Viongozi 2 wa upinzani wanyongwa Bangladesh
Bangladesh imewanyonga viongozi wawili wa upinzani kutokana na uhalifu wa kivita uliofanyika wakati wa vita vya uhuru na Pakistan mwaka 1971.
Salahuddin Quader Chowdhury na Ali Ahsan Mohammad Mujahid walinyongwa muda mfupi baada ya rais kukataa ombi lao la kutaka wasamehewe.
Bwana Chowdhury, ambaye ni mwanasiasa wa zamani mwenye ushawishi bungeni alipatika na makosa yakiwemo mauaji na mateso.
Salahuddin Quader Chowdhury na Ali Ahsan Mohammad Mujahid walinyongwa
Bwana Mujahid alikuwa mmoja wa watu mashuhuri katika chama cha kislamu nchini Bangladesh cha Jamaat e-Islami na alipatikana na hatia ya kuwaua watu wasomi.
Shirika la Human Rights Watch linasema kuwa kuna hofu kuwa kesi zao hazikuwa za haki.
No comments:
Post a Comment