WANAUME
wawili waliokuwa wakituhumiwa kwa wizi wa vifaa vya gari la muigizaji
wa Fast & Furious, Paul Walker alilopata nalo ajali na kupoteza
maisha wamefikishwa mahakamani na kuhumiwa , Jumatano, August 6.
Mahakama
imewakuta na hatia wanaume hao waliotajwa kwa jina la Anthony Janow
na Jameson Witty na hakimu alipendekeza kuwa kila mmoja anapaswa
kufungwa jela kwa muda wa miezi sita.
Muendesha mashitaka alieleza kuwa Janow na Witty waliiba sehemu ya roof ya gari hilo na vifaa vingine.
Baada ya kukamatwa, watuhumiwa hao walijitetea kuwa walichukua vifaa hivyo kwa ajili ya kumbukumbu tu na sio vinginevyo.
Paul
Walker alifariki katika ajali ya gari akiwa na rafiki yake Roger Rodas,
November 30 mwaka jana huko Los Angeles, eneo la Santa Clarita.
No comments:
Post a Comment