Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye maisha mapya ya ndoa mwezi Septemba mwaka huu, msanii wa Bongo Fleva, Kleyah amefunguka mipango yake ya kuachia albamu.
Baada ya kufanikiwa kuingia kwenye maisha mapya ya ndoa mwezi Septemba mwaka huu, msanii wa Bongo Fleva, Kleyah amefunguka mipango yake ya kuachia albamu.
“Nina nyimbo kama 20, tunaangalia tunaangalia nyimbo gani zitakuwa kwenye albamu hiyo ambayo itakuwa na nyimbo 12,” ameimbia Bongo5.
Kleyah ameongeza kuwa kwa sasa ameshaanza kufanya kzazi na wasanii wa nje akiwemo wa Afrika Kusini, Kenya, Nigeria na Uganda lakini pia yupo kwenye mipango ya kushoot video za nyimbo zake mbili ikiwemo aliomshirikisha Joh Makini na nyingine ya msanii wa Namibia, Chikune.
Wimbo wa ‘African Drum’ wa muimbaji huyo unaongoza kutazamwa mara nyingi kwenye mtandao wa Youtube kati ya video za wasanii wa kike Tanzania zilizotoka mwaka huu ukiwa tayari umeshatazamwa zaidi ya mara 1.3 milioni.
No comments:
Post a Comment