Monday, November 30, 2015

MAJIBU YA NEYMAR KUHUSU KUSAJILIWA NA REAL MADRID

Barcelona-v-AS-Roma-Pre-Season-FriendlyNeymar
Baada ya kipigo cha goli 4 kwa bila kutoka kwa wapinzani wao Barcelona, habari za chini chini zilianza kusambaa kuwa Real Madrid inataka kuweka dau kwa staa wa Barcelona, Neymar.
Tetesi hizo zilidokeza kuwa rais wa Real Madrid, Florentino Perez alikuwa tayari kumuwekea mezani Neymar kitita cha Euro Milioni 190 ili kupata saini ya nyota huyo.
Baada ya tetesi hizo mtandao wa Espnfc umeripoti kuwa Neymar amesema hayupo tayari kujiunga na Real Madrid na jambo hilo halina nafasi kwake hasa baada ya kuwepo na habari kuwa mchezaji huyo anapewa mkataba mpya.
Aidha wakati wa kipindi cha joto Manchester United ilionesha kuhitaji huduma ya mchezaji huyo ambapo taarifa zinasema ofa hiyo anaweza ipokea kama ikiwa nzuri lakini kwenda Real Madrid haiwezekani.

UKAWA KUCHUKUA JIJI LA DAR

Wafuasi wa vyama vinaonyounda Ukawa. 
Kama wingi wa madiwani katika halmashauri ndicho kigezo cha chama kumpata meya, basi safari hii jiji la Dar es Salaam litakuwa chini ya mameya kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Manispaa ya Ilala ambayo kuna karibu ofisi zote za Serikali zikiwamo wizara na Ikulu itakuwa chini ya meya wa Ukawa kwa mara ya kwanza kama ilivyo Kinondoni ambako karibu vigogo wengi wa serikali wanaishi.
Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi wa madiwani katika jiji hilo, Manispaa ya Ilala ina jumla ya madiwani 52 wakiwamo wabunge watatu wa Ukonga, Segerea na Ilala. Kati ya madiwani hao CCM ina madiwani 22, Chadema 23 na CUF saba.
Ukawa inaundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD ambavyo vimeshatoa msimamo wa kusimamisha mgombea mmoja kwenye manispaa hiyo kuwania umeya.
Hii ina maana kwamba Chadema na CUF wakiungana, watakuwa na jumla ya madiwani 30 huku CCM ikiwa na 22.
Katika Manispaa ya Kinondoni, matokeo yanaonyesha kuwa kuna jumla ya madiwani 47 ambao wakichanganywa na wabunge wa majimbo ya Kawe, Kinondoni, Ubungo na Kibamba wanafika 51.
Mchanganuo wa vyama na idadi ya madiwani kwenye mabano ni CCM (15), Chadema (28) na CUF (8).
Katika mchanganuo huo, vyama vya CUF na Chadema vikiungana katika umoja wao vitakuwa na madiwani 36 ambao watapambana na wenzao 15 wa CCM, hivyo kuweka manispaa hiyo yenye idadi kubwa ya vigogo wa Serikali mikononi mwa Ukawa.
Kwa upande wa Manispaa ya Temeke ambayo ndiyo pekee CCM ina madiwani wengi Dar es Salaam, wapo 46 wakiwamo wabunge watatu wa Temeke, Mbagala na Kigamboni.

Kati ya madiwani hao, CCM ina 29 wakati Ukawa ikiwa na jumla ya madiwani 17, Chadema (9) na CUF (8).

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA DIGNITY WAFANYA SEMINA JUU ELIMU KUHUSU HAKI ZA BINADAMU!!

DSC_1095
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Bahame Tom Nyanduga akielezea mambo mbalimbali katika semina hiyo. kulia kwake ni afisa kutoka DIGNITY, Bi. Brenda Van Den Bergh. (Picha zote na Mpiga picha wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora).
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Tume ya haki za binadamu na utawala bora ikishirikiana na Taasisi ya haki za binadamu kutoka Denmark (DIGNITY) wamefanya semina inayohusu haki za binadamu   kwa kutoa elimu kwa asasi mbalimbali kuhusu haki za binadamu.
Akizungumzia semina hiyo, Mwenyekiti wa Tume ya haki za binadamu na utawala bora, Bahame Nyanduga amesema wameshirikiana na DIGNITY ili kutoa elimu kuhusu haki za binadamu na kuiambia serikali kuhusu umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu.
Amesema kuna baadhi ya sheria za haki za binadamu zimekuwa hazitekelezwi na serikali zaidi kupitia Jeshi la Polisi ambapo kunaonekana kuwepo na uvunjwaji wa haki za binadamu na kupitia semina hiyo watapata kutambua haki za wananchi na umuhimu wa kuzifuata.
“Tunafanya semina kushirikiana na wenzetu kutoka Denmark tunataka kutoa elimu kuhusu umuhimu wa haki za binadamu jambo hilo linajitokeza sana na tunachofanya ni kuangalia ni jinsi gani tunaweza kumaliza tatizo hilo ndiyo tunatoa elimu kupitia wao ambao ndiyo wanatenda mambo hayo unaweza kuwa rahisi kumaliza tatizo hilo,” amesema Nyanduga.
Aidha ameitaka serikali kusaini mkataba wa kimataifa wa haki za binadamu ili kusaidia kubana watu ambao wamekuwa hawafati sheria zilizopo na kuyataja maeneo ambayo yamekuwa kunatokea vitendo hivyo kuwa ni pamoja na magerezani na vituo vya polisi ili wakisaini vitendo hivyo vitaisha.
Kwa upande wa Mkuu wa DIGNITY, Brenda Van Den Bergh amesema taasisi yao imekuwa ikipambana kutetea haki za binadamu na wameamua kushirikiana na watu wa haki za binadamu Ili kuongeza nguvu kuoambana na vitendo hivyo na kuiomba serikali kusimamia haki za binadamu na kuwachukulia hatua wale wote wanaovunja haki za binadamu.
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi katika semina hiyo, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Yusuph Itembo amesema jeshi hilo limekuwa likifanya vikao na semina mbalimbali kwa askari wao kuhusu jinsi ya kufanya kazi zao bila kuvunja haki za binadamu.
Amesema kuna makosa yanajitokeza na kutumia fulsa hiyo kuwataka Polisi wote kufanya kazi kwa kufata sheria za nchi kama jinsi wanavyofundishwa wakati wa mafunzo.
DSC_1081
Mmoja wa maafisa kutoka taasisi ya DIGNITY  akitoa elimu ya masuala ya haki za binadamu katika semina iliyofanyika jijini Dar es Salaam makao makuu ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. 
DSC_1117
Baadhi ya wadau katika seminaa hiyo..
DSC_1109
Semina hiyo ikiendelea..
DSC_1085
Mkutano huo ukiendelea…
DSC_1132
Maafisa wa tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini wakiwa katika picha ya pamoja na  Taasisi ya haki za binadamu kutoka Denmark (DIGNITY).

Saturday, November 28, 2015

MFAHAMU MBUNGE MWENYE UMRI MDOGO KULIKO WOTE *PICHAZ*


AMINA ABDALAH NDIE MBUNGE MDOGO KABISA MWENYE UMRI WA MIAKA 24 KATIKA BUNGE  LA 

TRA YAANZA KUNG’ATA, WAFUNGA SAPNA, WAKAMATA MAGARI UDA KISA? IPO HAPA

MAMLAKA ya Mapato Tanzania(TRA), imeanza operesheni maalumu ya kunasa wafanyabishara wakubwa ambao wengine ni wadaiwa sugu ambapo wanadaiwa na mamlaka hiyo huku wafanyabishara wa duka la simu la Sapna lililopo eneo la Posta mpya jijini Dar es Salaam likitiwa kufuli.
Operesheni ya TRA dhidi ya wanaodaiwa fedha ilianza jana maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam ambapo maofisa wa mamlaka hiyo walikuwa wanakwenda eneo moja hadi jingine na kote ambako wamekwenda wamefunga ofisi za wafanyabishara hao.
Maofisa wa TRA waliokuwa na nyaraka mbalimbali za madeni walipokuwa wanafika kwenye maeneo ya wafanyabishara hao hawakuwa na muda wa kupoteza zaidi ya kufunga ofisi huku baadhi ya maofisa hao walikuwa wakisema kuwa Hapa Kazi Tu.
Duka la Sapna ililifungwa jana saa tisa alasiri ambapo maofisa wa TRA ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao walidai kuwa wamiliki wa duka hilo ni miongoni mwa wanaodaiwa na TRA na tena ni kiasi kikubwa cha fedha.Hata hivyo hawakutaja kiwango halisi cha fedha huku wakifafanua kuwa wamiliki wa duka hilo walipewa taarifa mapema, hivyo hawakuvamia zaidi ya kutumia utaratibu maalumu.
Wakati duka hilo linafungwa wananchi walikuwa eneo hilo walijikuta wakishangaa kuona namna ambavyo wamiliki wa duka hilo wenye asili ya Asia wakibaki wameshika vichwa bila kujua la kufanya. Moafisa wa TRA mbali ya kufunga duka hilo, pia waliamua kufunga gari la mmoja wa wamiliki wa duka hilo.
Mbali ya kufunga duka hilo pia maofisa wa TRA walikwenda kwenye ofisi za Shirika la Usari Dar es Salaam (UDA), ambako nako wamekamata baadhi ya magari kutokana na kudaiwa kodi huku pia ikielezwa eneo lingine ambalo mamlaka hiyo imefanya operesheni ni eneo la Victoria ambapo kuna kampuni inayohusika na uuzaji wa redio upepo na rimoti za magari
. Kwenye eneo hilo magari manne yamechukuliwa na TRA.
Kwa mujibu wa mmoja wa maofisa wa TRA ni kwamba operesheni hiyo itaendelea tena leo huku pia ikielezwa kuna viwanda mbalimbali ambavyo vimefungwa kwa kushindwa kulipa kodi. Hata hivyo alipotafutwa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi TRA Richard Kayombo kuzungumzia operesheni hiyo hakupatikana.

DIAMOND: SITAKI KABISA KUSHIKA SIMU YA ZARI NAOGOPA KUUMIA!


Diamond Platnumz ameweka wazi kuwa yeye na mpenzi wake Zari ni watu ambao huwa hawapendi
kupekuliana simu simu zao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kusababishwa na simu za mikononi.

Simu za mikononi huwa ni moja ya chanzo cha ugomvi kwa wapenzi wengi, na tumekuwa tukisikia story za couple nyingi kuingia kwenye matatizo kutokana tu na mmoja kukuta ujumbe au picha zenye utata kwenye simu ya mwenzie hata kama haimaanishi kuwa anamsaliti.

Diamond na Zari wote ni watu maarufu ambao wana mashabiki wa jinsia tofauti, hivyo kwa kutambua mazingira ya kazi zao wameona ni bora kuaminiana bila kupekuana kwenye simu zao.


“Hicho ni kitu cha kwanza ambacho siwezi kudiriki kabisa,” alijibu Diamond alipoulizwa na Millard Ayo kama huwa anashika simu ya Zari.

Diamond aliendelea kutoa sababu za kutoshika simu yake, “sidiriki kwasababu namjua ni binadamu , unajua sometimes ukizingatia na yeye (Zari) ni mtu maarufu so sometimes watu wengine wanakuwa wanamsumbua, anaweza kukutwa na vishawishi sometimes anaweza akamjibu mtu akaitikia tu poa, kwangu mimi kikanikwaza kwasababu nampenda kwahiyo ikaniumiza, kwahiyo sitaki kabisa kushika simu yake.”

Pamoja na kwamba yeye hashiki simu ya mpenzi wake, vipi kuhusu Zari kushika simu yake?

“ Simu yangu mi haina password naiachaga tu lakini nafikiri na yeye ni mtu wa dizain hizo ambaye hataki kabisa kudiriki kushika simu yangu, yaani simu zinaleta ugombanishi sana.”

Diamond pia aliwashauri watu wengine kutoshika simu za wapenzi wao ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuepukika.

“Kwahiyo simshauri mtu kushika simu ya mpenzi wake, cha muhimu tu kuzingatia kama anakupenda anakujali anakuheshimu na umuone na hivyo vitu, lakini kwenye simu yake mwache afanye chochote anachojua yeye.” Alisema Diamond.

RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.SHEIN ATEMBELEA KIWANDWA CHA SUKARI MAHONDO LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Bw, Mahesh Patel  Mwenyekiti wa Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho Kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka Nchini India.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wakati alipowasili katika  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Bw,Afani Othman Maalim mara alipowasili katika  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi mbali mbali wa Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda  kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambachokinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (wa pili kulia) kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,(kulia ni ) Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akiangalia hatua ya ujenzi na kupata maelezo katika  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja alipofanya ziara maalum ya kutembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,
Hili ni jengo la Kiwanda cha Sukari cha Mahonda ambalo linamitambo  mbali mbali ambayo inafanyiwa ukarabati wa hali ya juu na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,na baadae mitambo hiyo iweze kuzalisha Sukari itakayouzwa ndani na Nje ya Nchi,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Sheinleo alitembelea na kuona hali ya ukarabati huo akiwa katika ziara maalum
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kulia) akipata maelezo wakati alipofuatana Meneja wa  Kiwanda cha Sukari cha  Mahonda Bw.Rajesh Kumar (katikati) alipotembelea kiwanda hicho leo,ambacho kinachofanyiwa ukarabati naKampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,kiliopo katika Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,(kulia) Meneja mradi Tushar MEHTA
Baadhi ya Mashine katika kiwanda cha Sukari cha Mahonda Wilaya ya Kaskazini B. Unguja,ambacho kinachofanyiwa ukarabati na Kampuni ya Shanta Sugar Holding Ltd kutoka nchini India,Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiambatana na Viongozi mbali mbali wa Serikali alitembelea kiwanda hicho leo
#Picha na Ikulu

MAMIA WAUAGA MWILI WA ALFONCE MAWAZO *PICHAZ*

 
Alfonce Mawazo enzi za Uhai wake
Viongozi wa Kitaifa wa Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), leo wamewaongoza mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho, za kuuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoa wa Geita Marehemu Alphonce Mawazo.
Katika shughuli hiyo baba mdogo wa Marehemu Alphonce Mawazo, Charles Lugiko na mtoto mkubwa wa Marehemu Prescious Mawazo wakatoa ujumbe mzito, huku mwanaye anayesoma darasa la nne akiahidi kuwa siku moja atarithi mikoba ya baba yake katika ulingo wa Siasa.
 
Aliyekuwa Mgombea Urais wa CHADEMA na kupeperusha bendera ya UKAWA, Mhe. Edward Lowassa akitoa salamu zake za mwisho kwa aliyekuwa M/kiti CHADEMA moa wa Geita Alphonce Mawazo aliyeuwawa kikatili kwa kukatwakatwa mapanga
Safari ya kuusindikiza Mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, imeanzia hapa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza, ambapo mwili wake ulihifadhiwa kwa kipindi cha siku takribani kumi na nne, tangu mahuti hayo yalipomkuta Novemba 14 mwaka huu.
Kituo cha kwanza cha safari hii kikawa nyumbani kwa baba yake mdogo kata ya Luchelele Nyegezi eneo la Sweya, ambapo taratibu mbalimbali za kifamilia zimefanyika, kabla ya kuanza safari ya kuupeleka mwili wake katika viwanja vya Furahisha kwa ajili ya kuagwa.
 
Mwenyekiti CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akitoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita kamanda Alphonce Mawazo ambaye ameagwa kitaifa katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanz
Taratibu hizo zilipokamilika safari ya kuelekea katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza ikawadia, ambapo katika viwanja hivyo viongozi wa Kitaifa wa (Chadema) wakaungana na mamia ya wakazi wa mkoa wa Mwanza kutoa heshima za mwisho.
Baada ya shughuli hiyo wafuasi wa Chama hicho wakaungana katika safari ya kuusindikiza mwili wa Marehemu Alphonce Mawazo, hadi mkoani Geita ambako utahifadhiwa katika Hospitali ya wilaya hiyo, kwa ajili ya kuagwa siku ya Jumapili katika viwanja vya Magereza.
Shughuli hiyo itakapokamilika Mwili wake utapelekwa katika mji mdogo wa katoro, ambako aligombea Ubunge wa Jimbo hilo kwa ajili ya kuagwa, kabla ya safari ya kuelekea Kijijini kwao kata ya Chikobe, ambako mazishi yatafanyika siku ya Jumatatu majira ya saa nne asubuhi.
  
 Familia ya Marehemu Alphonce Mawazo wakiendeshwa na mchungaji kwa ibaa fupi iliyofanyika nyumbani kwa baba Mdogo wa Marehemu.
  
Mwili wa marehemu Alphonce Mawazo ikiwasili nyumbani kwa baba mdogo (Charles Lugiko) Nyegezi jijini Mwanza ukitokea Hospital ya Bungando kwaajili ya ibada fupi
  

MAKONTENA 31 YA MAGOGO YAKAMATWA BANDARINI DAR

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,
By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Wizara ya Maliasili na Utalii imekamata makontena 31 yaliyokuwa na magogo ya mninga katika Bandari ya Dar es Salaam yenye thamani ya zaidi ya Sh300 milioni ambayo yalikuwa yanasafirishwa kwenda China.

Usafirishaji wa magogo hayo ambayo taarifa za awali zinaeleza yametoka Zambia, ilipigwa marufuku na Serikali za nchi zote mbili, hivyo biashara yake kuwa haramu.

Akizungumza na waandishi wa habari ambao pia walijionea baadhi ya makontena hayo akiwa sambamba na Balozi Mdogo wa Zambia nchini, Elizabeth Phiri, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Adelhelm Meru alisema wizara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia ofisi za Tunduma inaendelea kufuatilia nyaraka muhimu za kampuni zilizohusika.

“Usafirishaji wa magogo ulishazuiwa chini ya Sheria ya Misitu ya mwaka 1999 na yeyote anayepewa kibali cha biashara ni ile ya mbao na bidhaa nyingine za misitu ambazo zimechakatwa.

“Miti ya magogo haya inapatikana mikoa ya Mbeya na Ruvuma na baadhi ya maeneo nchini. Bado tunaendelea kujiridhisha kama hazikutoka huko,” alisema Dk Meru.

Akifafanua juu ya umuhimu wa rasilimali hizo za asili, alisema kutokana na unyeti wake Serikali iliamua kuilinda miti hiyo ili isipotee na hakuna kibali kinachotolewa kwa ajili ya uvunaji wake, hivyo washukiwa waliokuwa wanayasafirisha kwenda China watakuwa wamevunja sheria za nchi.

Pamoja na changamoto iliyopo, alisema ingawa biashara hiyo haramu inashamiri na kujitengenezea mtandao mkubwa, wizara kwa kushirikiana na TRA imejipanga kukabiliana nayo kwa nguvu zote.

“Miti hii inapatikana Tanzania na Zambia pekee. Kuna dalili ya kuwapo kwa mchezo mchafu,” alisema katibu mkuu huyo.

Licha ya hapa nchini, biashara ya usafirishaji wa magogo hayo imeharamishwa katika mataifa mengine.

Balozi Phiri alisema kuna haja ya kujiridhisha kwa nchi zote, ili hatua stahiki za kisheria zichukuliwe dhidi ya waliohusika.

“Nchi za (Umoja wa Maendeleo Kusini mwa Afrika) SADC zilisaini mkataba wa kuzuia biashara hii kutoka miongoni mwao. Zambia ni mwanachama hivyo kwa kilichotokea hata kama kampuni hizi zilikuwa na vibali vya biashara, bado hii waliyofanya ni haramu. Chochote kitachobainika kwenye nyaraka zao bado wana kesi ya kujibu mahakamani,” alisema.

Kwa kuwa watuhumiwa bado hawajafikishwa mahakamani mpaka sasa, Dk Meru alisema watatajwa baada ya taratibu za kuwachukuliwa hatua za kisheria kukamilika na kukabibidhiwa kwenye mamlaka husika.

Monday, November 23, 2015

SERIKALI YATOA MASHARTI KWA WATUMISHI WA UMMA KUSAFIRI NJE YA NCHI

OFISI ya Rais imesambaza mwongozo unaoweka masharti ambayo watumishi wa umma wanaotaka kusafiri nje ya nchi watatakiwa kutimiza ili wapewe kibali, ikiwa ni mkakati wa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kudhibiti safari holela za nje.

Rais alitoa agizo hilo baada ya kikao baina yake na makatibu wa wizara kilichofanyika Ikulu siku chache baada ya kuapishwa, akisema ofisi yake ndiyo itakayotoa kibali kwa watumishi ambao wana safari za nje.

Kwa mujibu wa waraka huo, sharti la kwanza linalotakiwa kuzingatiwa na watumishi hao ni kuomba kibali kwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Pili, kwa mujibu wa mwongozo huo, maombi yawasilishwe kwa msajili wa hazina kabla ya kwenda kwa katibu ili aweze kujenga hoja kwa kuzingatia umuhimu wake na tija itakayopatikana kutokana na safari hiyo.

Tatu, mtendaji mkuu wa shirika au taasisi lipime maombi ya safari husika ili kuona kama yana tija na yana umuhimu wa kuombewa kibali kwa katibu mkuu kiongozi, kabla ya kuwasilishwa kwa msajili wa hazina, kwa mujibu wa mwongozo huo.

Sharti la nne, lina vipengele vitano ambavyo vinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kuwasilisha hoja ya safari.

Kipengele cha kwanza ni chanzo cha safari husika, cha pili ni faida yake, tatu kwa nini ni muhimu kwa safari hiyo kufanyika na isipofanyika itaathiri vipi.

Kipengele cha nne kinachambua gharama za safari, kikiweka masharti yanayomtaka mwombaji aainishe gharama ya tiketi ya ndege, posho za safari husika, mlipaji wa gharama za safari na uwezo wa taasisi kifedha.

Kipengele cha tano cha sharti la nne kinamtaka mwombaji aeleze manufaa ya safari hiyo kwa taasisi na Taifa kama imewahi kufanyika huko nyuma.

Akizungumzia hilo, Balozi Sefue alisema ni kweli ofisi ya Rais ilituma taarifa ya kupiga marufuku safari za nje na kinachofanywa na ofisi za umma ni taratibu za safari hizo zisizoepukika.

Alisema tangu Rais Magufuli apige marufuku safari za nje, ofisi hiyo imesambaza agizo hilo katika ofisi za umma kuwa ni marufuku mtumishi wa umma kusafiri isipokuwa kwa kibali, kiwe cha Rais au cha Katibu Mkuu Kiongozi.

Alisema miongozo ya safari hizo inazitaka ofisi za umma kuhakikisha kuwa ombi la kila anayetaka kusafiri, lichujwe na kuhakikisha safari yake haiepukiki.

“Ofisi inapoleta maombi kwetu ijiridhishe kuwa haiepukiki. Maombi mengi yataishia kwenye ofisi zao, ikija kwetu inatakiwa ionyeshe wazi kuwa haiepukiki na tukipima vigezo vyake na kuona haviridhishi, tunaweza kuikataa vile vile,” alisema.

Alisema miongozo iliyobandikwa katika ofisi za umma kuhusu safari za nje ni taratibu ambazo zinafuatwa na taasisi baada ya agizo hilo kutoka ofisi ya Rais.

Ofisi za umma zilipokea barua kutoka kwa msajili wa hazina, yenye kumbukumbu namba CEA.111/372/01 iliyowasilishwa Novemba 12 mwaka huu ikielekeza kuwa Rais Magufuli ametoa zuio la jumla la safari za nje ya nchi katika utumishi wote wa umma na mihimili yake.


Zuio hilo linayagusa mashirika na taasisi zote za umma. Barua hiyo ya msajili ilieleza kuwa zuio hilo litadumu hadi pale itakavyoelekezwa vinginevyo.

TAZAMA *VIDEO* YA BINTI AMBAYE NI KIPOFU & KIZIWI KUTOKA ERITREA ALIYEHITIMU CHUO KIKUU CHA HARVARD

HABEN Girma ni mwanafunzi wa kwanza asiyeweza kuona au kuisikia, kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Harvard. Ana lengo kubwa katika maisha. Alizaliwa Carlifornia baada ya mama yake kukimbia kutoka Eritrea miaka ya 80, na kwenda Marekani kama mkimbizi.
Alifaidika kutokana na sheria ya mfumo wa elimu nchini Marekani inayowapa haki walemavu, jambo ambalo kaka yake ambaye pia haoni alinyimwa nchini kwao Eritrea. Sasa hivi ni mwanasheria anayejitahidi kuimarisha upatikanaji wa teknoljia kwa watu wasioweza kuona au kusikia.

MISA TAKATIFU YA KUMBUKUMBU YA NYAMITI LUSINDE BALTIMORE, MARYLAND

Picha ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde ikiwa kanisani siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 siku ilikofanyika misa takatifu ya kumbukumbu na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. Nyamiti alikua mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani alipatwa na mauti alipokua likizo Tanzania katika hospitali ya Kariuki alipokua amekwenda kwa matibabu baada ya kuugua ghafla alipokua huko na baadae kuaga Dunia Novemba 17, 2015.
Father Honest Munishi akiongoza misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 na kuhudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiwa ameongozana na mkewe pamoja na mwanae. 
Father Lehandry Kimario akisaidiana na Father Honest Munishi katika kuongoza misa takatifu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Mhe. Balozi Wilson Masilingi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani akiwa na mkewe Marystella Masilingi wakifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde iliyofanyika siku ya Jumapili Novemba 22, 2015 Baltimore, Maryland nchini Marekani.
Balozi Mhe. Wilson Masilingi akiongea machache jinsi alivyomjua Nyamiti na kutoa shukurani zake kwa watu mbalimbali ikiwemo kamati iliyowezesha kufanikisha misa hiyo na shukurani za pekee kwa Father Honest Munishi na Father Lehandry Kimario.
Kulia ni Sima Kazaura akisoma soma la kwanza huku akiwa amesindikizwa na Dorothy.
Kulia ni Farida Sarita akisoma soma la pili huku akiwa amesindikizwa na Dorothy.Mshereheshaji Tuma akiongea jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
Kulia ni Rosemary Commodores akisoma wasifu wa marehemu.
Kulia ni Afisa Ubalozi Suleiman Saleh akitoa salamu za Ubalozi, kushoto ni mkewe.
Dorothy akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
Sima Kazaura akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
Patrick Kajale akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Eddah Gachuma akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti.
Dj Luke akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Joyce akieleza jinsi alivyomfahamu mpendwa wetu Nyamiti
Pius Mtalemwa kiongozi wa kanisa la ibada ya Kiswahili DMV akihitimisha kwa kutoa shukurani kwa wote.
Nelson Masilingi, mtoto wa Mhe. Balozi akifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Mwambata wa Jeshi Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na Canada Col. Adolph Mutta akiwa na mkewe wakifuatilia misa takatifu ya kumbukumbu ya mpendwa wetu Nyamiti Ivan Lusinde.
Watu mbalimbali waliohudhuria misa.