WENGI wenu najua mnamkumbuka mwanadada huyu aliyewika miaka ya 1990’s, hususani kupitia filamu ya SARAFINA.
Sarafina ni jina la muusika mkuu wa kwenye filamu hiyona pia ni jina lililobeba tittle ya filamu hiyo iliyojaribu kuelezea maisha halisi ya nchini Afrika ya kusini dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Leleti Khumalo ukipenda muite Sarafina kama wengi wenu mnavyomjua, amezaliwa miaka 44 iliyopita (30 March 1970)huko KwaMashu kaskazini mwa Durban, nchini Afrika Kusini. Sarafina alianza kubainika kuwa anakipaji na mwenye nia ya kuwa muigizaji tangu akiwa mdogo na ndipo baba yake mzazi kuamua kumpeleka kwenye kikundi cha dance “AMAJIKA”.
Mnamo mwaka 1985 alijiunga na kikundi cha muziki “Mbongeni Ngema’s music”. Sarafina aliweza kuuvaa uhusika kwa kuweza kuigiza maigizo ya jukwaani na kushinda NAACP Image Award kama Muigizaji bora wa kike kwenye jukwaa mnamo mwaka 1987.
Mwaka 1992 aliweza kuungana na baadhi ya waigizaji maarufu wakiwemo; Whoopi Goldberg, Mariam Makeba na John Kani na kuweza kuigiza filamu yake iliyompa umaarufu ya Sarafina.
Mbali na kuweza kuwa muigizaji maarufu Afrika na dunia nzima, Sarafina mwaka 1993 alitoa Album yake ya Leleti and Sarafina ambayo iliweza kuuza na kumpa pato kubwa.
No comments:
Post a Comment