Thursday, December 29, 2016

YAFAHAMU MADHARA YA PUNYETO IKIWEMO UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME

KUPIGA punyeto kwa muda mrefu ni moja kati ya vyanzo vikuu vya tatizo la la ukosefu wa nguvu za kiume. Asilimia kubwa ya vijana wenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, linasababishwa na upigaji wa punyeto kwa muda mrefu.

JINSI PUNYETO INAVYO SABABISHA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.
Unapopiga punyeto unakuwa unaiminya mishipa ya uume ambayo ndio inaufanya uume usimame. Matokeo yake unaifanya mishipa hiyo ilegee na kutokuwa na uwezo wa kusimama tena. Mishipa ya uume iliyo legea kutokana na upigaji punyeto, huleta madhara yafuatayo :
Huondoa uwezo wa mishipa ya uume kurelax. (Unapopata wazo la kufanya tendo la ndoa, mishipa ya uume ina relax , mishipa iki relax husababisha mishipa ya ateri kupanuka na kuruhusu damu kuingie ndani ya mishipa ya uume na hatimaye kuufanya uume usimame na kuwa mgumu)
Mishipa ya kiume ikishindwa ku relax husababisha mishipa ya ateri kuziba
Mishipa ya ateri ikiziba, damu haiwezi kutiririka kuingia kwenye mishipa ya uume, na hata ikitokea damu imeingia ndani ya mishipa ya uume basi huingia kiasi kidogo sana tena kwa presha ndogo sana hivyo basi hata kama uume utasimama basi utasimama ukiwa legelege sana
Mishipa ya uume ikishindwa kurelax basi haitakuwa na uwezo wa kuipush na kuiziba mishipa ya vena ambayo ndio hunyonya damu kutoka kwenye mishipa ya uume ulio simama. Matokeo yake basi, damu kidogo iliyo ingia ndani ya mishipa ya uume na kuufanya uume kusimama, hunyonywa na kutolewa nje ya mishipa ya uume ndani ya sekunde chache sana na hivyo kuufanya uume usinyae ndani ya muda mfupi sana.
Mishipaya uume kulegea
Uume kurudi ndani na kusinyaa na kuwa kama uume wa mtoto.

Tatizo la unene kupita kiasi : Tatizo la unene na uzito kupita kiasi ni miongoni mwa mambo yanayo sababisha upungufu wa nguvu za kiume. Unene kupita kiasi humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na magonjwa kama vile kisukari, presha, moyo na shinikizo kuu la damu. Na magonjwa ya kisukari, moyo,presha na shinikizo la damu husababisha upungufu na ukosefu wa nguvu za kiume, na hivyo kumuweka muhusika katika hatari kuu ya kupatwa na tatizo la ukosefu/upungufu wa nguvu za kiume.
Hivyo basi kwa wewe mwenye tatizo la unene na uzito kupita kiasi , pamoja na kutumia tiba ya nguvu za kiume, ni vyema ukafanya na mpango wa kupunguza unene na uzito wako.
Matatizo Katika mfumo wa Ubongo
Uume hauwezi kusimama bila ya kuwa na ushirikiano na ubongo. Ili mtu uume uweze kusimama, mtu lazima apate wazo la kufanya tendo la ndoa (UBONGO UNA HUSIKA HAPO ), akishapata wazo, ubungo hupeleka ishara kwenye mishipa ya fahamu iliyopo katika uti wa mgongo ambayo nayo hupeleka taarifa kwenye mishipa ya uume then uume usimama. Hivyo basi ili mtu aweze kuwa na uwezo wa kusimamisha uume wake ni lazima kuwa na mawasiliano mazuri na imara kati ya mishipa ya fahamu (ubongo), mishipa ya kwenye uti wa mgongo na mishipa ya kwenye uume. Bila ushirikiano kati ya vitu hivyo vitatu, uume hauwezi kusimama.

Magonjwa yanayoweza kuathiri ushirikiano kati ya mishipa ya ubongo na mishipa ya uume, yanaweza kusababisha kushindwa kusimama kwa uume.
Magonjwa hayo ni pamoja na kiharusi,kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), multiple sclerosis pamoja na ugonjwa wa Parkinson.

Ni vyema mgonjwa akatibiwa kwanza magonjwa hayo kabla ya kuanza kutumia dawa ya nguvu za kiume.
Mambo mengine yanayo sababisha ukosefu na upungufu wa nguvu za kiume, ni pamoja na maumivu & majeraha kwenye uti wa mgongo, chango la kiume , ngiri na matatizo katika homoni.

VIASHRIA VYA MTU MWENYE TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

Mtu mwenye tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume huwa na dalili zifuatazo ;
Kushindwa kabisa kusimamisha uume wake
Uume kusimama ukiwa legelege
Kuwahi kumaliza tendo la ndoa
Mwanaume kutokuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa katika baadhi ya staili (Mara nyingi mwanaume huyu huwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa staili moja tu). Hapa mwanaume anakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa kwa staili ya “ missionary” pekee. Ikibadilishwa staili, mwanaume anakuwa hana tena uwezo wa kusimamisha uume wake japo katika hali ya u lege lege
Uumekuto kuwa na uwezo wa kusimama wenyewe bila kushikwashikwa ama kutomaswa kwa muda mrefu.

Uume kusinyaa ukiwa ndani ya mwanamke.
Uume kusinyaa, pindi inapotokea activity yoyote ya kiungo ama ogani nyingine ya mwanaume wakati wa tendo la ndoa. Kwa mfano, wakati wa tendo la ndoa, ikitokea mwanaume amekohoa au kupiga chafya, uume nao unasinyaa.
Uume kusinyaa mara tu baada ya kutolewa ndani ya uke (Kwa mfano kama unafanya tendo la ndoa, halafu uume ukatoka nje, kitendo cha kuushika kuurudisha ndani, tayari unasinyaa)
Kutokuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa.
Kupatwa na maumivu wakati wa tendo la ndoa.

VIASHIRIA VYA MWANAUME ASIYE NA TATIZO LA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.
Mwanaume asiye na tatizo la ukosefu wa nguvu za kiume, huonyesha ishara zifuatazo ;
Uume husimama ukiwa imara kama msumari.
Hukaa kifuani kwa muda mrefu (Wastani ni kati ya dakika 20 hadi 45)
Huweza kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila misuli ya uume kuchoka.
Huweza kufanya tendo la ndoa kwa staili yoyote ile.
Uume husimama wenyewe bila kushikwa shikwa wala kuwa stimulated kwa namna yoyote ile
Kwa ufupi anakuwa na uwezo wa kufanya na kukamilisha tendo la ndoa kwa uukamilifu mkubwa.
Source: Ruwehy blog

MCHUMBA WA AY NI 'MSUPUUUUU' UNAAMBIWA…AISEE NDOA INANUKIA!!! *PICHAZ*

MWANAMUZIKI AY kwa Mara ya kwanza amemtambulisha rasmi Mpenzi wake aitwaye Remy….
Habari hii wiki hii imekuwa gumzo mitandaoni kwa wengi walikuwa wakijiuliza Ay mpenzi wake ni nani hasa baada ya Swahiba wake wa Karibu Mwana FA Kuoa…!
Picha zaidi za Remy




RAY C AJA KIHINDI ZAIDI *PICHAZ*

HUENDA huu ukawa ndio ujio mpya wa msanii mkongwe wa muziki wa bongofleva Rehema Chalamika aka Ray C baada ya misukosuko ya hapa na pale katika maisha yake ya muziki.
Muimbaji huyo ambaye amedaiwa kuweza kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya baada ya kushindwa kwa muda mrefu,wiki chache zilizopita aliweka kambi ndani ya studio ya Wanene kwa ajili ya maandalizi ya ujio wake mpya.

HUDDAH MONROE AELEZA SABABU YA KUITOSA WASAFI BEACH PARTY YA DIAMOND PLATNUMZ

WASAFI Beach Party iliyofanyika Disemba 24, Jangwani Sea Breezy jijini Dar es Salaam, ilikuwa iwakutanishe mahasimu warembo Huddah Monroe na Vera Sidika jukwaani kama mahost.

Wengi tulikuwa tukisubiri kushuhudia drama ya kufungia mwaka kutoka kwa warembo hao wa Kenya, lakini bahati mbaya fahari mmoja hakutokea.

Huddah Monroe ametumia Snapchat kuelezea sababu iliyomfanya ashindwe kuja kwenye party hiyo kuwa ni kushindwa kufikia makubaliano waliyokuwa wamejipangia na Diamond na hivyo ikamlazimu kukatisha kuja katika dakika za mwisho.

Hata hivyo Vera na mrembo mwingine wa Uganda, Anita Fabiola walikuwepo na kila kitu kilienda freshhh…

AUNTY EZEKIEL - 'SIWEZI TENA 'KU-KISS' KWENYE MUVI'

STAA wa Bongo Movie nchini mwanadada Aunty Ezekiel, amerudi upya kwenye tasnia hiyo huku akiweka wazi baadhi ya mabadiliko aliyoyafanya katika maisha yake kuwa ni pamoja na kutoweza tena 'ku-kiss' kwenye movie atakazocheza.

Aunty ambaye kwa sasa amerejea na movie mpya inayokwenda kwa jina la Chritmass Eve, amesema kilichomfanya afikie maamuzi hayo ni majukumu aliyonayo kwa sasa ya kifamilia ikiwa ni pamoja na malezi ya mtoto.

Akiwa kwenye kipindi cha FNL cha EATV Aunty amesema kuanzia sasa akiwa kwenye movie, kabla hajakubali ku-kiss na mtu kwanza anamkumbuka mtoto wake huku akitaja mabadiliko mengine kuwa ni kuweza kuigiza kama 'house girl' uhusika ambao awali aliwahi kusema hawezi kuuigiza.

"Nimechenji baada ya kuzaa, nimekuwa na mawazo tofauti, nimerudi nyuma mara mbili hata ikitokea kwenye movie natakiwa ku-kiss, najifikiria sana hivi mwanangu akiona atafikiria nini" Alisema

Amesema hivi sasa amebadilika kwa kuwa amekuwa mtu mzima na kusisitiza kuwa kwa sasa ameacha mabo yote ya kitoto aliyokuwa akiyafanya ikiwemo kuishi kwa skendo maana ameona hayana faida.

Katika hatua nyingine Aunt alisema anatarajia kupata mtoto wa pili ambaye angependa awe wa kike.

KUTANA NA MWANAMUZIKI WA BONGO ANAYETAMANI KUMUOA RAPPER WA KIKE CHEMICAL

RAPPER Stereo amedai kuwa anatamani rapper Chemical aje kuwa mke wake wa ndoa.
Stereo amesema Chemical ambaye jina lake halisi ni Claudia Lubao ni msichana anayemzimia kupita maelezo. Ameamua kufungua moyo wake kwenye mahojiano na mtangazaji wa CG FM ya Tabora, Manoni MJ wa Pili.

“Nadhani tukioana tutakuwa na familia hivi ya aina yake,” alisema Stereo na kuongeza kuwa bado hajamweleza Chemical takwa la moyo wake.

“Mimi nampenda Chemical kuliko mnavyofikiria,” amesisitiza rapper huyo.

TATHIMINI YA 'MDAU' KATIKA SHOW YA DIAMOND PLATNUMZ DAR NA IRINGA NA MTONYO ALIOINGIZA NDANI YA SIKU MBILI

KATIKA kuperuzi mitandaoni tukakutana na tathmini ya mdau kuhusu show aliyofanya Diamond Platnumz pale Jangwani - Dar na Samora Iringa.
Ulimwengu wa Habari haujahusika na kuchanganua chochote zaidi ya kurusha hewani mchanganuo huo.
Lakini nawe pia unaweza kutoa maoni yako hapo chini kuhusu Tathmini hii ya mdau!
Najua wengi mlikuwa Mkisubiri hili kwa hamu kujua tadhimini nzima ya show mbili za Diamond na Team nzima ya Wasafi zilizo Fanyika Iringa na Dar! Sasa leo nimekuleteeni tathimini ya show zote mbili alizo Fanya Diamond!
Kabla sijatoa tathimini nzima naomba ifahamike hizi show zote mbili za Diamond zilikuwa na Mdhamini mkubwa ambaye ni VODACOM huyu amedhamini show zote mbili Dar na Iringa hadi kupelekea show Hiyo kuitwa VODACOM WASAFI BEACH FESTIVAL!
Kama unajua kadhi ya mdhamini basi ujue hicho ndicho walicho Fanya Vodacom moja ya Kazi yao kubwa ni KUANDAA NA KUTEKELEZA MATAYATISHO YOTE YA SHOW ZOTE MBILI…..
kuanzia stage na kuwalipa wote walio husika kwa namna moja au nyengine ikiwa ni pamoja na malipo ya wasanii wote walio toka nje ya Tanzania chini ya SALLAM,NA BABU Tale, Malipo ya matangazo yote ikiwa ni pamoja na kuwalipa Clouds Fm na Ebony Fm walio husika katika kutangaza hii show Dar na Iringa!, Kusafirisha na kulipia sehemu ambazo show itafika na wahusika kama vile kulipia Jangwani na Samora! …. 
Kwa kuwa Diamond ndie alie na Mkataba na Vodacom huenda pia vodacom ilihusika kuwalipa Harmonize,Rich Mavoko,Rayvanny na Queen Darling (JAPO KWA HILI SINA UHAKIKA SANAA ILA MSININUKUU VIBAYA)

Kifupi katika tathimini ninayo ileta Pesa Iliyo patikana ni itaingia moja kwa moja Katika Lebal ya WCB na Itafuata mkataba unavo sema kwa ma meneja!
Tukianzia na Dar Diamond aliingiza Mashabiki zaidi ya 3000 ikiwa sehemu waliyo iindaa ilikuwa na uwezo wa kuchukua watu 1500 hivyo waliingia Mara mbili ya Mategemeo Yao! Na kulikuwa na Tiketi za aina mbili kawaida na VIP.......Tukianza na Kawaida ambayo kiingilio kilikuwa 30,000 waliuza tiketi zaidi ya 2,800
Sasa chukua 2,800+×30,000= Millioni 84+
Kwa VIP waliuza Tiketi 200+ ambapo kila tiketi iliuzwa kwa shilingi 100,000
Sasa chukua 200+x100,000=Millioni 20+

Kwa Dar Jumla ni sh.Millioni 104+
Baada ya Hapo ni Alienda kufanya Show Iringa! Iringa alifanikiwa kuingiza watu 9,000+ kwa kiingilio cha sh 10,000
Sasa chukua 9,000+×10,000=Millioni 90+
Sasa chukua Millioni 104+ + Millioni 90+ =Millioni 194+
Hiyo hela ni kaingiza kwa Siku mbili Tuu!

Kifupi hiyo ndiyo tathimini ya haraka haraka sasa kaaa wewe na Nafsi yako jiulize Ni msanii gani mwingine Tanzania hii anaweza kufanya hivyo? Ifike muda anae Jua apewe heshima yake!
Wasanii wengine waangalie Mikataba ya kuingia..watu walimlaumu Diamond kwa kutokushiriki Fiesta kwa kuwa na Mkataba na Vodacom sasa nafikiri sasa mnaelewa maana ya mkataba alio ingia nao na manufaa anayo yapata! Imagine bila vodacom Diamond hizo millioni 104+ angezigawa vipi?
Sasa kupitia Vodacom wanataka kuzindua Wasafi Festival Ambayo watazunguka mikoa 10 Tanzania wakiaanza na Dar tarehe 14 Feb! Wakiwa na Vodacom means hiyo itakuwa ni zaidi ya Fiesta!
Hiyo Tathimini
DANYA nawasilisha!

MASHABIKI WADAI FEDHA ZAO BAADA YA ALI KIBA KUSHINDWA KUFANYA SHOW DODOMA


DISEMBA 25, ikiwa ni sikukuu ya Krismasi mashabiki wa mwanamuziki Ali Kiba walibaki wakiwa wamepigwa butwaa bila kuona mtu jukwaani huku muda ukiyoyoma katika tamasha la muziki ambalo Ali Kiba alitakiwa kutumbuiza siku hiyo.


Hadi inafika saa saba usiku mwanamuziki hiyo hakuwepo ukumbini alipotakiwa kuanza kutumbuiza saa nne. Baadhi ya watu waliokuwa ndani ya ukumbi walianza kuleta vurugu na kudai fedha zao ili waondoke kwani muda ulikuwa umekwenda sana.



Akizungumza, mtayarishaji wa tamasha hilo Rashid Adam maarufu Chidi Perugina alisema tatizo kubwa lilikuwa ni suala la usafiri ambapo Ali Kiba alichelewa kufika mkoani Dodoma.



Ali Kiba alikuwa Nairobi na alitegema apande ndege awahi kufika Dar es Salaam na kisha aanze safari ya kuja Dodoma, lakini tatizo lilitokea baada ya Ali Kiba kukosa ndege ya kwanza aliyotakiwa kutoka nayo Nairobi. Ndege ya pili aliyopanda ilichelewa kufika Dar es Salaam na kuanza mchakato wa safari ya kufika Dodoma ulisababisha Ali Kiba kufika hapa saa saba usiku na madakika, alisema Rashid Adam.



Baada ya Ali Kiba kufika aliwaomba radhi mashabiki wake wachache waliokuwa bado wapo ukumbini na hakuweza kutumbuiza sababu ya uchache wao.



Baada ya tamasha hilo kusindwa kufanyika hiyo tarehe 25 Disemba, Ali Kiba anatarajiwa kutumbuiza terehe 28, Januari 2017 ambapo mashabiki walio na tiketi wametakiwa kuzitunza ili kuzitumia kwenye tamasha hilo lingine.

AZAM FC IMEWAFUTA KAZI MAKOCHA WAKE KUTOKEA HISPANIA!

AZAM FC imeamua kuwatimua makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uamuzi wa Azam umekuja baada ya mfululizo wa matokeo mabovu kwenye ligi kuu Tanzania bara msimu huu tangu ‘wahispaniola’ walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

“Uongozi wa Azam FC umewatimua makocha wao leo mchana baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili,” chanzo cha kuaminika toka ndani ya Azam FC kimeiambia shaffihdauda.co.tz.

Katika mechi 17 za VPL ambazo Hernandez alisimama kama kocha mkuu wa Azam FC, timu hiyo imeshinda mechi saba (7), imetoka sare mara sita (6) na kupoteza michezo minne (4).

Hadi sasa Azam ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa VPL ikiwa na pointi 27 baada ya kucheza mechi 17. Azam inazidiwa pointi 14 na Simba ambao ndio vinara wa ligi huku wakiwa nyuma kwa pointi 10 dhidi ya Yanga huku wakizidiwa pointi moja na Kagera Sugar.

RAIS WA BOLIVIA ANASWA AKITAZAMA VIDEO YA NGONO MAHAKAMNI…..!

RAIS wa Bolivia, Evo Morales amekumbwa na fedheha kubwa baada ya simu yae kutoa sauti zinazoaminika ni za watu wanaofanya ngono wakati akiwa katika kikao ndani ya mahakama.

Mkasa huo umetokea wakati Rais huyo akiwa katika mazungumzo na wanasheria wa kimataifa kabla ya kuchukua simu yake na muda mfupi sauti za mwanamke na miguno zinasikika kutoka kwenye simu hiyo ndipo ghafla akaitupa chini.

Video hiyo iliyovujishwa na mtandao wa LiveLeak.com  imewaacha watu wengi waliokuwa ndani ya mahakama hiyo wakicheka kufuatia tukio hilo huku baaadhi wakiishia kuguna.

PRODUCER MR T TOUCH ADAI HATAKI KUSIKIA HABARI ZA NAY WA MITEGO

MTAYARISHAJI wa muziki wa bongo fleva Mr T Touch ambaye kwa mwaka 2016 ametengeneza ngoma nyingi kali na zilizofanya vizuri katika vyombo mbalimbali vya habari amefunguka na kusema haitaji tena kumzungumzia Nay wa Mitego

Mr T Touch ambaye alikuwa ni moja kati ya maproducer wa Nay wa Mitego ambaye ametengeneza ngoma nyingi za Nay wa Mitego zilizofanya vyema sana kipindi cha nyuma alisema anawashukuru sana watu ambao wamekuwa na mchango kwake katika kufanikiwa na kupiga hatua za maendeleo.

"Nilishasema zihitaji habari za kiuhanagwa kama hizi, mimi sihitaji kumzungumzia huyo Nay wa Mitego, tuzungumzie shughuli yangu na mipango yangu kwa mwaka 2017 kwani mjini usipokuwa na shughuli watu hawawezi kukuelewa kidogo, kwa hiyo tusimzungumzie atakapokuwa na shughuli nadhani hiyo shughuli itanihusu kwa hiyo tusimzungumzie" alisikika Nay wa Mitego kwenye kipindi cha eNEWZ
#EATV

DIAMOND PLATNUMZ AWAONGOZA WATZ KATIKA WATSUPTV AFRICAN AWARDS 2016…!!!

USIKU wa December 28 2016 tuzo za WatsUp TV Africa Music Video Awards 2016 ndio zilitangazwa Accra Ghana, washindi 22 walitangazwa kupitia Press Conference wakiwemo wasanii wa Tanzania waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo kwa mwaka 2016.

Kama hufahamu WatsUp TV Africa Music Video Awards (WAMVA) ni tuzo ambazo zinaandaliwa na WatsUP TV, zikiwa na lengo la kushawishi au kuhamasisha wasanii kufanya video za viwango vya juu pamoja na ubora.
Wametangazwa washindi 22 wasanii na waongozaji wa video 170 waliyokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo wakati zinazinduliwa mwezi September 2016, kwa mujibu wa mtandao wa Zionfelix.net ni kuwa washindi watafanya show katika tamasha la Made in Africa litakalofanyika 2017 Accra Ghana.

List ya washindi wote 22 waliyotangazwa
Best Newcomer Video of the Year
Harmonize ft Diamond Platinium ( Badoo)

Best African Reggae Dancehall Video
Shatta Wale ( Chop Kiss ) Ghana

Best Afro Pop Video
Scientific Ft Quincy B (Rotate) Liberria

Best African Hip Pop Video
Iba One (Dokera) Mali

Best African RnB Video
Alikiba (Aje) Tanzania

Best African Traditional Video
Tay Grin FT 2BABA ( Chipapaa ) Malawi

Best African Dance Video
Oudy 1ER (Lokolo) Guinea

Best African Collabo Video
Diamond ft AKA (Make me sing ) Tanzania

Best African group Video
Navy Kenzo (Kamatia ) Tanzania

Best African Male Video
Diamond Platinium ft Psquare ( Kidogo ) Tanzania

Best African Female Video
Vivian Chidid ( Wuyuma) Senegal

Best African Performance
DJ Arafat (Concert a Korkogo) Cote D’Ivorire

Best International Video
Beyonce – Formation (USA)

Best East African Video
Alikiba (Aje) Tanzania

Best Central African Video
Ferre Gola ft Voctoria Kimani (Tucheze) DR Congo

Best North Africa
Ibtissam Tiskat

Best South African Video
Casper Nyvorvest (War Ready)

West Africa Video
DJ Arafat

Best African Video Director
Godfather Kidogo (Nigeria)

Best African Music of the Year
Diamond Platinium ft PSquare (Kidogo) Tanzania

Special Recognition Award Music Video Africa
Mr Eazi ft Efya (Skin Tight) Nigeria

Viewer’s Choice Awards

Designer Panda (USA)

MPENZI MPYA WA SHILOLE: 'MIMI KUCHORA TATTOO YA SHILOLE NI MOYO WANGU TU UMETAKA KUFANYA HIVI'

MPENZI mpya wa Shilole ambaye ni mfanyabiashara wa nguo, Adam, amefunguka na kuzungumzia jinsi wanavyopendana na Shilole.

Kijana huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hamwangalii Shilole alipotoka bali anaangalia hapo alipo kwa sasa na anamuomba sana Mungu ili waweze kufika mbali zaidi.

“Mimi sijafuata boost kwa Shilole bali nimefuata mapenzi na mimi naweza kusema kuwa hayo ya nyuma siyaangalii bali naangalia hapa tulipo,” alisema Adam

Aliongeza “Kwa sasa na mimi kuchora tattoo ni moyo wangu tu umetaka mimi kufanya hivi, na ninachomuomba Mungu ni kufika mbali tu na yeye basi,”

Hapo awali Shilole kabla ya kuingia kwenye mahusiano na kijana huyo alikuwa anatoka na msanii chipukizi wa muziki aitwae Hamadai.

WALIOFAULU USAILI WA KAZI SERIKALINI WATAKIWA KUOMBA AJIRA UPYA

WALIOFANYA usaili serikalini, wakafaulu lakini kabla ya kupangiwa vituo vya kazi ajira zikasitishwa; watakiwa kuomba ajira upya.

Taarifa ya Sekretarieti ya Utumishi wa Umma imesema kuwa huo ni utaratibu wa kawaida wa sekretarieti hiyo.

Aidha majina ya waliofaulu huhifadhiwa kwenye kanzi data (Database) kwa muda usiozidi miezi sita, na baada ya hapo majina hayo hufutwa.

Saturday, December 17, 2016

MRISHO NGASSA - 'MANENO NA MINONG’ONO MINGI KUHUSU UWEZO WANGU MUDA SI MREFU YATAISHA'

Mrisho Ngassa akisaini kuichezea Mbeya City fc.
HATIMAYE mchezaji Mrisho Ngassa aliyekuwa anacheza soka la kulipwa kwenye klabu ya Fanja Fc ya Oman, amemwaga wino kuitumikia klabu ya Mbeya City fc akiungana na nyota wengine 9 waliojumishwa kikosini kwenye usajili wa dirisha dogo lililofikia tamati desemba 15.
Ngassa amesaini mkataba wa mwaka mmoja utaomuweka kwenye kikosi cha Kinnah Phiri mpaka Novemba 30, 2018,na kukabidhiwa jezi namba 10 iliyokuwa inavaliwa na Joseph Mahundi aliyetimkia Azam fc ya Dar es Salaam kufuatia kumalizika kwa mkataba wake.
Baada ya kusaini mkataba huo wa mwaka mmoja Ngassa amesema anatakakufanya kazi kwa kiwango ambacho kitaipa mafanikio timu yake mpya na kuwaziba ‘midomo’ wale wanaamini kwamba soka lake limefikia tamati.
“Najua kuna maneno na minong’ono mingi kuhusu uwezo wangu, muda si mrefu yataisha kwa sababu najua nini nataka kufanya, soka ndiyo maisha yangu, naomba watu wote walio nyuma ya timu hii waniunge mkono nina uhakika tutakuwa na majibu mazuri mwisho wa msimu” alisema Ngassa

ANGALIA BRAND NEW *VIDEO* YA JOSLIN – ONLY YOU

Msanii Joslin baada ya kuwa kimya huu ndio ujio wake tena ameachia video mpya wimbo “Only You”, video imeongozwa na Rich Cash X.

PRINCE HARRY NA MPENZI WAKE MEGHAN MARKLE WAONEKANA PAMOJA KWA MARA YA KWANZA

MAISHA ya uhusiano ya Prince Harry wa Uingereza yamekuwa yakifuatiliwa kwa muda sasa huku akidaiwa kuwa na uhusiano na muigizaji Meghan Markle. Na usiku wa Alhamis hii, wawili hao walionekana hadharani na kupigwa picha kwa mara ya kwanza wakiwa pamoja jijini London.
Wawili hao walionekana wakiwa karibu kwenye mtaa ulio na watu wengi zaidi jijini humo, Shaftesbury Avenue wakitembea kwa mguu kwenda kwenye jumba la sinema la Gielgud Theatre huku wakifuatwa nyumba na mlinzi wa kifalme.
Tovuti ya The Sun imeandika kuwa walinunua tiketi za mwisho kwenda kuangalia mchezo wa The Curious Incident of the Dog in the Nighttime.
Watu wa karibu wamedai kuwa wawili hao wanapendana sana. Meghan ni muigizaji maarufu wa filamu nchini Marekani. Amekuwa akiishi na Harry, 22 kwenye nyumba iliyopo kwenye viwanja vya ikulu ya Kensington.
Meghan ni maarufu kwenye series ya Suits.


THE WEEKND AFANYA POA KWENYE CHATI ZA BILLBOARD

THE Weeknd ameendelea kufanya vizuri kwenye chati za Billboard.
Muimbaji huyo amejiwekea rekodi yake ya kuwa msanii wa tano kukaa kwa muda mrefu kwenye chati za Billboard Hot 100 akiwa amekaa kwa kwa wiki 10 mpaka sasa huku albamu ake mpya ya ‘Star Boy’ ikishika nafasi ya pili kwenye chati za Billboard Top 200.
Wasanii wengine waliowahi kukaa kwenye chati hizo kwa muda mrefu ni pamoja na Taylor Swift (31), Drake (23), Justin Bieber (11) na Adele (10).

SIKILIZA BRAND NEW *AUDIO* YA BUSHOKE & MAUA SAMA – TUPENDANE SASA

Msanii Bushoke akiwa pamoja na Maua Sama wameachia wimbo unaitwa “Tupendane Sasa”, ni wimbo mzuri wenye ujumbe wa mapenzi, Producer Ema The Boy.

PAUL MAKONDA AMWAGA WANASHERIA DAR KUSAIDIA WANANCHI BURE

MKOA wa Dar es Salaam utaanza kutoa huduma za kisheria kwa wananchi wote bure kupitia wanasheria 35 ambao wamegawanywa katika wilaya zote za mkoa huo, kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake.
Makonda amesema hatua hiyo itasaidia kutatua kero za wananchi ambao wamekuwa na uelewa mdogo wa sheria na kusababisha wananchi hao kukosa haki zao hususani katika masuala ya ardhi,mirathi, malalamiko ya rushwa na kufukuzwa kazi na waajili wao kinyume na sheria.
“Hawa vijana tulionao ni vichwa wanaenda kututatulia kero wananchi wa Dar es Salaam, tunawakabidhi leo kwa wakuu wa wilaya tena kwa wilaya zote tano na watapangiwa majukumu yao na niwataarifu tu wananchi kuanzia mwakani mwezi wa kwanza nenda kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya utawakuta wanasheria kabla hujachukua hatua yeyote ya kwenda mahali mahakamani hakikisha unapitia wanasheria wetu hawa ukiona kama unadhulumiwa.Watakupa msingi wa kisheria na hautalipa hata senti tano,” alisema Makonda.
Makonda alisema ili kutatua changamoto hizo kila Wilaya itakuwa na mawakili, Kinondoni (9), Temeke (4), Ubungo (6), Kigamboni (6) na Ilala (6).

MAHAKAMA YA UGANDA YAAMURU KUKAMATWA KWA WIZKID BAADA YA KUSHINDWA KUTOKEA KWENYE SHOW

WIZ KID anakabiliwa na kifungo cha miaka 11 jela, baada ya mahakama ya Uganda kutoa hati ya kukamatwa kwake na meneja wake, Sunday Aare.
Wizkid alishindwa kutokea kwenye show iliyokuwa ifanyike December 3 mwaka huu mjini Kampala. Kampuni iliyomlipa, Face TV, kupitia mwanasheria wake, Fred Muwema, imepata kibali cha kumkamata muimbaji huyo kwa kuchukua dola $60,000 na kushindwa kutokea kwenye show. Gharama zingine walizotoa ni brokerage fee, $5,000 na per die, $3,000 kwa muda ambao Wizkid angekaa Uganda.
Muimbaji huyo alidaiwa kushindwa kusafiri na ndege toka Marekani kwenda nchini humo kwa show hiyo.
“Between 29th August 2016 and 29th November 2016, our client (Face TV) paid to Mr. Sunday Are, Wizkid’s manager the full performance fee of US$60,000, a brokerage fee of US$5,000 and US$3,000 being per diem for the days they were going to stay in Uganda,” yanasomeka maelezo ya mlalamikaji.
Zaidi ya watu 25,000 walikuwa wamenunua tiketi kwaajili ya show hiyo. Maelezo yaliyowasilishwa mahakamani yameeleza kuwa mwandaaji wa shiw hiyo amekula hasara ya zaidi ya $300,000 kutokana na maandalizi aliyofanya.

RAIS MAGUFULI AMTEUA PROF YUNUS MGAYA KUWA MKURUGENZI MKUU NIMR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli amemteua Profesa Yunus Mgaya kuwa mkurugenzi mkuu NIMR.

MISS TZ DIANA EDWARD AWAFUNDISHA KISWAHILI MAMISS WENZIE…HIYO LAFUDHI SASA!!! *VIDEO*

Miss Tanzania 2016, Diana Edward anazidi kujikusanyia sifa nchini kwa uzalendo wake wa kuwafundisha mamiss wengine waliopo nchini Marekani kwaajili ya shindano la Miss World vitu mbalimbali kutoka nchini.
Baada ya kuwatambulisha warembo hao muziki wa Bongo Fleva na Singeli, Diana ameonekana kuwa mwalimu mzuri wa Kiswahili kwenye shindano hilo. Kupitia Instagram, Diana amepost video mbili zikiwaonesha, Miss Hondurus, Kerelyne Campigoti Webster na Miss Mexico, Ana Girault wakijifunza lugha ya Kiswahili.
“Iam happy in anyhow the outcome of the competition will be,One day left Asanteni Tanzania nawapenda nawaheshimu asante with rafiki zangu @anagirault @kerelyneiwebster@yes_sirg @derickguidotti_official Snapchat Dianaflave2 i adore you Tanzania🇹🇿❤️#missworld#missworldtanzania2016,” ameandika Diana kwenye moja kipande cha video alichokiweka kwenye mtandao huo.

HAYA NDIO MASHARTI YA DURU LA PILI LIGI KUU YA TANZANIA BARA

DURU la Pili la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza leo Jumamosi Desemba 17 kwa michezo minne kabla ya michezo mingine minne kufanyika siku ya Jumapili Desemba 18, mwaka huu.
Katika mechi za kesho, Mabingwa watetezi wa taji hilo, Young Africans SC ya Dar es Salaam itakuwa mgeni wa JKT Ruvu ya Pwani kwenye mchezo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Licha ya kwamba mwenyeji wa mchezo huo ni JKT Ruvu ambayo uwanja wake wa nyumbani mara nyingi huwa ni Mabatini ulioko Mlandizi, lakini kwa mujibu wa Kanuni ya 6 (5) na (6) ya Ligi Kuu Bara, mechi zake za nyumbani dhidi ya Simba, Young Africans na Azam FC, hufanyika Uwanja wa Uhuru.
Michezo mingine ya leo ni Kagera Sugar kuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya wakati Ruvu Shooting ya Pwani itakuwa mwenyeji wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ilihali Mwadui ya Shinyanga itaikaribisha Toto Africans ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex.
Jumapili, Desemba 18, mwaka huu Mbao FC ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza wakati Ndanda itakuwa mwenyeji wa Vinara wa Msimamo katika Ligi Kuu ya Vodacom, Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
African Lyon ya Dar es Salaam itaikaribisha Azam FC pia ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru jijijini siku hiyo ya Jumapili wakati Majimaji ya Songea itakuwa Mbeya kucheza na Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, limetoa masharti kadhaa likitaka klabu za Ligi Kuu ya Vodacom kufuata.
Masharti hayo, ni kwa klabu kutumia makocha wenye sifa kwa mujibu wa kanuni ya 72 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Mpira wa Tanzania (TFF) na kwa mujibu wa kanuni hiyo, makocha wanaopaswa kukaa kwenye benchi la Ligi kuu kwa msimu huu wasipungue sifa ya kuwa na leseni B ya CAF.
Pia kwa timu za Ligi Daraja la Kwanza na Pili, masharti ni lazima makocha wawe na sifa za kuzinoa timu hizo ambazo zimeanishwa kwenye kanuni za ligi husika.
Kadhalika, tunaagiza klabu kutotumia wachezaji wa kigeni au makocha kama hawana vibali vya ukaazi na kufanya kazi kutoka Idara ya Uhamiaji nchini iliyoko chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani.

MANENO ALIYO SEMA AUBAMEYANG KUHUSU KUJIUNGA NA REAL MADRID

MCHEZAJI wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ameweka wazi kuwa kwa wakati huu hana mpango wowote wa kujiunga na klabu ya soka ya Real Madrid.
Aubameyang ambaye ni raia wa Gabon, amesema kwamba ataendelea kusalia klabuni kwake Dortmund mpaka mwisho wa mkataba aliousaini alisema alipo ongea na waandishi wa habari.

HABARI NJEMA KWA MASHABIKI WA LEICESTER KUHUSU SCHMEICHEL

GOLIKIPA wa klabu ya Leicester Kasper Schmeichel hatimaye amerejelea mazoezi katika timu yake baada ya kuumia mkono mwezi Novemba.
Huenda akaweza kucheza mechi ya Jumamosi ya ugenini dhidi ya Stoke City.
Schmeichel, 30, aliumia mkono katika mechi ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen tarehe 2 Novemba ambayo ilimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Leicester wameshinda mechi mbili pekee kati ya nane walizocheza ligini na katika michuano ya kombe la ligi tangu wakati huo.
“Kasper alishiriki mazoezi vyema leo,” kocha wa Leicester Claudio Ranieri alisema Alhamisi wakati akiongea na waandishi.
Schmeichel msimu ulipita alichezea Leicester timu yake mechi 38 za ligi na kumaliza mechi 15 kati ya hizo bila kufungwa.