Thursday, September 3, 2015

SOMA JIBU LA SERGIO BUSQUETS WA FC BARCELONA BAADA YA KUULIZWA...MAPENZI NA MPIRA BORA NINI?

Kama ulikuwa unafikiri kila mtu ana mawazo ya kuchuja hiki cha kuongea hadharani na hiki cha siri, basi sio kwa kiungo mkabaji wa klabu ya FC Barcelona ya Hispania Sergio Busquets ameingia katika headlines baada ya kauli yake aliyoitoa ya kutofautisha mapenzi na mpira kipi bora?
Sergio Busquets ambaye amezoeleka kwa umahiri wake wa ukabaji na kucheza mipira ya tackling kwa ustadi mkubwa uwanjani, amefanya kitu ambacho hakikutarajiwa na wengi hususani kumsikia akizungumza katika mahojiano ya kituo cha Tv cha Hispania Sergio Busquets alikuwa na majibu haya.
25F3799900000578-0-image-m-112_1424640947774
“katika mpira furaha ya mechi inaweza ikakaa kichwani kwa siku tatu hadi nne lakini kwa upande wa furaha katika mapenzi unaweza ukafurahi kwa dakika moja pekee baada ya hapo unasahau”>>> Sergio Busquets
Hili ni suala ambalo wengi hawakutegemea kama Sergio Busquets anaweza kulizungumza hadharani hususani katika mahojiano ya kipindi cha Tv, lakini wengine wanafikiri kauli hiyo kaitoa ili kutafuta attention kwa watu.

No comments:

Post a Comment