Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akielezea mambo mbalimbali katika semina hiyo. kulia kwake ni afisa kutoka DIGNITY, Bi. Brenda Van Den Bergh. (Picha zote na Mpiga picha wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Tume ya haki za binadamu na utawala bora ikishirikiana na Taasisi ya haki za binadamu kutoka Denmark (DIGNITY) wamefanya semina inayohusu haki za binadamu kwa kutoa elimu kwa asasi mbalimbali kuhusu haki za binadamu.
Akizungumzia semina hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, Bahame Nyanduga amesema wameshirikiana na DIGNITY ili kutoa elimu kuhusu haki za binadamu na kuiambia serikali kuhusu umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu.
Amesema kuna baadhi ya sheria za haki za binadamu zimekuwa hazitekelezwi na serikali zaidi kupitia Jeshi la Polisi ambapo kunaonekana kuwepo na uvunjwaji wa haki za binadamu na kupitia semina hiyo watapata kutambua haki za wananchi na umuhimu wa kuzifuata.
“Tunafanya semina kushirikiana na wenzetu kutoka Denmark tunataka kutoa elimu kuhusu umuhimu wa haki za binadamu jambo hilo linajitokeza sana na tunachofanya ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza kumaliza tatizo hilo ndiyo tunatoa elimu kupitia wao ambao ndiyo wanatenda mambo hayo unaweza kuwa rahisi kumaliza tatizo hilo,” amesema Nyanduga.
Aidha ameitaka serikali kusaini mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu ili kusaidia kubana watu ambao wamekuwa hawafati sheria zilizopo na kuyataja maeneo ambayo yamekuwa kunatokea vitendo hivyo kuwa ni pamoja na magerezani na vituo vya polisi ili wakisaini vitendo hivyo vitaisha.
Kwa upande wa Mkuu wa DIGNITY, Brenda Van Den Bergh amesema taasisi yao imekuwa ikipambana kutetea haki za binadamu na wameamua kushirikiana na watu wa haki za binadamu Ili kuongeza nguvu kuoambana na vitendo hivyo na kuiomba serikali kusimamia haki za binadamu na kuwachukulia hatua wale wote wanaovunja haki za binadamu.
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi katika semina hiyo, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Yusuph Itembo amesema jeshi hilo limekuwa likifanya vikao na semina mbalimbali kwa askari wao kuhusu jinsi ya kufanya kazi zao bila kuvunja haki za binadamu.
Amesema kuna makosa yanajitokeza na kutumia fulsa hiyo kuwataka Polisi wote kufanya kazi kwa kufata sheria za nchi kama jinsi wanavyofundishwa wakati wa mafunzo.
Mmoja wa maafisa kutoka taasisi ya DIGNITY akitoa elimu ya masuala ya haki za binadamu katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Baadhi ya wadau katika seminaa hiyo..
Semina hiyo ikiendelea..
Mkutano huo ukiendelea…
Maafisa wa tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini wakiwa katika picha ya pamoja na Taasisi ya haki za binadamu kutoka Denmark (DIGNITY).
No comments:
Post a Comment