Hayati
Mwl. Julius
Kambarage Nyerere.
WANANCHI wa Tanzania
leo wanaadhimisha kumbukumbu ya miaka 15 tangu kufariki kwa Rais wa kwanza na
Baba wa Taifa hilo marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Mwalimu alifariki
nchini Uingereza alikokuwa amaelazwa kwa kusumbuliwa na maradhi ya kansa ya damu.
Na kuzikwa katika
kijijini cha Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania ambapo alizikwa Kiongozi
huyo wa zamani na rais wa kwanza wa Tanzania.
wakati maadhimisho
haya ya kitaifa yatafanyika mkoani Tabora, yakiambatana na kuzimwa kwa mwenge
wa uhuru, familia ya Mwalimu, muasisi wa Taifa la Tanzania wao wameadhimisha
misa ya kumuombea mwalimu anayetajwa kuwa mwenye heri na harakati za kumtangaza
zikiendelea, familia hiyo imesalia kijijini Mwitongo, na kudai kuwa siku hadi
siku kumbukizi hiyo inapoteza maana.
Chanzo: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment