MKOA wa Dar es Salaam utaanza kutoa huduma za kisheria kwa wananchi wote bure kupitia wanasheria 35 ambao wamegawanywa katika wilaya zote za mkoa huo, kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.
Makonda amesema hatua hiyo itasaidia kutatua kero za wananchi ambao wamekuwa na uelewa mdogo wa sheria na kusababisha wananchi hao kukosa haki zao hususani katika masuala ya ardhi,mirathi, malalamiko ya rushwa na kufukuzwa kazi na waajili wao kinyume na sheria.
“Hawa vijana tulionao ni vichwa wanaenda kututatulia kero wananchi wa Dar es Salaam, tunawakabidhi leo kwa wakuu wa wilaya tena kwa wilaya zote tano na watapangiwa majukumu yao na niwataarifu tu wananchi kuanzia mwakani mwezi wa kwanza nenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya utawakuta wanasheria kabla hujachukua hatua yeyote ya kwenda mahali mahakamani hakikisha unapitia wanasheria wetu hawa ukiona kama unadhulumiwa.Watakupa msingi wa kisheria na hautalipa hata senti tano,” alisema Makonda.
Makonda alisema ili kutatua changamoto hizo kila Wilaya itakuwa na mawakili, Kinondoni (9), Temeke (4), Ubungo (6), Kigamboni (6) na Ilala (6).
No comments:
Post a Comment