KUNA namna nyingine
inapaswa kufanyika....mlolongo wa recording studios na wasanii umekuwa
mrefu lakini mfumo umebakia ule ule, (kurekodi, kupeleka redioni,
halafu kusubiri malipo ya show)..Avarage airplay kwa sasa ni angalau
wiki tatu kwa hit wonder...wachache sana wanaofanikiwa kukaa zaidi ya
mwezi na hii ni wote(wakongwe na chipukizi), utengenezaji wa matangazo
unabakia kwenye rotation ya studio hazizidi Sita... Mwishowe madaraja ya
stress yanajipanga..kuanzia kwa Msanii, Producer na sasa yanahamia hadi
kwenye radio Stations..ila wahanga wakubwa ni recording Studio..mfumo
wetu hauwapi fursa ya moja kwa moja ya kurudisha mitaji yao ya
uwekezaji..mfumo wa royalty haupo na ni mgumu kuusumakisha katika mazingira
yetu..lakini sidhani kama ni tija za ukuaji kwa mtazamo wa studio pale
msanii anapolipa 400k kwa nyimbo..halafu mwimbo ukamuingizia zaidi ya
10m...kuna namna ambayo tu mfumo wa uzalishaji wa muziki Tanzania
unapaswa kujikagua na kuangalia maslahi yao...otherwise..miaka mitano
ijayo mateja wengi watakuwa ni producers kuliko wasanii
By Patrick Gondwe/Mlab Records
By Patrick Gondwe/Mlab Records
No comments:
Post a Comment