Kwa mtu ambae anafatilia sana movie majina ya mastaa kama Angelina Jolie, Will Smith au Bruce Willis sio mageni kwao… hao wote ni mastaa wanaofanya poa wakiiwakilisha industry ya Holywood Marekani.
Nimepata kitu kingine kilichonivutia mtu
wangu, unajua ni rahisi kumuona mtoto wa staa wa movie kwenye Movie za
Bongo, tena urahisi wenyewe ni kwamba staa mwenyewe anaweza kumshika
mkono mwanae akaenda nae location na mtoto nae akawa na scene yake ya
kucheza.
Marekani mambo sio rahisi kiasi hicho, unaambiwa kama una mkataba na Will Smith basi ni wewe na Mr. Smith mwenyewe,
masuala ya kumuingiza mtoto wake kwenye movie hiyo ni biashara nyingine
kabisa.. yani mtoto nae lazima awe na mkataba wenye malipo yake kabisa,
baada ya kukamilika kila kitu mambo mengine yanaendelea.
Kuna movie nyingi kumbe mastaa wako na
watoto wao aisee, utaratibu ni huohuo wa Mikataba… nimeipata stori ya
baadhi ya mastaa ambao wamewahi kucheza Movie pamoja na watoto wao
Marekani mtu wa nguvu.
Angelina Jolie na Vivienne Jolie Pitt… Hapo ni mama na mtoto wake mtu wangu, wote wawili kwenye movie ya ‘Maleficent’ iliyotoka mwaka 2014.
Will Smith na mwanae wa kiume, Jaden Smith.. Wao wameonekana pamoja kwenye movie mbili, ya kwanza ni ‘Pursuit of Happyness’ iliyotoka mwaka 2006 na nyingine ni ‘After Earth’ iliyotoka mwaka 2013.. zote ni movie kali sana mtu wangu, baba na mwana wamefit poa kabisa mwanzo mwisho !!
Yes yes, bado niko na Familia ya Will Smith mtu wa nguvu.. Hapo ni mama na mwana, Jada Pinkett Smith na mtoto wake Jaden Smith sauti zao zimetumika kwenye movie ya wanyama ambayo ni animation ya ‘Madagascar: Escape 2 Africa‘ iliyotengenezwa mwaka 2008.
Billy Ray na Miley Cyrus ni mtu na baba yake, Miley
ni kama nguvu nyingi zaidi anaiweka kwenye muziki na kwenye masuala ya
movie sio sana… Hawa nao wamecheza pamoja kwenye series ya ‘Hannah Montana’.
Angelina Jollie na baba yake, Jon Voight wamecheza pamoja kwenye movie ya ‘Lara Croft: Tomb Raider‘ ambayo ilitoka mwaka 2001. Mzee Jon Voight ni staa mkubwa sana kwenye movie, aliwahi pia kucheza movie ya Anaconda na akina Ice Cube pamoja na Jennifer Lopez.
Rumer Willis na baba yake Bruce Willis waliwahi pia kushiriki pamoja kwenye movie ya ‘The Whole Nine Yards’ ya mwaka 2000 na pia ikafuatia ‘Hostage’ ambayo ilitoka mwaka 2005, wote wawili ndani.
Kuna movie yoyote kati ya hizo umeiona mtu wangu? Ipi umeipenda zaidi ukaona mzazi na mtoto wake walivyotisha ndani ya Movie?
No comments:
Post a Comment