi na Rwanda.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment