INAWEZEKANA ukafikiri ni rahisi bosi wako kupenda unachofanya; ila kuna mambo ya msingi ambayo unatakiwa kufanya ili uthaminiwe na kupendwa.
1. Tafuta sababu ya kumpenda na kumheshimu bosi wako.
Binadamu tuna ujinga fulani wa kujifanyisha kuhusu kitu fulani au watu fulani , na mawazo yetU kutuambia kutoamini watu na hivyo hivyo hata bosI wako ni binadamu kama wewe. Usifikiri unachofanya ni mjanja kuliko bosi wako naye Anakutizama kwa namna unavyomtazama maamuzi yako kwako.
Hautaweza kuwa na mahusiano mazuri na bosi wako kama ndani ya moyo wako haumheshimu. Kumuheshimu mtu si mambo rahisi ila unatakiwa utafute kwa undani namna utakavyomheshimu na ukubali hivyo alivyo. Ili kujua namna ambavyo utamheshimu ni lazima ujibu swali lifuatalo; je ni kitu gani ambacho unakipenda kwa bosi wako? Kama ni utu wake, au utendaji wake. Tumia kitu hicho hicho utakapoulizwa na mtu mwingine na hata taaluma yake. Utagundua unapomzungumzia vizuri kwa watu wengine na heshima yako kwake inaongezeka. Bosi wako akigundua unamzungumzia vizuri kwa watu wengine, ataendelea kukuheshimu au kuboresha mahusiano yenu.
2. Timiza kila neno unaloliongea
Kama umesema utafika saa mbili na nusu fika muda huo au kabla ya muda huo. Kama umesema utafanya kazi fulani na itakuwa tayari siku fulani hakikisha imekamilika ndani ya huo muda, usidanganye au kutoa visingizio. Kama umekosea au kutokufanya kwa wakati uwe muwazi na omba msamaha kwa kuchelewesha. Jambo lolote linaloongelewa kwa siri liache huko huko.
Kama umekuwa ni mtu ambaye hautimizi ahadi zako jaribu kuongea na wenzako wakusaidie namna ambavyo unaweza kuboresha utendaji wako. Unapokuwa muwazi kuhusu mile unachotaka kufanya inakufanya use ni mtu wa kuaminika.
3. Weka mipaka na wakati mwingine ‘Sema Hapana’.
Bosi anayeelewa mambo anaheshimu watu wanaoongea ukweli hata kama ukweli huo ni kusema “hapana”.Unapoweka mipaka ambayo inawezekana na bosi wako unajipunguzia kurundikiwa kazi nyingi au mambo mengi. Unapoweza kuweka mipaka hasa wakati unapokuwa na kazi nyingi inakusaidia usiharibu utendaji wako wa kila siku. Vile vile fanya maamuzi kwa umakini hasa kuhusu kazi ambazo zinatakiwa kuisha kwa muda fulani.
4. Weka vipaumbele kwa vitu wanavyohitaji kwanza.
Kuna miradi ambayo bosi wako anaihitaji kwanza imalizike, hakikisha miradi hiyo inamalizika kwanza au unaiwekea kipaumbele na wewe. Vile vile kila hatua ya miradi hiyo hakikisha bosi wako anapata taarifa na kujua kitu gani kinaendelea. Hakikisha kila jambo lililokamilika kwenye mradi huo na waliofanya wafahamike na mabosi wao kuonyesha kwamba imefanyika kwa umoja au kama timu moja.
5. Waonyeshe kuwa marejesho ya kitu kilochofanyika unakitilia maanani sana
Bosi wako atakuhitaji kwaajili ya kutoa marejesho ya mambo yanayoendelea, hakikisha unarekodi ya vitu vyote kwa usahihi. Onyesha wapi mmetoka na mmefikia wapi na mnaelekea wapi kwa kuzingatia maoni ambayo yamekuwa yakitolewa na namna mlivyoyafanyia kazi.
6. Kuwa mwaminifu hata wanapokuwa hawapo
Uaminifu ni kitu cha msingi kwenye mahusiano uliyonayo na bosi wako, uaminifu unapovunjika unahatarisha mahusiano yenu kwa kiasi kikubwa. Hutakiwi wala kushauriwa kuwaongelea kwenye umati wa watu au kuwasema chini chini na wanapokuwa hawapo. Namaanisha hupaswi kuwa mnafiki juu yao hata kama unaona kuna kitu unastahili kuwaongelea.
Unapojenga uaminifu kwa bosi wako, unajijengea sifa kwamba wewe ni mtu unayepaswa kuaminiwa na kuwa mtu mwenye maadili mazuri kitaaluma. Kurekebisha mahusiano yaliyoharibika na bosi wako yanahitaji nguvu kubwa na yanaweza yakaathiri sehemu utakayopata kazi. Hivyo unavyojenga uaminifu si kwamba inakusaidia kazini peke yake bali unapata marafiki na watu ambao wataweza kukusaidia kwenye maisha yako ya baadaye.
No comments:
Post a Comment