Mchezaji
bora wa dunia mwaka 2014 na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo (pichani)ameweka rekodi mpya katika mashindano ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya UEFA baada ya hapo jana kufunga goli 4 katika mchezo kati
ya Real na Malmo.
Magoli
ya Ronaldo yalifungwa katika dakika ya 39, 47, 50 na 58 na kufanikiwa
kufikisha magoli 11 katika michezo ya makundi rekodi ambayo ilikuwa
haijawahi kufikiwa na mchezaji yoyote.
Kabla
ya kuweka rekodi hiyo mpya, Ronaldo alikuwa na rekodi ya kufunga goli 9
katika hatua ya makundi kwa msimu wa 2013/2014 rekodi ambayo pia
ilikuwa imefikiwa na mchezaji wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano
aliyoiweka mwaka jana.
Baada
ya kufikisha magoli hayo Ronaldo anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga 11
katika michezo ya hatua ya makundi akifuatiwa na Luiz Adriano goli 9 na
Ruud Van Nistelrooy, Hernan Crespo na Filippo Inzaghi ambao walifunga
goli 8 kila mmoja.
Magoli
mengine ya Real Madrid katika mchezo huo wa Malmo yalifungwa na Karim
Benzema dakika ya 12, 24, 74 na Mateo Kovacic dakika ya 70.
No comments:
Post a Comment