Monday, December 12, 2016

WATU 26 WAUAWA KUFUATIA SHAMBULIO LA KIGAIDI NJE YA UWANJA WA SOKA UTURUKI

MILIPUKO miwili imetokea kwenye mji wa Istanbul nchini Uturuki jioni ya Jumamosi, likiwemo gari lililolipuka kwenye uwanja wa soka na kuua watu 29, huku 199 wakijeruhiwa.
Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo, Suleyman Soylu amesema shambulio hilo limefanywa na mtu aliyejitoa muhanga na kwamba polisi walikuwa wamelengwa zaidi.
Milipuko hiyo imetokea masaa mawili baada ya mechi ya timu za soka za Besiktas na Bursaspor.

No comments:

Post a Comment