Licha ya kuwepo wanjeshi CAR vita vingali vinaendelea.
VIONGOZI wa wakristo na waislamu duniani wanapaswa kuhusika zaidi katika vita vinavyoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya kati.
Dunia sasa inakaribia kuadhimisha miaka 20 tangu mauaji mabaya zaidi kuwahi kutokea barani Afrika kushuhudiwa nchini Rwanda mwaka 1994.
Mauaji haya ya halaiki yalikuwa ya kutisha kiasi cha kwamba yalimpokonya kila mwafrika sehemu Fulani ya utu wake kama binaadamu.
Basi kwa nini sisi waafrika tunaruhusu kuwepo kwa uwezekano wa jambo kama lile kutokea tena katika Jamhuri ya Afrika ya Kati?
Hakika, kuna wanajeshi wa Umoja wa Afrika huko , wanaosaidiana na kikosi cha Ufaransa kujaribu na kuokoa maisha ya watu wanaohofia kuuwawa na vita vya kisiasa ambavyo sasa vimechukua mkondo wa kidini.
Hata hivyo, idadi ya askari ni ya chini mno kiasi cha kwamba Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ametoa wito kwa askari wa ziada 3,000 , wakisaidiana na wanajeshi wa angani.
Waisilamu wamalazimika kutokea nchi jirani kutokana na kushambuliwa na waisilamu
Inakadiriwa kuwa hata kama Baraza la Usalama litakubalia ombi lake vikosi hivyo havitofika katika eneo hilo hadi mwezi Septemba huku vita hivi vikionekana kuongezeka sana.
Viongozi wa kidini nchini humo Imam Omar Layama-, Mchungaji Nicolas na Askofu Mkuu Dieudonne Nzapalainga walienda katika afisi za UN kumrai Ban Ki Moon kumrai kuongeza jitihada ili kuleta amani CAR.
Hatua ya viongozi wa kidini kujitolea binafsi kuunga mkono juhudi za kuleata amani katika nchi hiyo ambayo imesambaratishwa na vita pamoja inapaswa kupongezwa.
Dini zote hapa zinahusika kwani wakristo wawe wakatoliki ama wapentekoste wamekuwa wakiwavamia waislamu huku waislamu wawe ni wale wa shia au sunni wakiwashambulia wakristo.
Hivyo basi itakuwa jambo la muhimu sana kwa wakuu wa mashirika ya Kikristo na waislamu yaliyona wafuasi wake katika Jamhuri Ya afrika ya kati kutishia kuchukua hatua dhidi ya wafuasi wao watakao patikana wakishambulia wafuasi wa dini nyingine.
Rais wa mpito wa CAR Catherene Samba Panza
Kwa mafano, Papa wa kanisa katoliki ambaye ana wafuasi wengi zaidi CAR anatakiwa kutuma waraka usomwe wakati wa misa ya Jumapili na kutishia kufukuza au kutenga mkatoliki yeyote atakaye patikana akiendeza uhalifu au kueneza chuki dhidi ya watu wa dini zingine.
Vile vile uongozi wa Saudi Arabia wanapaswa kutoa Tishio kuwa ikiwa vita nchini CAR havita komeshwa mara moja hawatatoa stakabadhi za kusafiri kwa wananchi wa nchi ile ili kuenda Makkah kufanya Haji.
Itakuwa vizuri zaidi ikiwa Papa na mfalme wa Saudi watatuma wajumbe nchini CAR ,ili kuwajulisha wananchi wa CAR jinsi hawajafurahishwa na jinsi mabo yanavyo endelea katika nchi ile.
Ili kuonyesha kujitolea kwao, viongozi hawa wawili wanaweza kuunda kundi litakalofuatilia matukio katika nchi ile pamoja na kuoredhesha majina ya viongozi wa miji na vijiji vya nchi ile wanaochochea umma kutekeleza uhalifu na kueneza chuki.
Watu hawa lazima washtakiwe katika mahakama itakayoundwa na Umoja wa Africa.
BBC SWAHILI.
No comments:
Post a Comment