Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Na Emmy Mwaipopo
SIKU chache baada ya agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli kupiga marufuku uuzwaji holela wa sare za jeshi hapa nchini, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira amesema wizara yake tayari imeanza kutekeleza agizo hilo.
Katibu mkuu huyo amezungumza katika mahojiano maalumu na TBC1 kuwa agizo la mheshimiwa rais limeanza kutekelezwa na kuwaelekeza magereza kufanya utafiti kwa watu wanaojihusisha na mambo ya uuzwaji wa sare.
“Tumeshawaelekeza magereza watufanyie utafiti na watuletee majina na wale watu wanaojihusisha kuuza sare za jeshi, na wahakikishe kwamba wanatekeleza agizo la mheshimiwa rais na kuhakikisha kwamba hizo nguo zinarudishwa magereza. Lakini vilevile tumeshachukua hatua za kuwataka sasa magereza watuletee mahitaji halisi ya sare za jeshi ili kusudi tuweze kuyawasilisha kwa mheshimiwa rais,” alisema Rwegasira.
No comments:
Post a Comment